Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
Monday, August 13, 2012
Wednesday, July 25, 2012
TARATIBU NA MASHARTI YA MKOPO WA KUKARABATI TREKTA
1. Mwombaji atajaza fomu
maalum ya maombi inayopatiakana kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa na kweye tovuti ya
mfuko. Fomu hii itapitishwa na Afisa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya husika.
2. Afisa Zana
katika Halmashauri watashirikiana na mmiliki pamoja na fundi wake kufanya
tathmini ya kiwango cha ubovu wa matrekta hayo katika maeneo yaliyoanishwa
katika taarifa ya tafiti za awali ya ukarabati. Mapendekezo yazingatie kiwango
cha matengenezo ili gharama za vipuri na fundi zisizidi kiwango cha juu
kinachoweza kutolewa.
3. Mwombaji atachagua
Mtengenezaji/Fundi kutoka kwenye orodha
ya kampuni zitakazoingia mkataba na Mfuko wa Pembejeo.
Mtengenezaji/Fundi atafanya ukarabati chini ya usimamizi na ukaguzi wa Afisa
Zana. Mtengenezaji/Fundi atawajibika kutoa hati ya kuthibitisha ubora wa
kazi/matengenezo na
gerentii ya miezi sita kwa vipuri
vilivyokarabatiwa.
4. Fomu za
maombi pamoja na vielelezo vinavyohitajika zitatumwa kwa Mkurugenzi Mtendaji,
Mfuko wa pembejeo.
5. Dhamana ya
mkopo huu ni kadi halisi ya trekta na mali nyingine isiyohamishika.
6. Muda wa mkopo ni
mwaka mmoja na nusu kwa riba ya asilimia nane (8%).
7. Mwombaji sharti
awe tayari kutoa huduma ye kukodisha trekta hilo kwa wakulima wenzake
TARATIBU NA MASHARTI YA MKOPO WA KUNUNUA TREKTA JIPYA
1.Mwombaji
atajaza fomu maalum ya maombi inayopatikana katika Ofisi za kilimo za
Halmashauri za Wilaya na Makao makuu ya Mfuko wa Pembejeo, jijini Dar-es-salaam
na katika tovuti ya wizara ya kilimo.
2. Fomu za
maombi zilizojazwa na kuambatanishwa na vielelezo vinavyohitajika
zitapitishwa/kuidhinishwa na Afisa Kilimo wa Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya husika na baadaye kutumwa mapema kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo.
3. Mikopo ya
kununua matrekta inatolewa na Mfuko wa Pembejeo, baadhi ya benki na taasisi za
fedha na SCCULT
(T) Ltd. kwa niaba ya Mfuko, mwombaji sharti atimize yafuatayo:-
a. Awe na dhamana yenye hati
miliki isiyohamishika iliyoandikishwa kwa jina la mwombaji.
b. Awe na shamba binafsi
lisilopungua hekta 50 na awe tayari kutoa huduma ya kuwalimia wakulima wengine
c. Awe tayari kutekeleza
masharti yote ya Mfuko wa Pembejeo au taasisi ya fedha na SCCULT yanayohusu
mkopo wa ununuzi wa trekta jipya.
d. Awe tayari kulipa asilimia
moja (1%) ya mkopo kama gharama za nyaraka za mkopo na kusajili trekta
kwa pamoja kwa jina lake na Mfuko
e. Riba inayotozwa ni
asilimia nane (8%) na marejesho hufanyika kwa muda wa miaka
mitatu kila baada ya miezi mitatu.
KILIMO BORA CHA MPUNGA CHA UMWAGILIAJI
Maandalizi sahihi ya shamba ni jambo la msingi katika kuboresha kilimo cha umwagiliaji wa mpunga. shamba lisipoandaliwa vema husababisha mbinu bora zinazoshauriwa kutoonyesha matokeo katika kiwango kinachotarajiwa hasa katika
uzalishaji. Kimsingi maandalizi ya shamba yanatakiwa yafanyike kwa usahihi
na kwa wakati katika mtiririko unaotakiwa. Zifuatazo ni hatua saba muhimu na za msingi katika kilimo cha mpunga
1. KUSAFISHA SHAMBA
Safisha shamba mapema kabla ya msimu kuanza. Kusanya na kuangamiza visiki na takataka
nyingine zote. Masalia ya mazao yanaweza kutumika kutengeneza mbolea ya mboji. Inapobidi tumia moto kwa uangalifu sana maana moto unaweza kuharibu mazingira, unaua wadudu rafiki, unaharibu udongo na kuteketeza mboji.
2. KULIMA
Kulima husaidia kupunguza kiasi cha magugu, huruhusu mzunguko mzuri wa hewa na maji, hurahisisha mizizi kupenya na
kuchanganya masalia ya mazao kwenye ardhi. Wakati wa kulima uangalifu unahitajika ili kuzuia kuharibu
usawa wa ardhi. Kina cha kulima kiwe kati ya sentimeta 10 na 15. Ili
kurahisisha na kuharakisha kazi ya kulima ni vema kutumia zana/mashine rahisi
kama Trekta la mkono na wanyamakazi
3. KUKARABATI/KUJENGA MAJARUBA
Baada ya kulima hakikisha kuwa kingo za jaruba zimekarabatiwa ili kuweza kuhifadhi maji vema. Kama ni shamba jipya, ujenzi wa kingo za jaruba ufanyike kwa kufuata utaalamu unaotolewa. Kingo imara ni muhimu kudhibiti vema maji shambani.
4. KUVURUGA
Weka maji shambani kiasi cha sentimeta 3 hadi 5 juu ya usawa
wa ardhi ili kukamilisha vema uvurugaji. Jembe la mkono linatumika lakini ili kurahisisha na kuharakisha kazi hii ni vema kutumia trekta la mkono au wanyamakazi. Unapotumia wanyamakazi au trekta la mkono weka maji shambani si zaidi ya siku moja kabla. Shamba lililovurugwa vema huiwezesha mizizi ya miche kupenya vema ardhini.
5. KUSAWAZISHA SHAMBA
Baada ya kuvuruga ni lazima kuhakikisha kwamba shamba limesawazishwa vema. Shamba lililosawazishwa vema linaruhusu usambaaji mzuri wa maji. Wakati
wa kusawazisha kina cha maji kiwe kiasi cha sentimeta 3-5 juu ya usawa wa ardhi Ili kurahisha kazi hii tumia reki ya ubao ili kuvuta udongo kutoka sehemu zilizoinuka kuelekea sehemu zilizo bondeni
6.VYANZO NA ATHARI ZA UPOTEVU WA MAJI YA UMWAGILIAJI
Ili kupata maji ya kutosha inabidi kuhakikisha kwamba upotevu wa maji ya umwagiliaji unapungua kwa kiwango kikubwa na wakulima wanamwagilia maji kwa kiasi kinachohitajika bila kuzidisha
kiwango.
Vyanzo vya upotevu wa maji ya umwagiliaji katika skimu za mfano ni pamoja na:
• Maji yanayopotea kwenye mifereji mikuu, ya kati na ile midogo ya kusambaza maji mashambani.
• Maji yanayopotea
mashambani wakati wa kumwagilia.
Upotevu wa maji kwenye mifereji mikuu, ya kati na ile ya kusambaza maji unasababishwa na aina ya udongo uliotengeneza kingo za mfereji, uchafu na matengenezo hafifu ya mifereji.
Katika baadhi ya skimu upotevu wa maji kwenye mfereji mkuu uliosababishwa na kuvuja maji kwenye tuta la
mfereji mkuu na kunywea chini ya ardhi ulikuwa mkubwa kiasi cha
kuathiri upatikanaji wa maji kwenye mashamba yaliyoko
mbali na banio.Vilevile athari nyingine ilikuwa ni maji mengi kuingia sehemu yasikohitajika na kusababisha
tatizo la maji kutuama kwa muda mrefu.Hivyo wakulima wanashauriwa kupunguza
upotevu huu wa maji kwenye mfereji kwa kujengea na kusakafia. Upotevu wa maji mashambani wakati wa kumwagilia unasababishwa na kuvuja kwenye tuta linalozunguka jaruba, kunywea chini na kuzidisha kiwango cha maji ya kumwagilia kinachotakiwa. Hii mara nyingi inasababishwa na utengenezaji
mbovu wa jaruba. utengenezaji wa majaruba na uimarishaji wa kingo
za jaruba umesaidia kupunguza upotevu wa maji kwa kiwango kikubwa na hatimaye kuongeza mavuno na kipato cha mkulima.
7. UPANDIKIZAJI MPUNGA
Ili kupata mavuno mengi na kukifanya kilimo cha mpunga kuwa cha faida ni muhimu
wakulima kuzingatia mbinu hii muhimu na kuachana na kilimo cha kiholela kwa kumwaga mbegu moja kwa moja shambani. Aidha kwa wakulima wanaofuata kanuni hii wamepata mafanikio makubwa.
Faida zinazopatikana kwa kupandikiza mpunga
• Mkulima huweza
kuchagua miche bora na mizuri ikiwa
kitaluni.
• Miche hukua haraka
na yenye afya .
• Kiasi kidogo cha
mbegu huhitajika.
• Mavuno huwa mengi.
Njia za kupandikiza
miche ya mpunga
Zipo njia kuu mbili za kupandikiza miche ya mpunga, nazo ni:
• Kupandikiza kwa
mistari
• Kupandikiza bila ya
kufuata mistari (Mchaka mchaka).
Aidha kati ya njia hizi mbili, njia ya kupanda kwa mistari ndiyo inayopendekezwa.zaidi. Pamoja na kwamba upandikizaji wa mistari unahitaji nguvu kazi zaidi, njia hii imeonyesha
kuwa na mafaniko mengi ikilinganishwa na kupandikiza kiholela. Shamba lililopandwa kwa mistari ni rahisi kupalilia kwa kutumia kipalizi cha kusukuma kwa mkono. Pia ni rahisi kwa mkulima kupanga idadi ya mashina/mimea kwa eneo kwa uchagua nafasi aitakayo itakayompa mazao
mengi.
Uandaaji wa miche
Kabla ya kupandikiza miche shambani ni muhimu kufanya
maandalizi yafuatayo:
• Inashauriwa kumwagilia
miche kwanza ili kupata urahisi wa kungo’a
• Ili kuzuia miche
isikatike ovyo, miche ing’olewe kwa kushikwa chini zaidi ya shina
• Epuka kung’oa miche
mingi kwa wakati mmoja
• Miche ifungwe
kwenye mafungu madogo madogo ili kurahisisha usafirishaji na upandikizaji shambani
• Miche bora tu ndio
ichaguliwe. Sifa za miche bora
• Iwe na kimo
kinacholingana,
• Iwe na majani
mafupi yaliyosimama, yenye mizizi mingi
na yenye afya, isiyoshambuliwa na wadudu wala magonjwa,
Jinsi ya kupandikiza miche
• Miche ishikwe kwa vidole vitatu kama inavyoosha kweye picha
chini
• Pandikiza kati ya
miche 2 -3 kwa kila shina
• Kwa mafanikio zaidi, miche ipandikizwe katika kina cha sentimita 2-3.
Friday, July 20, 2012
KUKU WA KIENYEJI WANAUZWA
Kuku wa kienyeji wenye uzito kati ya kilo moja na nusu na kuendelea wanauzwa bei ni kuanzia shilingi elfu kumi mpaka elfu kumi na tano tu (10,000 - 15,000) kutegemeana na ukubwa wa kuku mwenyewe kuku wanapatikama wengi kama 200,
Pia mayai ya kuku wa kienyeji yapo , kwa trei moja ni shilingi elfu kumi tu (10, 000)kwa maulizio piga namba 0755-462970 ulizia Livin Matabaro
Tuesday, July 3, 2012
SUMA JKT NA SABA SABA
FARMTRAC trekta bora kwa ajili ya kilimo cha kisasa
Kuku wazazi (parent stock) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga vya kuku bora wa mayai na wa kienyeji (improved breed)
Battery cages kwa ajili ya kufugia kuku wa mayai, mfumo huu hutumia sehemu ndogo tu ya banda kufuga kuku wengi, na ni rahisi kwa sababu mifumo ya maji na chakula unaweza kuweka inayojiendesha yenyewe (automatic) na pia ni rahisi kukusanya mayai na haya vunjiki hovyo
Kuku wazazi (parent stock) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga vya kuku bora wa mayai na wa kienyeji (improved breed)
Battery cages kwa ajili ya kufugia kuku wa mayai, mfumo huu hutumia sehemu ndogo tu ya banda kufuga kuku wengi, na ni rahisi kwa sababu mifumo ya maji na chakula unaweza kuweka inayojiendesha yenyewe (automatic) na pia ni rahisi kukusanya mayai na haya vunjiki hovyo
Hawa ni bata wa kawaida
Bata mzinga
FSABA SABA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Hii ni sehemu ya kwanza mara baada ya kuingi akwenye banda hili ambapo utakutana na sanamu kadhaa za wanyama wa mbugani
Hii ni sehemu ya nyuma kwenye wakala wa mbegu za miti, hii ni baadhi ya miche inayopatikana kwenye vitalu vyao
Mzinga wa nyuki wa kufugwa, huu ni mzinga wa kisasa kabisa
Mdau akinunua mbegu za miti ya misoji (mitiki) kutoka kwa wakala wa mbegu za miti (TTSA) kwa ajili ya kuotesha mwenyewe
Hii ni sehemu ya nyuma kwenye wakala wa mbegu za miti, hii ni baadhi ya miche inayopatikana kwenye vitalu vyao
Huu mti unaitwa msabuni au mhalinta
Mzinga wa nyuki wa kufugwa, huu ni mzinga wa kisasa kabisa
Mdau akinunua mbegu za miti ya misoji (mitiki) kutoka kwa wakala wa mbegu za miti (TTSA) kwa ajili ya kuotesha mwenyewe
PAN 4M-19 MBEGU BORA YA MAHINDI
aka MKOMBOZI mbegu bora kutoka kampuni ya mbegu ya PANNAR, mbegu hii ya chotara inafaa sana kwenye maeneo mbali mbali ya ukanda wa chini na kati wenye mvua kidogo na inavumilia sana ukame. mbegu hii ndiyo mkombozi wauhakika na itakufanya uepukana na njaa haswa katika kipindi hiki ambacho hali ya hewa haitabiriki
- Punje zake ni ngumu za zinakoboleka vizuri, haishambuliwi na wadudu kwa urahisi na inauwezo wa kutoa magunia 25 kwa ekari moja
- Inafaa kwenye maeneo mengi yenye hali mbaya ya hewa hasa ukame
- Inavumilia sana magonjwa ya majani kama maize strips
- Ni matamu sana kwa kuchoma
- Inakomaa mapema sana siku 90 - 100 tangu kupanda
- Inauwezo wa kutoa mahindi mawili mawili
Kwa wanaokwenda saba saba watembelee nyuma ya banda la PTA kwenye bustani za jeshi la magereza
na kwa mawakala wa jumla wasiliana nao kwa mawasiliano haya
P.O.BOX 10677 Arusha Tanzania
Tel +255 (0)27 250 4669
Fax +255 (0) 27 254 4669
info@pannar.co.tz
www.pannar.com
Wednesday, June 27, 2012
KILIMO BORA CHA MIPAPAI
MAHITAJI
Hali ya hewa inayofaa
kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha
maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya
kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu,
kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama
hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza
ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni
Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani
huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga
upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia
inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita
10 mpaka 20 juu zaidi
Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza
kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao
hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa
Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya
michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti na
mboga mboga yanaweza kulimwa
Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike na yenye jinsia zote (multiplesex/hermaphrodite)
ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na
mapapai mafupi sana
MBEGU
Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na
kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha
hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja
KUOTESHA MBEGU
Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia
miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu
zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo wenye rutuba au
pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 – 27 na itachukua
kati ya wiki 1 – 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3. Panda mbegu
zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta
15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya
copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na
fangasi
UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA
Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea
ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia
kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 5 kila shimo maana miche mingine
inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume
KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU
Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 –
40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta
40 – 60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na
shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni
mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha
KUPUNGUZA MIPAPAI
Baada ya miezi 3 – 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na
hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume,
mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume ibaki
mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe
RUTUBA YA UDONGO
Weka kiasi chakilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa
mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama
matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu
usipotee.
MAGUGU
Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka
ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka
kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka
matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu
UANGALIZI
- Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako
- Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.
- Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu
- Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike
- Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3) kwani mpapai unapo kuwa mkubwa basi rutuba yote huishia kwenye mti wenyewe
Tuesday, June 19, 2012
UTITIRI - WADUDU WASUMBUFU WA MIKOROSHO
Utitiri wa mikorosho
au kwa jina lingine thrips (Thrips rubrocinctus), ni wadudu wadogo sana wenye
mwili laini na rangi kati ya njano, kahawia au nyeusi. Utitiri wakubwa
(adults) hutambulika kwa kuwa na mabawa na mwili wa kahawia (dark brown)
au mweusi, pamoja
na upito (band) wa rangi nyekundu
kifuani. Wanaonekana vizuri kwa kutumia kikuzia umbo (lens).
Katika kipindi kirefu, utitiri ulikuwa ukionekana katika maeneo mengi yanayolimwa korosho, lakini
athari zake zilikuwa ndogo. Katika miaka ya hivi karibuni wameonekana kwa
uwingi na kuleta hasara kubwa hasa katika
tarafa za Lisekese na Chikundi
wilayani Masasi. Pia mashambulizi ya wadudu hawa yameonekana katika wilaya za
Nachingwea na Newala kwa kiwango kidogo.
Inakisiwa kuwa uongezekaji wa
wadudu hawa husababishwa na
mabadiliko ya hali ya hewa.
MZUNGUKO WA MAISHA
Utitiri wakubwa hutaga mayai katika sehemu yachini ya majani. Mayai yanaanguliwa baada ya siku 3
hadi 4 na kutoa vijititiri
vidogo sana (larva I) ambavyo
huwa ni vyepesi sana. Huingia
hatua ya pili (larva stage II)
baada ya siku 7 hadi 8. Hatua hizi
ndizo ziletazo uharibifu mkubwa maana
ndizo hatua za ulaji na ulafi wa hali ya juu. Baada ya wiki moja tena, ndipo
hutokeza hatua ya kwanza ya “ninfu” (Nymph stage I) na hatua yake ya pili baada
ya siku 3 hadi 4. Katika hatua hizi mbili (nymph stages), vijidudu hivi
havitembei wala kula chakula bali hukaa mahali pamoja, hasa
kwenye ardhi. Hatua hii ya “ninfu” hudumu kwa siku 11 hadi 12 kabla ya kupevuka
na kuwa utitiri wakubwa (adults). Hivyo Mzunguko wa maisha yao toka yai hadi
kupevuka ni mwezi mmoja. Utitiri hushamiri sana wakati wa kiangazi mara tu baada
ya mvua, hasa kati ya mwezi June
na Oktoba. Utitiri hupungua kabisa wakati wa mvua, hata hivyo huvuka msimu hadi
mwingine kama utitiri wakubwa.
MASHAMBULIZI
Utitili wachanga pamoja na
wakubwa, hushambulia upande wa chini wa majani hasa yaliyokomaa,
machipukizi na mashada ya maua. Utitili wachanga hubeba tone la majimaji mkiani
na kudondoshea juu ya majani, ambapo likikauka
huacha doa la kahawia au nyeusi, lakini hasa rangi ya kutu. Maeneo
yaliyoshambuliwa na utitili hubadilika rangi na kuwa na weupe weupe wenye
mng’aro wa rangi ya fedha (silvery).
Baadaye hubadilika na kuwa na rangi ya udongo (kahawia), hatimaye hukauka
na majani hupukutika Eneo
linaloshambuliwa hudumaa na uzalishaji
kuathirika. Maeneo mengi ambayo hushambuliwa na utitili huwa korosho
hazizai kabisa. Miti iliyopukutisha majani kwa sababu yamashambulizi ya utitiri, huweza kuchipuza tena kwenye
mwezi Novemba na Desemba.
MAZAO MENGINE YANAYOSHAMBULIWA NA UTITIRI
Wadudu hawa hushambulia majani na hata maua ya aina mbalimbali ya mazao na mimea, kama vile mazao ya bustani (vitunguu nk), michungwa,
pamba, aina ya nafaka. Kwa sababu ya wingi wa aina ya mimea inayoshambuliwa na utitiri, udhibiti
wa wadudu hao unaweza kuwa mgumu kwa kiasi fulani.
KUSHAMIRI KWA UTITIRI
Wadudu hawa hupendelea mikorosho iliyosongamana, isiyopitisha hewa vizuri, mikorosho isiyopogolewa na mashamba yasiyohudumiwa kwa
ujumla. Hupendelea hasa miti mikubwa.
Utitiri hupendelea hali ya ukame au kiangazi cha muda mrefu.
KUSAMBAA
Utitiri husambazwa hasa kwa njia ya upepo au kwa kupanda vipando (propagation
materials) ambavyo vimeshambuliwa.
KUDHIBITI KWENYE MIKOROSHO
Njia pekee inayotumika kudhibiti utitiri ni matumizi ya
madawa. Dawa ya BASUDIN au KARATE ndiyo iliyopendekezwa
na watafiti kudhibiti utitiri wa korosho. Mchanganyiko wa mililita 5 za KARATE
na lita moja ya maji unatosha kudhibiti wadudu hawa katika mti mkubwa usiozidi
kipenyo (diameter) cha mita 10. Ni jambo la muhimu kukagua mashambulizi kuanzia
mwezi Mei. Upuliziaji unaanza mara tu baada ya kuona dalili za mashambulizi
au kuwaona wadudu wenyewe na kurudia baada yawiki tatu (siku 21). Upuliziaji
unafanyika kutumia mashine ya moto (Mist blower) au yakawaida (Knapsack
sprayer) kutegemeana na ukubwa wa mti. Ni muhimu kuanza kupuliza
dawa mapema, ili kuweza kuwathibiti wadudu hawa wakiwa katika hatua zao za
mwanzo kabisa za ukuaji wao ( hatua za lava na ninfu). Hii ni muhimu kwa sababu ni vigumu kuudhibiti
utitiri wakubwa. Awamu 2 hadi 3
zinatosha kuthibiti wadudu hawa katika msimu mmoja. Ikibidi, matunda (mabibo) yaliyopuliziwa dawa
yasitumike mpaka baada ya siku 21
UBWIRI UNGA - UGONJWA MKUU WA MIKOROSHO
Moja ya matatizo makubwa ya uzalishaji wa zao la
korosho ni ugonjwa wa Ubwiri unga.Ugonjwa huu unasababishwa na vimelea aina ya uyoga (fungus) viitwavyo
Oidium anacardii. Ugonjwa huu ni muhimu sana, kiasi kwamba kama
haukuthibitiwa, unaweza kupunguza mavuno
kwa zaidi ya asilimia 70. Ugonjwa huu
umeenea katika mikoa yote inayolima zao hili Tanzania. Hapo awali ugonjwa huu ulikuwa unaitwa kwa
jina la“ukungu” kutokana na uhusiano wake mkubwa na haliya hewa ya ukungu (litabwe
kwa Kimakonde) unaoonekana alfajiri/asubuhi katika miezi ya Juni - Septemba. Hivyo
basi, jina la Ubwiri unga
linatumika sasa ili kuwawezesha wakulima wasichanganye vitu hivyo viwili.
MASHAMBULIZI
Ugonjwa huu unashambulia maeneo yote machanga na teketeke katika
mti wa mkorosho, hasa machipukizi, majani, maua, mabibo na korosho
changa (tegu). Athari kubwa ya
ugonjwa huu inatokana na mashambulizi ya
maua, ambayo hushindwa kufunguka na kuwezesha chavua kufanya kazi yake, hatimaye
hunyauka na kukauka.
DALILI
Maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu, hufunikwa na unga
unga mweupe au wakijivujivu ambao huonekana
kama vumbi vumbi. Vimelea au chembe chembe zinazoshambulia ni ndogo ndogo sana na
hazionekani dhahiri kwa macho, ila kwa darubini. Chembe chembe hizi
zinapozaliana kwa wingi katika maeneo ya mshambulizi, ndipo huonekana kama unga
unga mweupe/kijivu.
KWENYE MAJANI
Pamoja na kufunikwa na unga unga, majani yaliyoshambuliwa husinyaa, hubadilika
rangi, wakati mwingine hukunjamana. Majani machanga zaidi yanaweza kupukutika,
ambapo yale yaliyokomaa hayashambuliwi. Masalia ya mashambulizi kwenye majani yaliyokomaa, huonekana kama
mabaka ya kahawia, hata hivyo hayapukutiki.
KWENYE MAUA
Maua yanaweza kushambuliwa hata kabla ya kuchanua. Pamoja na
kufunikwa na unga unga weupe/kijivu, maua yaliyoshambuliwa sana
hushindwa kuchanua na hatimaye hukauka kabisa na kuwa kama
“majani yachai”. Hili ndilo sababisho kubwa la upungufu wa zao la korosho.
KWENYE MABIBO
Mabibo yaliyoshambuliwa huonyesha unyafuzi,hupasuka pasuka na ngozi yake
huonekana kuwa chafu. Hatimaye,
mabibo hayo huwa madogo kwa umbo,
yenye maji kidogo sana, hivyo kuyafanya maji yake kuwa matamu
sana.
KWENYE TEGU NA KOROSHO
Tegu
zilizoshambuliwa huweza
kubadilika rangi yake ya kijani/nyekundu na kuwa ya hudhurungi au bluu iliyo
mzito. Tegu zikishambuliwa zingali changa sana, huweza kupukutika. Tegu
zilizoshambuliwa zikifikia kukomaa, zinaonyesha uharibifu mkubwa wa ngozi yake
na huonekana chafu, hatimaye, wakati wa mauzo hutengwa katika daraja
lachini (grade II).
KUSTAWI KWA UBWIRI UNGA
Vimelea vya Ubwiri unga vinaishi kwenye mimea iliyo hai tu,
haijawahi kuoteshwa katika maabara. Ugonjwa huu hushamiri na kustawi vizuri
katika majira yenye ukungu, hasa kuanzia mwezi Mei/Juni hadi Septemba karibu
kila mwaka. Mazingira mwafaka kwa ugonjwa huu ni:
• Joto: 26 - 28 0C (bora 25 C)
• Unyevu (RH): 80-100% (bora 95%)
Ubwiri unga pia hupendelea
zaidi mikorosho iliyosongamana na isiyopitisha hewa vizuri. Ugonjwa huu
hupendelea mazingira ya kiangazi, hasa
kuanzia mwezi Juni hadi Septemba, haupendelei hali ya mvua na joto jingi.
Hivyo basi, katika miezi mingine (hasa wakati wa masika), vimelea
hujificha na kuishi Kwenye maotea au
machipukizi uvunguni mwa mikorosho au kwenye
maua yasiyo ya msimu. Hivi ndivyo vyanzo
vya Ubwiri unga, vyenye uwezo wa kuhifadhi ugonjwa msimu hadi mwingine. Ugonjwa
huu husambazwa kwa upepo ambao nao pia hushamiri
sana katika miezi ya Mei/Juni hadi Septemba.
KUDHIBITI
Zipo njia aina tatu zinazotumika kuthibiti Ubwiri unga, nazo
ni mbinu za asili, mbegu bora na madawa.
MBINU ZA ASILI
(Cultural control)
Kuondoa vyanzo vya
Ubwiri unga (sanitation).
Hii ni kazi ya mikono ya kuondoa machipukizi na maotea yanayojificha
kwenye uvungu wa mikorosho, kutumia vifaa kama vile upanga,
mundu, shoka nk. Msingi wa kazi hii ni kupunguza kasi ya ugonjwa huu katika
shamba kwa kuchelewesha mlipuko na kasi
ya mashambulizi.
Kubadili mazingira ya
ugonjwa katika miti.
Kupunguzia
matawi (prunning) ya mikorosho
ili kufanya umbile la
mwamvuli katika miti, ili kuruhusu joto na upepo kupenya kirahisi,
inasaidia sana kuthibiti Ubwiri unga.
Kupunguza miti (thinning)
iliyosongamana na kuacha nafasi ya kutosha kati
ya miti, itasaidia kupunguza kuenea kwa ugonjwa. Miti ikiwa
katikanafasi ya kutosha,
itawezesha hewa kupenya vizuri na kubadili mazingira ili yasiwe
mazuri kwa kustawi kwa ugonjwa.
Kupanda mikorosho
inayovumilia/kuhimili ugonjwa.
Ipo baadhi ya mikorosho
ambayo inaweza kuhimili mashambulizi ya ugonjwa hata
kuweza kutoa Mazao bila ya kutumia kinga yoyote. Aina zingine zinaweza kutoa maua na kuzaa
kabla ya
athari za ugonjwa hata kuweza kukwepa mashambulizi. Hii
ni baadhi ya mikorosho
bora ambayo hatimaye imepandwa
katika eneo moja katika vituo vyetu
vyote vya kuendeleza korosho (Cashewnut Development Centre )kama NALIENDELE.
Mbegu zinazopatikana toka mashamba hayo ni mbegu bora (polyclonal seed) ambazo
zinaweza kuzaa bila madawa, lakini huzaa vizuri zaidi kama mtu atatumia dawa
pia.
MATUMIZI YA MADAWA
Dawa ya Salfa
(Sulphur)
Salfa ndiyo dawa inayotumika kwa wingi zaidi kukinga ugonjwa
wa Ubwiri unga. Dawa hii ambayo ni ya unga, inapulizwa kwa kutumia mashine
maalumu (motorised blower) ya kupulizia
dawa k.m. Maruyamana Solo. Kiwango cha
gramu 250 kwa mti, kwa mzunguko,
ndicho kinapendekezwa. Hivyo basi kwa
mizunguko mitano kiasi cha kilo 1.25
cha salfa kwa mti kwa mwaka kinahitajika. Pia kuna salfa za maji kama Thiovit ambazo unaweza
kupulizia kwa kutumia vinyunyuzia dawa vya kawaida (knapsack sprayer)
Wakati wa kuanza kupulizia
sailfa
Mpulizo wa kwanza unaanza ambapo karibu asilimia 20za maua
yamejitokeza na wakati sawa, zaidi ya asilimia 5 ya maua hayo tayari yawe yanaonyesha dalili za ugonjwa. Upimaji wa maua ili kujua lini
upuliziaji uanze, inasaidia
kufanya matumizi sahihi ya dawa,
hatimaye faida/pato litakuwa kubwa kwa mkulima.
Inashauriwa kwamba upuliziaji ufanyike asubuhi na mapema,
wakati ambapo kuna umande. Asubuhi, upepo nao
huwa hauna nguvu sana na
inashauriwa upuliziajiusizidi ya saa 3 asubuhi. Umande unasaidia salfa ya unga iweze
kunata kwenye majani na maua. Ila kwa salfa ya maji kama thiovit unaweza
kupulizia wakati wowote.vipindi vifuatavyo, vimependekezwa katika upuliziaji:Siku
14 14
14 21 21
Dawa zingine badala
ya salfa.
Madawa kadha wa kadha yamefanyiwa utafiti sambamba na salfa. Aina tatu za dawa
hizo (waterbased organics), zimependekezwa kwa matumizi ya wakulima,
nazo ni Bayfidan, Anvil na Topas. Kiwango
cha upuliziaji ni ml 10 - 15 za dawa ndani ya0.75 -
1.25 za maji kutegemeana na ukubwa wa mti. Vipindi
kati ya mipulizo ni wiki tatu (siku
21) na awamu (raundi) 3 zinatosha
kwa msimu. Inashauriwa kwamba kutokana na gharama za dawa yamaji, zinafaa
zitumike kwenye mikorosho ambayomkulima ana uhakika wa kutoa zaidi ya kilo 4
baada ya kupulizia. Miti inayotoa chini
ya kiasi hicho heri isipuliziwe, vinginevyo italeta hasara
KIFA UWONGO - MDUDU HATARI KWA MIKOROSHO
Kifa-uwongo (Mecocorynus loripes),. ni mdudu aina ya
“weevil” ambaye hushambulia mashina ya mikorosho hata kufikia hatua ya kuuwa mti
mzima. Mdudu huyu huitwa “kifa-uwongo” kwa sababu ya mbinu yake makini
anayotumia kujihami. Mara tu aonapo mtu anapita karibu yake, huanguka chini na
kujifanya kama amekufa kabisa. Kisha baada ya mtu yule kupita, yeye huamka tena
na kuendelea na shughuli zake kama kawaida. Wamakonde humwita mdudu huyu
“Nang’ang’ana”, ambapo Wayao nao humwita “Ng’ang’ani.
MAISHA YA KIFA UWONGO
“Kifa-uwongo” kama wadudu wengine, hupitia hatua za yai,
“lava” na “buu” kabla ya kuwa mdudu kamili. “Kifa uwongo” kamili aliyekomaa,
ana rangi ya kahawia na urefu wa kama sentimita 2. Ana mdomo mrefu uliochongoka
(snout) ambao daima anauficha kwa kuulaza kifuani pake. “Lava” wake ni aina ya
funza (grab) mweupe, mwenye ngozi ya kukunjamana na kichwa cha rangi ya kahawia
mzito (dark brown), yeye daima huonekana
amejikunja kama upinde.
“Kifa uwongo” wa kike hutoboa gamba la mkorosho kwa kutumia
mdomo wake mkali, na kutaga yai moja moja. Baada ya mayai kuanguliwa, mafunza
huanza kushambulia gamba la mti mara moja. Funza hawa wana midomo mikali kama
misumeno, nao wanakula kwa bidii sana gamba la mti. Kadri wanavyokula ndivyo
wanavyoongezeka ukubwa pia. Funza akaribiapo kuwa Buu (pupa), hupekecha ndani
ya mti (kiasi cha sentimita 2.5 chini ya gamba) na kutengeneza matundu kwa
ajili ya maficho ya buu (pupal chambers). Mabuu hujifungia ndani ya matundu
hayo na hatimaye hugeuka na kuwa “Kifa uwongo” kamili. Mzunguko wa kutokea yai
hadi “Kifa-uwongo” kamili, huchukuwa muda wa miezi sita, ambapo muda wa karibu
miezi 2 - 2.5 huwa katika hatua ya mafunza, ambayo ndiyo yenye uharibifu
mkubwa. “Kifa-uwongo” kamili ana mabawa na anaweza kuruka kwa nadra toka mti
hadi mwingine. Mara nyingi wadudu hawa, huonekana wakidumu katika maeneo ya mashambulizi. Mashambulizi yanaweza kuchukua muda wa mwaka
au miwili katika mti mmoja, ambapo mti wa jirani unaweza kuwa huru kabisa bila
mashambulizi!. Mara nyingi “Kifa-uwongo”
hupenda kuhamia mkorosho mwingine baada ya kuua kabisa mkorosho waliouanza
kushambulia.
DALILI ZA MASHAMBULIZI
Maeneo ya mashambulizi huonekana wazi wazi hata toka mbali,
kwa sababu ya uwepo wa Mchanganyiko wa utomvu na takataka kama za maranda ya
seremala ambayo hatimaye hugeuka rangi na kuwa nyeusi. Rangi ya majani ya mkorosho ulioshambuliwa
sana, hubadilika na kuwa njano, kisha hunyauka na hatimaye hukauka. “Kifa-uwongo”
hupendelea kushambulia miti mikubwa tu. Utafiti umeonyesha pia kwamba
hupendelea miti iliyojeruhiwa kutokana na kukatwa kwa ajili ya ubebeshaji (top-work) au hata ile ya kupunguzwa matawi.
Inasadikika kwamba aidha eneo la jeraha ni rahisi kwa kifa uwongo kutaga mayai
yake, au huenda kuna mvuto wa aina yake kutokana na harufu ya utomvu utokao eneo
lenye jeraha na kufanya mvuto wa pekee kwa kifa uwongo kushambulia!
MKOROSHO ULIOSHAMBULIWA NA KIFA-UWONGO
JINSI YA KUDHIBITI KIFA UWONGO
Hakuna dawa ambayo inashauriwa kutumika katika kuthibiti
wadudu hawa, badala yake, mkulima
mwenyewe anashauriwa kupambana nao ana kwa ana: Mwanzoni mwa mashambulizi. Ukaguzi
wa mara kwa mara ufanyike kwa kila mkorosho kukagua mashambulizi hayo. Mara tu
baada ya kuona dalili za mashambulizi ya wadudu hawa, bandua eneo la
mashambulizi kwa kutumia kisu au upanga
na kuwaondoa mafunza wote. Funza akidondoka chini hana uwezo tena wa kupanda kwenye mti au kufanya mashambulizi.
Mabuu waliojifungia kwenye matundu ya maficho yao, wanaweza kuuawa kwa kutumia ncha
kali, kama vile spoku yabaiskeli, ili kuwatoboa wakiwa ndani
yamashimo yao. Inashauriwa pia
kuwasaka na kuwaua kila “Kifa uwongo” kamili (adults) kwa kuwakata vichwa
vyao.
MASHAMBULIZI YALIYOKITHIRI
Inashauriwa
kukata na kuchoma moto mikorosho yote iliyoshambuliwa kwa kiwango cha
hali ya juu, ili kuuwa mabaki ya mayai na funza waliopo
MILIBAGI - MDUDU MHARIBIFU WA MIKOROSHO
UTANGULIZI
Milibagi (Pseudococcus longispinus) ni wadudu waharibifu
katika zao la korosho, waliojitokeza kuwa maarufu sana katika miaka ya tisini.
Hawa ni wadudu wanaoonekana katika maeneo mengi ulimwenguni, lakini hushamiri
na kuleta athari kubwa katika mazingira ya Tropikali. Mnamo mwaka 1990,
milibagi walionekana kushambulia mikorosho katika maeneo ya mjini Masasi. Mwaka
1993, walionekana kuenea hadi wilaya za Nachingwea na Tunduru. Hivi leo, wadudu
hawa wameenea karibu sehemu nyingi za kanda ya kusini, ingawa mashambulizi
makubwa yapo wilayani Masasi, Tunduru, Nachingwea na Liwale. Milibagi ni moja ya wadudu waharibifu wanaoishi
na kuponea mimea. Wadudu hawa hutengeneza utando mweupe (scale) juu ya miili
yao kwa ajili ya kinga na kujihami dhidi ya adui zao.
Milibagi huonekana katika mazao ya aina nyingi ikiwa ni
pamoja na miembemafuta, mihogo, michungwa, minanasi nk. Pamoja na hivyo, kuna
tofauti kati ya milibagi wanaoshambulia hayo mazao mbalimbali. Kwa mfano,
milibagi wa mihogo (Phenacoccus manihoti), miembe (Rastrococcus invadens) ni tofauti
na wale wa mikoroshoni (P. longispinus). Dalili za Mashambulizi ya Milibagi. Maeneo
yaliyoshambuliwa na milibagi huonekana yamefunikwa na weupe weupe ambao ni
utando unaofunika miili ya wadudu hao. Mikorosho iliyoshambuliwa sana na
milibagi, huonekana kwa mbali kama vile imefukikwa na theluji. Mashambulizi ya
Milibagi Milibagi wanaweza kushambulia eneo lolote la mmea kwa njia ya
kufyonza. Kwa jinsi hiyo, milibagi huingiza matemate yao katika maeneo ya mashambulizi na hatimaye
huweza kueneza vimelea vya virusi. Milibagi hutoa utomvu mweupe mweupe kama asali
na kufunika maeneo ya mashambulizi, hata kufanya mmea usiweze kupata mwanga wa
jua vizuri hata kuzuia utengenezaji wa chakula cha mimea (photosynthesis). Majani yaliyoshambuliwa sana na milibagi, hupukutika
hivyo kuathiri uzalishaji. Maua yaliyoshambuliwa mapema na milibagi yanashindwa
kuzaa. Korosho zilizoshambuliwa zingali zinakomaa, zinachafuliwa kwa utando na
utomvu.
Korosho hizo yamkini zisafishwe kwa mchanga kabla ya kufikiria kuuzwa, vinginevyo
hutengwa katika daraja la pili. Mashambulizi ya milibagi, yanaweza kupunguza
uzalishaji kwa kiwango cha asilimia 50% Kustawi kwa Milibagi. Milibagi
huonekana kwa wingi wakati wa kiangazi, hasa mwezi Septemba hadi Novemba.
Milibagi hupungua sana wakati wa mvua. Inaelekea kwamba mabadiliko ya hali ya hewa
ni chanzo kikubwa cha mashambulizi ya milibagi kwenye mimea. Maisha ya
Milibagi. Milibagi wa kike hutaga kiasi cha mayai 50-500 kutegemeana na
mazingira. Mayai huanguliwa na kutokea Vitambaazi (crawler). Hatua hii ni muhimu
kwa usambaaji wa milibagi. Hawa hutambaa mpaka kwenye ncha au vilele vya miti
na kujitegeshea miguu yao ili wasambazwe kwa upepo, ndege au wadudu wengine.
Binadamu pia wanahusika sana kusambaza wadudu hawa katika hatua hii. Hatua za
lava zinazofuata ndizo za ulaji na uharibifu. Milibagi waliokomaa (adults) huwa
hawajishughulishi (inactive), huwa hawali chakula na huishi muda mfupi (wiki au
mwezi)
KUDHIBITI
Zipo njia mbili
ambazo zinaweza kutumika kudhibiti milibagi:
◊ NJIA YA KIBAIOLOJIA
Utafiti umeonesha kwamba
wapo wadudu wengine ambao
wanaweza kushambulia milibagi, kama vile:
a) Ladibedi bito (Chilocorus spp)
b) Manyigu (Chrysopa spp)
Utafiti umeonesha kwamba idadi ya wadudu hawa mashambani ni
ndogo kwa kuweza kudhibiti idadi kubwa ya milibagi. Utafiti wa kina zaidi
unafanyika kuona jinsi ya kuwafanya wadudu
hawa waongezeke idadi ili kuweza kuwadhibiti milibagi mikoroshoni.
◊ NJIA YA KUTUMIA MADAWA
Njia pekee inayotumika hivi sasa kuwadhibiti milibagi ni
kutumia madawa. Dawa aina ya Selecron 720 EC
ndiyoiliyothibitishwa na utafiti itumike dhidi ya milibagi.
Dawa ya Selecron 720 EC Dawa hii ni ya aina ya maji, inayosambazwa na kampuni ya Norvatis (Ciba Geigy).
Inapulizwa kwa kutumia mashine za
moto (motorized blowers) kama vile Maruyama 150DX au Solo
◊ Kiwango cha upuliziaji
ni mililita 7.1 ya dawa, ndani ya lita 1 ya maji kwa mti mkubwa.
◊ Upuliziaji unaanza mara tu
baada yakuona dalili
za mashambulizi yamilibagi.
◊ Marejeo ya
upuliziaji yafanyike kila baada ya siku 7 – 14 kutegemeana na hali ya
mashambulizi yalivyo.
Thursday, May 17, 2012
MBOLEA VUNDE
1. Namna ya kutayarisha
Mboji/Mbolea Vunde/Mbolea Hai
Mboji
ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama (matamahuruku)) ambayo
imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo. Sehemu za vitu
kama majani, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya
kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva
hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri.
Mboji
ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa
kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba.
Vipande
vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani
bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini
itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama
muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa.
Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea mboji.
Mboji
iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji
huchemka hata kiasi cha kuua magonjwa ya mimea na mbegu za magugu.
Majani
makavu ya ndizi ni mazuri kwa kutunza vifaa vya mbolea na kuweka ukavu. Hali
hii huwa huzuia kupotea kwa maji kabla ya kujenga lundo la mboji na wakati
mbolea inapokuwa inaiva.
1.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa
kwenye mboji
Sehemu za mimea ambazo
zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua wadudu (viuatilifu) na kwekwe juzijuzi
(Pesticide/herbicides). Vipande vya nyama kwa sababu vinavutia panya na
wadudu wengine. Sehemu nyingi za Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na
wanyama (matamahuruku)) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe
vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga
hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile
sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi,
tifutifu na hunukia vizuri. Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea , Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za
chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba.
Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au
shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji
lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea.
Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na
ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea
mboji. Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa
shambani. Mboji huchemka hata kiasi mimea na majani ambazo ziliambukizwa
ugonjwa. Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi
mikono na miguu. Magugu ambayo yanarudiarudia
kila mwaka. Magugu kama hayo huuliwa kwa kuanikwa kwenye jua kali ili yakauke
baadaye huchomwa ili yasienee na jivu lake
huongezwa kwenye biwi, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya
kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva
hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu na hunukia vizuri.
Mboji
ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za chini sana na inafaa mno kuongezwa
kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba.
Vipande
vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au shambani
bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji lakini
itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini kama
muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa.
Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea mboji.
Mboji
iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa shambani. Mboji
huchemka hata kiasi cha kuua magonjwa ya mimea na mbegu za magugu.
Majani
makavu ya ndizi ni mazuri kwa kutunza vifaa vya mbolea na kuweka ukavu. Hali
hii huwa huzuia kupotea kwa maji kabla ya kujenga lundo la mboji na wakati
mbolea inapokuwa inaiva.
1.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa
kwenye mboji
Sehemu za mimea ambazo
zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua wadudu (viuatilifu) na kwekwe juzijuzi
(Pesticide/herbicides). Vipande vya nyama kwa sababu vinavutia panya na
wadudu wengine. Sehemu nyingi za Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na
wanyama (matamahuruku)) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu ili kusazwa na viumbe
vidogo vidogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya mboga
hutengeneza mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku ni tofauti kabisa na zile
sehemu zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi,
tifutifu na hunukia vizuri. Maelezo ya msingi kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea , Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama zake ni za
chini sana na inafaa mno kuongezwa kwenye udongo ili kuinua mazao ya shamba.
Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe mara nyingi huwa vimejazwa nyumbani au
shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika kutengenezea mboji
lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba yake kupotea.
Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri na
ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika kutengenezea
mboji. Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa
shambani. Mboji huchemka hata kiasi mimea na majani ambazo ziliambukizwa
ugonjwa. Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi
mikono na miguu.huwa vimejaa nyumbani au shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza kutumika
kutengenezea mboji lakini itachukua muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba
yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili kushugulikia mbolea matokeo
yatakuwa mazuri na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni yanatumika katika
kutengenezea mboji.
Mboji iliyotunzwa vyema huwa na rutuba nzuri kwa mimea
inapotumiwa shambani. Mboji huchemka hata kiasi mimea na majani ambazo
ziliambukizwa ugonjwa.
Vifaa vilivyo na ncha kali kama mwiba ambavyo vyaweza
kujeruhi mikono na miguu.
Magugu ambayo yanarudiarudia kila mwaka. Magugu kama hayo
huuliwa kwa kuanikwa kwenye jua kali ili yakauke baadaye huchomwa ili yasienee
na jivu lake laweza kuongezwa kwenye lundo la mbolea.
Vitu visivyo kua na uhai kama plastiki na chuma.
1.2 Mfano wa vitu vinavyoweza kutumiwa kutengenezea mboji nyumbani
2. Namna ya kutengeneza
mboji ya mimea
Kusanya
vitu na vifaa vinavyohitajika katika utengenezaji wa mboji ambayo ni;
Majani mengi mabichi/kijani na
makavu. Majani jamii ya mikunde ni mazuri sana kwani hutengeneza kirutubishi
cha naitrojeni (N) kwa wingi.
Mabua ya mahindi au vitawi vya miti
Udongo wa kawaida wa juu
Samadi, mbolea yoyote ya wanyama au
mboji ya zamani
Majivu au vumbi la mkaa
Maji
2.1 Hatua
1) Chagua sehemu karibu na eneo ambalo
mboji itaenda kutumika na ambapo kuna hifadhi ya kutosha kukinga dhidi ya
upepo, jua na mvua.
2) Katakata majani yawe madogo madogo
ili yaweze kuoza haraka. Tengeneza msingi kama mita sita (6) urefu na upana
wake mita 2 kwa kutumia majani magumu kama matawi/vijiti. Hii itahakikisha
maji yanatiririka na hewa ina zunguka vizuri. Hakikisha kuna nafasi ya
kutosha kufanyia kazi kwenye biwi bila kulikanyaga.
3) Weka sentimita 10 ya majani ambayo
hayaozi haraka kwa mfano mabua vya mahindi au mimea mibichi/kijani.
4) Weka sentimita 10 ya vifaa ambavyo
huoza haraka kwa mfano maganda ya mboga na matunda.
5) Weka sentimita 2 ya samadi
(mbolea-hai ya wanyama), mabaki ya mbolea ya zamani kama yaweza kupatikana.
6) Weka udongo wa juu sentimita 10
kutoka kwenye shamba ambalo hulimwa.
7)
Majivu na mkojo vyaweza kunyunyuziwa juu ili kufanya biwi/lundo kuoza haraka.
Kukatakata majani
8) Nyunyizia maji kwenye biwi mpaka lilowe.
9)
Rudia mpangilio huu kuanzia namba nne (4) mpaka lundo lifike mita moja (1.m)
hadi moja na nusu (1.5m) kwenda juu isipokuwa vijiti/matawi ya kwanza.
2.2
Zingatia
Biwi/lundo
cha mboji kinatakiwa kifunukwe ili kupunguza/kuzuia mvuke ama mvua nyingi
ambayo hubeba rotuba kutoka kwenye mbolea. Weka gunia, nyasi ama matawi ya
ndizi yaliyokauka.
Kila tabaka/kunjo/safu
yafaa kupangwa kuanzia kwenye ukingo ili lundo la mbolea lisiporomoke.
Namna nyigine ya kuzuia lundo kuporomoka ni kwa kuweka vipande vya mbao kando
ya biwi. Wavu wa nyuzi za chuma utafanya biwi kukauka.
|
3. Wadudu wenye manufaa na
mazingira yanayohitajika kwenye Biwi
3.1 Wadudu ambao husaidia
kufanya biwi kuoza
Viumbe
wengi wanaohusika na kazi hii ya kuoza ni wadogo hawaonekani kwa macho matupu.
Ila viumbe hawa huhitaji maji, hewa na vipande/sehemu ya viumbe wengine ambazo
kwao ni chakula. Viumbe hawa hula vipande hivyo na hutoa hewa ya carbon dioxide,
maji na joto.
Kuna
hatua tatu kubwa wakati biwi linapooza; hatua ya kupanda joto, hatua ya
kupoa/kuwa baridi na hatua ya kukomaa.
Wakati
ya hatua ya kupanda joto, joto hufikia kiwango cha juu sana katikati mwa
biwi. Uzuri wa joto hili ni kwamba magonjwa yaliyokuwa kwenye viungo vya biwi
na mbegu za magugu huchomwa hadi kufa. Hatua ya pili ya
kuwa baridi; uyoga (fungi) huwa na faida nyingi kwa sababu kazi yake ni
kuzisaga nyuzi ngumu ambazo zimo kwenye viungo vya mimea au majani.
Kwenye hatua ya tatu,
‘hatua ya kukomaa’ viumbe wakubwa kama mchwa na nyungunyungu husaidia
kusaga na kuchanganya mbolea.
Hali ya anga ikiwa na
joto jingi viumbe hawa hufanya kazi haraka kuliko wakati ambapo hali ya anga ni
baridi. Aina ya viungo vilivyotumika kujenga/kukuza biwi na ukali/uchungu (pH)
wa udongo pia huathiri kiwango cha mbolea kuoza.
3.2
Mazingira yanayohitajika kwenye biwi
Biwi huhitaji vitu
vitatu: hewa, maji na joto.
Hewa
Viumbe wadogo kwenye
biwi huhitaji hewa ili waweze kuishi. Hewa ya carbon dioxide (CO2)
ambayo imetolewa na wadudu hawa huhitaji kutolewa nje. Ikiwa hewa safi
itakosekana, viumbe wengine wasiohitajika huingia na kutoa harufu mbaya na pia
kufanya mbolea isioze haraka.
Maji
Kazi ya viumbe wadogo
huwa polepole ikiwa biwi ni kavu. Aidha ikiwa biwi litalowa maji basi viumbe
wadogo watakufa na kufanya biwi kuwa na uchachu badala ya kutengeneza mbolea.
Hivyo basi kukagua kiwango halisi cha maji huhitaji ujuzi fulani.
Joto
Biwi hutoa joto wakati linaoza. Lundo
likiwa na joto jingi viumbe wadogo hutoka, kisha huweza kurudi pindi linapopoa.
4. Matunzo ya Biwi
Ili
kupata mbolea nzuri, biwi linapojengwa yafaa lishughulikiwe kwa utaratibu. Biwi
hilo litahitaji maji, kupinduliwa, joto na muda unaofaa wa kukomaa.
4.1 Maji
Wakati wa kiangazi biwi/lundo la mboji huhitaji
kumwagiliwa maji kila wiki. Maji katika lundo la mbolea hupimwa kwa kuweka
fungu dogo la nyasi na kulitoa baada ya dakika tano. Nyasi isipoonyesha
majimaji au unyevu itabidi maji yamwagwe kwenye lundo hilo.
Kuna njia kadha za
kuzuia mvuke kuinuka kutoka kwenye biwi, hali kadhalika kiwango cha maji
yanayomwagiliwa:
Funika lundo kwa majani ya ndizi ama nyasi.
Funika lundo kwa udongo.
Lundo
lisigeuzwegeuzwe
Biwi likilowa maji itabidi kifunuliwe na
kuachwa kikauke kwenye jua kabla ya kujengwa tena.
4.2 Kupindua/kugeuza
Katika
muda wa wiki tatu (3) baada ya kujenga/kukuza biwi/lundo ukubwa wake utakuwa
umepungua sana. Kupindua biwi uhakikishe ya kwamba majani yaliyo kando yameoza
pia hewa safi imerejeshwa. Kupindua biwi huchanganya majani yaliyotengenezwa na
kukijenga upya. Majani yalivyo kando huwekwa katikati, ikiwa kuna ukavu, maji
mengi na majani/viungo vikavu huongezwa. Kupindua kunatikiwa kufanyike kila
baada ya wiki tatu.
Hali ya joto na kiwango cha maji yafaa kupimwa siku
chache baada ya kupinduliwa. Kupinduliwa kwa mara ya tatu kutahitajika ikiwa
viungo havitakuwa vimeoza kikamilifu.
Mbolea
yaweza kutengenezwa bila kupinduliwa ila viungo vilivyo kando havitaoza. Mbegu
za magugu na viungo na magonjwa ya mimea hayatakufa. Viungo vilivyobaki
hutengwa na kutumiwa kwenye biwi lingine. Japokuwa kugeuza hakuna lazima,
kunapendekezwa ili kupata mbolea nzuri.
4.3 Kiwango cha Joto
Kupima kiwango cha joto kwenye biwi kunahitaji kijiti kirefu kichomwe ndani ya lundo siku kumi (10) baada ya kujengwa. Kijiti yafaa kionyeshe joto la kutosha kinapoguswa kwa mkono, la sivyo kuoza bado hakujaanza kufanyika. Katika hali kama hii, maji ama hewa itahitajika kwenye biwi na biwi kuachwa kwa muda. Ikiwa biwi lina joto jingi, biwi linaoza basi viumbe hai wanaweza kufa. Katika hali hii, hewa na maji itabidi kuongezwa ili kufanya biwi lipoe. Kiasi cha joto yafaa kupimwa mara kwa mara kwa kutumia kijiti.
Chini
ya 57C
Joto hili linaweza
kuivisha mboji lakini haliwezi kuua mbegu za magugu na magonjwa.
57-71C
Joto muafaka kwaajili ya kuivisha mbojj
na kuua mbegu za magugu na magonjwa. Katika kiwango hiki cha joto, mbegu zote
na vijimelea vyote vya magonjwa vilivyoko kwenye mchanganyiko wa mboji hufa na
hivyo kutokuwepo pale mboji inapokuwa imeiva.
Zaidi
ya 71C
Joto hili ni kali
sana na huweza kusababisha madhara mengineyo kama vile kuzalishwa kwa gesi
zenye madhara pia wadudu wenye manufaa ambao husaidia mboji kuiva huweza
kukimbia.
Muhimu kuhakikishakuwa joto halizidi sana ili kuweza kuwa na mboji bora yenye virutubisho
Subscribe to:
Posts (Atom)