KURASA

Saturday, December 6, 2008

WATER FILTER AND PUMP

WATER PUMP



Hiki ni chombo muhimu sana katika ufugaji wa samaki, kazi yake kubwa ni kuingiza hewa ndani ya chombo cha samaki. Kwa kawaida aquarium huwa inafunikwa sehemu kubwa ya juu na hivyo kupunguza kiwango cha hewa inayoingia. Water pump inaongezea hewa katika style tofauti, hewa inaingia kupitia mawe ya hewa(air stones) na pia kwa kupitia urembo mbali mbali ambao unakuwa ukicheza, kuzunguka au kufunuka na kuruhusu hewa kuingia

mirija ya pump


Kwa kawaida water pump inakuwa nje na inaingiza hewa kwa kutmia mirija inayoingia ndani ya maji mpaka kwenye sakafu ya chombo, ambako huunganishwa na vitu husika kama mawe ya hewa na urembo mbalimbali, pump pia husaidia kuleta mzunguko wa maji na kujenga hali ya mazingira ya uhalisia kwa samaki kama wako mtoni au bwawani/ziwani.

WATER FILTER
Hii hfanya kazi zote kama pump ila tofauti ni kwamba yenyewe ina kazi ya ziada ya kusafisha na kuchuja uchafu kwenye maji

Kwa filter ndogo huwa zinazama ndani ya maji (submeged) kwa sababu huwa zinapoozwa joto na maji hayo hayo,Sehemu ya chini ya filter huvuta maji na hewa huvutwa kutokea juu kwa kutumia mrija mdogo unaokuwa nje ya maji na sehemu ya kati huwa inatoa mchanganyiko wa maji na hewa.

Filter kubwa hukaa nje na mipira ya kutoa maji na kuingiza maji na hewa ndio huingia kwenye maji, hizi mara nyingi huwa zinatumiaka kwa ajili ya aquarium kubwa na mabwawa au vyombo vingi kwa mara moja kwa sababu vinaweza kusafisha vyombo zaidi ya kimoja kwa wakati

Ndani ya filter kuna chujio ambalo husafishwa kwa urahisi mara linapochafuka kwa wastani wa mara moja kwa wiki na likichoka huwa lina badilishwa

4 comments:

  1. ,,,Nataka kujuwa hizo bei za water filter na pump

    ReplyDelete
  2. kwa tank lisilozidi lita 200 (25 gallons) water filter ni shilingi 46,000 na water pump ni shilingi 18,000. Bei inaweza kupanda au kushuka kutokana na aina ya kitu unachotaka

    ReplyDelete
  3. https://netnaija.texhtok.co/blog/netnaija-latest-movies-download-site-full-hd-online

    ReplyDelete