KURASA

Thursday, November 10, 2011

KILIMO BORA CHA MINAZI




UPANDAJI
Uko wa ina mbili kuna wa vibox na wa pembetatu lakini kwa aina zote mbili umbali wa kupanda ni mita 7.6 kutoka shimo hadi shimo la mnazi, kiasi cha mashimo 175 kwa hecta huingia na kama utatumia mtindo wa pembetatu basi mashimo 13 zaidi yataingia kwa hecta.



Ukubwa wa shimo uwe futi tatu kwa kina, upana na urefu hi kwa maeneo yenye udongo mzuri na wakaida lakini maeneo yenye changarawe, mawe mawe na miamba ukubwa uongezeke hadi futi4 kwa mapana , urefu na kina, Shimo lijazwe majani kiasi cha kilo 15 – 20 unaweza kukisia kama theluthi moja ya shimo au futi moja baada ya kushindilia majani, weka juu yake kama, weka udongo wa juu (top soil) kiasi cha futi moja tena ongezea kiasi cha kilo 10 – 20 cha mbolea ya samadi.

Hakikisha haijai na kufunika shimo lote, pia kama utapata ule udongo mwekundu ambao wengi hupenda kuutumia kwenye bustani zao, pia weka humu kiasi kama utaukosa basi acha vivo hivyo, anza kumwagilia maji wiki moja kabla ya kupanda mbegu yako, kama shimo litatitia ongezea udongo wenye rutuba ya kutosha, kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanyia maji, ila kama ni sehemu ambazo hufurika kipindi cha mvua jaza udongo hadi kuweka tuta ili maji yasituame.

UPANDAJI
Ni vizuri kutumia mbegu ya nazi moja kwa moja kuliko kutumia miche, hii ni kwa sababu mbili kubwa, kwanza ukinunua mche unakuwa hujui imetoka mnazi gani, wenye ubora gani na hata uzaaji wake huujui, lakini inashauriwa kununua nazi kutoka kwenye mnazi moja kwa moja kwa kuchagua mnazi bora na unaozaa nazi nyingi na kubwa, chagua nazi kubwa zaidi kutoka katika kila mnzi bora.

Nazi ambayo haijafuliwa inakuwa na pembe tatu, moja ya pembe hizi huwa kubwa zaidi na mbili zilizobaki hufanan ukubwa, ule upande mkubwa ulazwe chini wakati wa kupandwa, na upande ule wenye kikonyo ambako nazi hujishika katika matawi ya mnazi (mahanda) ndipo ambapo huota, utatakiwa upatate au upapunguze kwa kisu ili kurahisisha kuota, wakati wa kupanda hakikisha nazi ina maji, ikiwa na maji kidogo sana usiipande, panda miezi miwili au mitatu kabla ya mvua kuanza, nazi inauwezo wa kuota yenyewe bila mvua kwa sababu ina maji ndani yake, ila baada ya kuanza kuota kama hakuna mvua ni muhimu kumwagilia ama sivyo mbegu yako itakufa.

Pia ni muhimu kutumia dawa za kuua mchwa au oil chafu wakati wa kupanda, pia kunadaadhi ya mimea ambayo mizizi yake hufukuza mchwa inaweza kupandwa pamoja na nazi yako. Kama utaamua kutumia miche basi hakikisha miche yako haipungui umri wa miezi sita tangu mbegu kupandwa ili kuzuia miche mingi kufa.

MAGONJWA YA MINAZI

- KUOZA VIKONYO
Huanza kwa majani machanga mawili ya mwanzo kubadilika rangi na kuwa njano na baadae huwa na vidoti vyeusi hutokea kwenye ukingo, majani hunyauka na kukauka na kisha sehemu ya chini linapoanzia jani huoza na kutoa harufu mbaya ambapo baadae mnazi wote hufa.

Ili kuzuia ugonjwa huu mara tu unapoona dalili za mwanzo tengeneza mchanganyiko ufuatao (gramu 100 za copper sulphate changanya na nusu lita ya maji) + (Gramu 100 za chokaa changanya na nusu lita ya maji) kila moja itengenezwe peke yake halafu kisha vichanganywe pamoja baadae kisha pulizia kwenye minazi iliyoanza kushambuliwa, kama mnazi umeshambuliwa sana ukatwe na kuchomwa moto kuzuia maambukizi zaidi. Pia pulizia mchanganyiko huu msimu wa baridi kuanzi mwezi wa 5 hadi wa 9 kwenye shamba lako kama kinga.

- KUOZA MAJANI
Majani huwa meusi kwenye ukingo na kuti likiliwa zaidi kati kati, majani machanga yakichomoza huwa dhaifu na kisha huchanguka, mnazi haufi ila mazao huwa duni kama ni mnazi unaozaa

ili kuzuia tumia dawa yoyote ya kuzuia fangasi za mimea kama Hexaconazol, Mancozeb au Dithane - M5, muhimu ukufika duka la pembejeo ulizia dawa ya kuua fangasi wa mimea utapata dawa na maelekezo ya kuchanganya usikariri haya majina ya dawa nilizotaja

Monday, November 7, 2011

MPWAPWA BREED - Mbegu bora ya ng'ombe iliyosahaulika

ASILI
Mbegu hii inatokana na mchanganyiko wa mbegu ya ng’ombe jike aina ya Zebu toka Tanzania na Red madume ya Sindhi na Sahiwal wenye asili ya india na Pakistan lakini waliotolewa nchini Kenya hii ilikuwa ni mwaka 1940 ambapo uzalishaji wa mbegu hii ulifanyika kwa mara ya kwanza katika kituo cha utafiti wa mifugo Mpwapwa Dodoma nchini Tanzania

Mwaka 1958 uboreshaji wa mbegu hii ulifanyika kwa kuongezea damu za ng’ombe wa ulaya (Bos Taurus) aina ya Ayshire na Jersey na mpaka kufikia mwaka 1960 mbegu ya Mpwapwa ikawa na na uwiano wa 20% Tanganyika Zebu 10% Boran 5% Ankole 55% Red Sindhi na Sahiwal na 10% Ayshire na Jersey. Mpaka mwaka 1971 mbegu hii ikawa na mchanganyiko wa 32% Red Sindhi, 30% Sahiwal, 19% Tanganyika Zebu 10% Boran na 10% Ayshire na Shorthorn, utagundua kwamba mbegu ya Jersey iliondolewa na kuingizwa short horn

MWONEKANO
Wanaonekana zaidi kama Sahiwal wakiwa na rangi nyekundu iliyofubaa mpaka kukooza sana au Nyekundu na nyeupe, Wana nundu kama ng’ombe wetu wa kienyeji, ngozi ya chini yashingo ijulikanayo kama DEWLAP ni ndogo zaidi ya Zebu lakini kubwa zaidi ya Ng’ombe wa kigeni, wana kiwele kikubwa zaidi ya ngombe wa kienyeji chenye kukamilika kirahisi ANGALIZO nundu na dewlap huwasaidia kupambana na mazingira ya Afrika hasa joto kali

MBEGU YA MPWAPWA


Madume yana uzito kati ya kilo 450 – 600 na majike kilo 275 – 300 wakati wa uzazi wa kwanza na huongezeka hadi kufikia kilo 450 hapo baadae, mbegu hii inauezo wa kuzalisha maziwa mengi kuliko ng’ombe wa kienyeji na pia uhimili mazingira ya joto na magonjwa kuliko Tanganyika Zebu

Serekali imeshindwa kusambaza mbegu hii kwa wafugaji na inasemekena karibia itapotea kwa sababu ng’ombe wa Mpwapwa waliobakia ni wachache sana na wanapatikana kwenye baadhi ya vituo vya utafiki kama Mpwapwa kwenyewe. Pia kuna tetesi kwamba kwa sasa hakuna MBEGU HALISI (pure breed) ya ng’ombe hawa kutokana na kuachwa wakapandana ndugu kwa ndugu (Inbreeding)

Wednesday, September 28, 2011

LEO NI SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI -

Wakati leo tunaazimisha siku ya kichaa cha mbwa duniani, ugonjwa huu hapa nchini kwetu bado umekuwa tatizo sugu. Katika wilaya ya Temeke pekee watu 202 waling'atwa na kati ya hao 19 waliugua kichaa cha mbwa. Wilaya hii inajumla ya mbwa 4500, paka 1500 ambapo kati ya hao 3418 walifanikiwa kuchanjwa.

CHANJO YA KICHAA CHA MBWA (RABIES) KWA AJILI YA WANYAMA


Ugonjwa huu huweza kumpata viumbe vingi ikiwemo binadamu, ng'ombe, mbuzi, kondoo na kadhalika, na wasmbazaji wakuu wakiwa mbwa na paka ingwa kuna baadhi ya poo (vampire bats) nao pia husambaza ugonjwa huu kwa kung'ata na kusambaza vimelea vya kichaa cha mbwa.

ugonjwa huu upo kila sehemu ya dunia ambapo kwa mwaka huua jumla ya watu 55,000 kote duniani ambapo Afrika watu 21,000 hufa kila mwana na wengine 34,000 hufa barani Asia na kwingineko

Kauli mbiu ya mwaka huu ni TUSHIRIKIANE KUFANYA KICHAA CHA MBWA KUWA HISTORIA na njia pekee ni kuwachanja wanyama wetu, na pia kuwazuia wasizurure hovyo mitaani, MUONE MTAALAM WA MIFUGO ALIYE KARIBU NAWE ILI MBWA NA PAKA WAKO WAPATE CHANJO KAMILI

WILAYA ZA NGORONGORO NA LONGIDO ZAKUMBWA NA UGONJWA HATARI WA HOMA YA MAPAFU YA NGOMBE



Wilaya za Ngorongoro na Longido ambazo zipo mpakani na Kenya zimekumbwa na ugonjwa wa mapafu wa ng'ombe, hali hii imefanya jumla ya ng'ombe milioni moja (1,000,000) kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu.

Ugonjwa huu ulitangazwa kama janga la kitaifa mnamo mwaka 2001 kwa sababau ni hatari sana na unaua ng'ombe kwa kasi sana, na unaweza kudhibitiwa kwa kuchanja mifugo mara unapoonyesha dalili za mlipuko.

Kutokana na hilo serekali imechukua hatua za dharura za kuwachanja ng'ombe wote katika wilaya ya Ngorongoro, Longido na zile za jirani kama Karatu na nyinginezo.

Historia ya ugonjwa huu inaanzia enzi za ukoloni mnamo mwaka 1905 na uliweza kudhibitiwa, lakini mnamo mwaka 1964 mwaka ambao ndio wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokea na Tanzania kuzaliwa, ugonjwa huu ulilipuka tena nchini mwetu. mnamo mwaka 1990 ugonjwa huu ulilipuka tena katika Wilaya ya Loliondo mpakani na Kenya.



Mwaka 1994 ugonjwa huu ulilipuka tena na kusambaa hadi mkoa wa Morogoro katika wilaya za kilosa na Mahenge. na mwaka 1998 ugonjwa huu ulisambaa katika mikoa 11 ya nchi yetu

Ugonjwa huu hujulikana kama contagious bovine pleural pneumonia au CBPP kwa kifupi na kama unataka mifugo yako ichanjwe wasiliana na maofisa ugani waliokaribu nawe au ofisi za wizara ya mifugo

Saturday, September 17, 2011

MBEGU BORA YA MIHOGO YAGUNDULIWA

SHAMBA DARASA LA MIHOGO




Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikishirikiana na taasisi ya kimataifa ya kilimo cha kitropiki (IITA) kwa pamoja zimezalisha aina mpya ya mbegu za mihogo zenye kustahimili magonjwa makubwa ya zao hilo. Mbegu hiyo mpya inayojulikana kama KIROBA inatoa wanga mzuri kwa ajili ya lishe na kuhimili magonjwa, pia inaweza kutoa mazao kufikia tani 35 kwa hecta.


MIHOGO BORA TAYARI KUVUNWA



Akiongea hayo Meneja wa mradi wa Shirika la chakula Duniani (FAO) BW. Raphael Laizer wakati anakagua mashamba darasa ya mihogo huko Mkuranga, alisistiza kutumia mashamba darasa ya zao la muhogo kwa ajili ya majaribio ili kupata mbegu bora ambazo zitalimwa karibu mikoa yote na ziwe zenye uwezo wa kuhumili ukame na magonjwa pia.

MIHOGO YA KUKAUSHA (makopa) KWA AJILI YA UNGA

Saturday, August 13, 2011

KILIMO CHA VITUNGUU TWAUMU - garlic





UDONGO
Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 – 6 mara mbili zaidi

UPANDAJI
Kipindi kizuri kwa upandaji ni kipindi ambacho hakuna joto hasa miezi ya May mpaka August kwa Tanzania, Unachukua kitunguu twaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 10 na kati ya mistari ni sentimeta 30. Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kungolewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu thwaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu.


UMWAGILIAJI

Kama kuna upungufu wa mvua au ni kipindi cha kiangazi basi ni vizuri ukamwagilia shamba lako, wakati mzuri wa kumwagilia vitunguu twaumu ni asubuhi na sio jioni au mchana, hii inasaidia vitunguu twaumu kujijengea uwezo wa kupambana na magonjwa, baada ya mizi miwili unaweza kupunguza umwagiliajai huku ukiangalia kwa kuchimba kidogo kama vitunguu twaumu vimezaliana vya kutosha na kuanza kukomaa, ukiona vimekomaa acha kabisa kumwagilia ili visioze

UANGALIZI
Aina nyingi za vitunguu twaumu vitakuwa kama vinatoa mbegu kwenye mmea (angalia picha chini), ingawa kuna nadharia nyingi lakini inashauriwa kukata hizi mbegu chini kabisa kwa kisu kikali na kisafi, usikate mapema mara baada ya kutokeza bali subiri mpaka mmea unapoanza kama kujikunja ndipo ukate, kwa wale wanaoacha mbegu hizi ukiamua kuzipanda kwa msimu wa kwanza zitazaa kitunguu kimoja tu cha duara lakini chenyewe ukikipanda tena kwenye mzunguko wa pili kitazaa vitunguu vingi kama kawaida



Ungoleaji wa magugu na majani ni muhimu muda wote ili kuondoa kugombea rutuba, hewa na maji shambani, kwa wenye mashamba makubwa wanaweza kutumia dawa za kemikali kama ROUNDUP na nyinginezo ili kudhibiti magugu, ingawa mimi sishauri hivyo.

MAGONJWA
Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako, inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo. Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku, kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea.

Monday, August 8, 2011

NANE NANE NA MELTON KALINGA

Leo ni siku ya wakulima yaani nane nane na maadhimisho kitaifa yanafanyika Dodoma, mimi niko na mtaalam wa Samaka Bw Melton Kalinga kwenye kituo cha Kingolwira nje kidogo ya Morogoro mjini kama km12. Kinachofanyika kwa leo ni upandishaji wa Samaki aina ya kambale

Unaanza kwa kutafuta majike makubwa yenye mayai tumboni, kisha unatafuta na Madume yaliyokomaa, ili kupandisha kwa njia ya kimaabara kambale dume inabidi umuue kisha unachukua pituitari gland na kumwingizia jike mwenye mayai aliye hai, baada ya masaa 24 mayai yanakuwa yame komaa, unayakamua toka kwa jike kisha unachanganya na mbegu za kiume toka kwa samaki uliyemuua jana yake, kwa kutumia mtambo wa maabara wenye maji ya vuguvugu unatotolesha mayai hayo kwa njia ya kitaalam.

Vifaranga wa samaki aina ya sato wanapatikana pia kwa shilingi 50 tu, kwa mawasiliano zaidi mpigie Bw Kalinga 0757891761 au 787596798

KAMBALE WAKIVULIWA KWENYE BWAWA






UKAGUZI NA UCHAMBUZI KUJUA MADUME NA MAJIKE WANAOFAA





SAMAKI JIKE MWENYE MAYAI

SAMAKI DUME



UTOAJI WA MBEGU TOKA KWA DUME

MTAMBO WA KUTOTOLESHEA MAYAI YA KAMBALE

Thursday, July 7, 2011

MATIKITI MAJI - water melon




Ili kulima matikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano Matango, maboga na maskwash.
Kwa mtu ambaye anaanza kilimo yatampa tabu kidogo tofauti na Yule ambaye ana ujuzi kidogo na mambo ya kilimo kwa sababu yanahitaji umakini kiasi.

HALI YA HEWA
Mimea hii haihimili hali ya joto kali sana, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu, inastawi vizuri kwenye kuanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa machi mpaka wa septemba .

UPANDAJI
Panda kwa kutumia Mbegu zinazouzwa madukani, ukitumia Mbegu kutoka kwenye tikiti ulilonunua linaweza likawa ni hybrid na matokeo yake matikiti yatakayozaliwa hayatakuwa bora kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Panda Mbegu yako moja kwa moja kwenye shamba, usinunue miche au kupanda Mbegu kwenyemifuko ya plastiki halafu ndi uhamishie shambani, panda Mbegu mbili sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 2 - 3 kutoka mstari hadi mstari, baada ya siku chache Mbegu zitaanza kuota, baada ya kama wiki 2 katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi, angalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Unaweza kupandishia udongo kwenye mashina na hii itasaidia kupunguza maji yasituame kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda yenye, na wakati wa kuanza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe mimea kwa kuielekezea kwenye waya na kufungia

MCHE ULIOCHIPUA


UANGALIZI
Miche ikiwa imetambaa kiasi unaweza kuweka matandazo kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu, unaweza kuweka samadi au mbolea za viwandani, mimea ikiwa midogo tumia zaidi mbolea zenye nitrojen na utumie zaidi mbolea za potasiam mara baada ya maua kutokeza hadi matunda kukomaa, matawi yakifikia urefu wa mita 2 kata mbele ilikuruhusu kutoa matawi na hivyo kupata maua mengi zaidi hatimaye mavuno zaidi

MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja, maua dume ambayo ni madogo zadi hutoka kwanza yakifuatiwa na maua jike ambayo ni makubwa zaidi, usipoona maua dume na jike kuna tatizo mfano maji kidogo yalimwagiliwa, upungufu wa viritubisho kwenye udongo, hali ya hewa ni joto/baridi sana n.k
Uchavushaji kwenye matikiti hufanyika na wadudu, kama huwaoni wakifanya kazi yao unaweza kufanya mwenyewe, muda mzuri ni wa asubuhi, unakata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi

UCHAVUSHAJI KWA MKONO


UVUNAJI MATIKITI
Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi

MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kjupata dawa sahii, dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia kwa mashambulizi ya fangasi

Sunday, June 26, 2011

LINDI - MTWARA

NYAMWAGE - MUHORO


MIKINDANI


MABIRIKA YA KUTENGENEZEA CHUMVI - LINDI


BEACH MTWARA


HIKI NDIO KIPANDE AMBACHO HAKINA LAMI KAMA KILOMETA 60

Thursday, June 16, 2011

NDANI YA RUFIJI

CHOMBO KINAKUJA



Wadau samahanini sana kwa kupotea humu kijiweni, ilikuwa ni lazima nipotee ili vitu vingine viende, lakini sasa nimerudi rasmi kwenye kijiwe changu

Wiki hii nilikuwa wilayani Rufiji nilifika sehemu kama Kibiti, Utete, Ikwiriri, Mkongwa na Nyamwage. Nililala Utete, ni sehemu tulivu na watu wake ni wakarimu kama tulivyo waTanzania wote.

Hali ya utete kwa wakati huu ni joto limepungua sana wala uhitaji kulala na feni kama DSM, kuna mbu wengi sana ni lazima ulalae na chandarua, mji hii uko pembeni ya mto Rufiji




Wakati wa kwenda tulitumia barabara ya Kilwa hadi Kibiti tukakata kulia kama unaelekea hifadhi ya Selous na kufika kijiji cha Mkongwa tukakata kulia na kuelekea kwenye kivuko cha Utete, tukasubiri pantoni baaddae tukavuka na kuingia Utete kama saa 3 asubuhi kwa kupitia njia hii ya mkato tuliokoa mwendo wa kilometa kama 40.

Utete tuliona vitu vingi maana kwanza kuna mto huu wa Rufiji, lakini bado hawajaanza kuutumia kiukamilifu, ila nina imani mambo yatakuwa mazuri maana kuna RUBADA ambayo mamlaka hii imepewa jukumu la kuendeleza bonde la Rufiji.

NAHODHA WA MV UTETE - BWANA ALLI


Wakazi wa Utete ni wakulima wa mazao kama Mpunga, mahindi na shughuli za uvuvi, pia kuna baadhi wanafuga samaki katika mabwawa binafesi ingawa ufugaji wao si mkubwa na si wakitaalam zaidi

TAA ZA BARABARANI - uswazi kwetu hamna hizi


Mji wa Utete una huduma za simu mitandao ya Voda, tigo , Airtel na Zantel, pia kuna umeme na taa mpaka za barabarani ingawa barabara hazina lami, mji una maji ya bomba lakini cha kuchekesha chanzo ni kisima waka mji unapitiwa na mto hapo hapo, maji ni ya chumvi

URITHI WETU



Usafiri ni wa mabasi mawili kwa siku moja saa 12 asubuhi na lapili kwenye saa 6 mchana ukiyakosa hayo, omba lifti kwenye magari madogo madogo ya Serekali au Binafsi au sivyo utalala.

WATAALAMU WA USHAURI KWENYE NYANJA ZOTE


Huduma nyingine ni Hospitali ndogo, pia kuna Magereza, kuna BOma lililojengwa na mkoloni linalotumika kama Ofisi ya Wilaya, Kuna posta, Nyumba za kulala wageni, sehemu za vinywaji, soko, na maduka ya bidhaa mbali mbali.

CHEMCHEM YA MAJI MOTO


Ukifika Utete ulizia wakulete huku, kwa pikipiki ni buku tu unalipia, wenyeji wanaamini maji haya ni yamaajabu na yanaweza kuytibu magonjwa, niliogopa kuwaambia hii ni volcanic feature

USAFIRI TOKA VIJIJI VINGINE KUJA UTETE


MAPATO NI MUHIMU


EWURA WAKIJA HUKU NI BALAA- PETROL INAUZWA KWENYE HIVYO VIDUMU



NILIUKUTA MTIKI IKABIDI NIUHUG



MKONGWA





KILMO KWANZA

Friday, June 10, 2011

KAJUMULO WORLD SOCCER TANZANIA LTD REGIONAL MANAGER - JOB DESCRIPTION



HI FELLOW TANZANIANS,

THANKS FOR THE OVERWHELMING RESPONSE. HERE IS A SHORT DESCRIPTION OF THE DUTIES AND REQUIREMENTS FOR THE REGIONAL MANAGER POSITIONS. I WILL BE HIRING ONE REGIONAL MANAGER FOR EACH OF THE 22 REGIONS IN TANZANIA.

1. YOU MUST BE RESIDENT FOR AT LEAST ONE YEAR IN THAT REGION. YOU MUST KNOW THE REGION AND BE VERY FAMILIAR WITH IT.
2. YOU MUST BE A UNIVERSITY GRADUATE OR HAVE AT LEAST 3 YEARS OF BUSINESS EXPERIENCE WITH EXCELLENT REFERENCES.
3. YOU MUST SPEAK, READ, AND WRITE ENGLISH FLUENTLY.
4. YOU MUST HAVE A VALID TANZANIA PASSPORT.
5. YOU MUST BE AN ACCOMPLISHED COMPUTER USER, ABLE TO USE THE INTERNET, EMAIL, SOCIAL NETWORKING (LIKE FACEBOOK, TWITTER, ETC) AND MICROSOFT WORD AND EXCEL. EXPERIENCE WITH PHOTOSHOP OR ILLUSTRATOR IS BENEFICIAL.

YOU MUST SEND A PAPER APPLICATION TO THE PO BOX ADDRESS.

DO NOT SEND AN EMAIL. I WILL NOT READ APPLICATIONS SENT BY EMAIL.

SELECTED CANDIDATES WILL TRAVEL TO THE U.S. DURING THE FIRST YEAR OF EMPLOYMENT FOR BUSINESS AND SPORTS MARKETING TRAINING.

MAIL COVER LETTER AND RESUME TO:

KAJUMULO WORLD SOCCER TANZANIA, LTD.
ATTN: HUMAN RESOURCES MANAGER
PO BOX 75935
DAR ES SALAAM TANZANIA


ok and you can you the page www.babukaju.com

Saturday, April 9, 2011

KUKU WA KIENYEJI WANAUZWA



Haya jamani kwa wale wapenzi wa kuku wa kienyeji ambao wanahitaji kuku wengi kwa mpigo ladba kwa ajili ya kuuza au kufuga uwanja niwenu sasa

Wednesday, April 6, 2011

SALAMU TOKA KWA MELTON KALINGA - MOROGORO

Wanachuo toka SUA wakipata maelezo toka kwa Bw Kalinga walipotembelea kituo cha utafiti na uzalishaji samaki Kingolwira Morogoro



Vifaranga wa sato wakiwa tayari kwa kupandikizwa kwenye bwawa



Uvunaji wa sato toka kwenye matanki ya kujengea na saruji eneo la Kingolwira


Sato waliokwisha vuliwa tayari kwa kuwa kitoweo


Kambale jike mwenye mayai tayari kwa ajili ya kufanya upandishaji na mbegu za dume kwa njia bandia ambao hufanyika nje ya mwili wa samaki hawa kwa kutumia mtambo maalum (rejea makala zangu)


Ndugu Melton Kalinga ni mtaalam wa ufugaji wa samaki toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anapatikana Morogoro Kwa mawasiliano zaidi mpigie kupitia 0757891761 au 0787596798 ili kupata maelezo kama ya ufugaji bora wa samaki, namna ya kupata vifaranga vya samaki anavyo zalisha, jinsi ya kulisha samaki wako, uchimbaji na ujenzi wa mabwawa n.k