KURASA

Tuesday, October 7, 2008

UANDAAJI WA VIPANDIKIZI KABLA YA KUPANDA


Kabla ya kupanda mche wa mtiki inabidi uandaliwe kukabiliana na mazingira magumu hasa ukame, ili miche iweze kumea vizuri baada ya kupandwa inabdi ikatwe juu na kwenye mizizi na kubakia kama vipandikizi.


Mche unakatwa juu na chini na kubakia juu robo na robotatu kwenye mzizi, hii inasaidia kuanza kukua mara moja na hata kama mvua zitakuwa hafifu bado miche hii itahimili ukame kwa muda mrefu zaidi.


Vipandikizi pia vina sifa ya kuwa na uwezo wa kunyooka bila kupinda pinda wakati wa ukuaji, tofauti na miche ya kwenye vipakti.
Sehemu ya juu ya kipandikizi inaachwa na macho mawili tu kwa ajili ya kutoa matawi ambapo yatakapoanza kuchipua moja litakatwa na kubakia na moja ambalo litakuja kuwa mche na mti bora hapo baadae


Ukiangalia picha hapo juu, kulia kwako ni miche kabla haijakatwa kubakia vipandikizi na kushoto kwako ni fungu la vipandikizi kabla ya kukatwa. Na huyo jamaa hapo anaonekana akipanda kwenye shimo la wastani moja ya vipandikizi vyake

9 comments:

  1. asante sana kwa mada ambayo nimeipenda.

    Naona hapo una seedlings nyingi ulizoandaa kwa njia ya bare root, pia nimeona survival rate ni kubwa hadi 70%
    Je, unauzoefu wowote wa kutumia containerized seedlings kama vile polyethlene tubes, na je survival rate inakuwa kiasi gani?

    Pia kutokana na uzoefu wako kwa large plantation kwa mitiki bila kuchanganya na mazao mengine spacing nzuri ipi?

    Just keeping you busy

    ReplyDelete
  2. Kwa kutumia polyethlene tubes survival rate inashuka kidoko chini ya 70% ambapo inaweza kufika hadi 65%
    Na kwa kawaida spacing inakuwa 2.5m mpaka 3.0m lakini mimi napendelea 3m kwa sababu inaipa nafasi zaidi miti kwa hiyo na mazao utapata mapema zaidi

    ReplyDelete
  3. Miche ya mitiki hutumia muda gani kukua mpaka kufikia hatua ya kuvunwa?na huwa na ukubwa gani wakati huo?unaweza kupata estimate ya mti huo kuuzwa kiasi gani wakati wa kuvuna?

    ReplyDelete
  4. @Michael Kamugisha Mitiki huwa tayari kuvunwa baada ya miaka 12 - 15 kwa wastani lakini ukisubiri zaidi utapata bei nzuri zaidi na miti mikubwa zaidi (miti miwili yenye ukubwa sawa ila umri tofauti ina bei tofauti, wenye umri mkubwa huuzwa bei zaidi) kuhusu bei isikuumize kicha maana mti wa miaka 12 baadae huwezi kujua bei leo ila cha maana ni kuwa Mbao ya mtiki ndio aghali zaidi duniani

    ReplyDelete
  5. Nimefurahi sana kuona blog hii, mtiki kwa sasa ni bei gani ???

    ReplyDelete
  6. Nafurahi sana kwa kutupatia elimu bora ihusuyo Kilimo cha miti ya mitiki.Mimi napenda kujua shimo la kupanda mche Wa mtiki linatakiwa liwe na ukubwa gani, namaanusha urefu, upana na kina chake, je na pia Shamba linalotakiwa kupandwa mitiki ni lazima lilimwe kwanza au laweza kufyekwa tu halafu yakaandaliwa mashimo kwa ajili kwa kupanda hiyo niche ya mitiki?

    ReplyDelete