KURASA

Monday, May 18, 2009

UPANDISHAJI/UZALISHAJI SAMAKI

Kama wewe ni mfugaji wa samaki kwenye mabwawa kwa ajili ya biashara, basi ni vizuri ukazalisha samaki wako, ndipo uwaweke kwenye bwawa wakiwa katika idadi inayojulikana nah ii itakusaidia kwenye ulishaji sahii na mavujo ya juu kulingana na ukubwa wa bwawa lako.

UTAMBUZI WA JINSIA
Hii ni kazi inayohitaji utaalamu na mazoea kidogo. Kwa kawaida samaki jike huwa na tumbo la mviringo kidogo wakati tumbo la samai dume huwa bapa, samaki dume huwa na vidoti vyeupe kwenye mapezi afikiapo umri wa kupanda, na huruka ruka zaidi ya jike mara watolewapo kwenye maji.



UPANDISHAJI
Kwa kawaida upandishaji hufanyika kwenye sehemu isiyo na kina kirefu kwenye vyombo maalumu, chombo kisiwe kwenye jua, na kiwekewe majani ya kutosha na mchanga chini. Kabla ya kuwapandisha samaki wawe kwenye vyombo tofauti kwa siku 3 – 4 na muda wote walishwe vyakula maalum nyenye protein nyingi, katika mazingira ya kawaida huwa tunawalisha nyungunyungu (earth worms) ambao hupatikana kwa kuchimba sehemu chepechepe, kama una samaki wazazi itakubidi uzalishe nyungunyungu (somo kuja baadae) walishe samaki wako kadri wanavyoweza kula
Baada ya kuridhika na maandalizi ya samaki wako, sasa unalichukua jike na kulipeleka kwa dume na si kinyume, dume huwalimechimba vishimo kwenye mchanga ambavyo baada ya muda jike likihamasishwa hutaga ndani yake na dume hurutubisha mayai, baada ya kurutubishwa jike huyachukua mayai na kuyaweka mdomoni kwake, baada ya hapo lazima jike arudishwe kwenye chombo chake kwa siku 6 – 10 na hapo watoto hutotolewa toke mdomoni mwake. Watoto wakitotolewa tu jike ataondolewa na kurudishwa kwenye bwawa la kawaida kwa sababu atawala watoto wake.

SAMAKI JIKE MWENYE MAYAI MDOMONI




Baada ya watoto kutotolewa utawalisha baada ya siku mbili na chakula chao kikuu ni viini vya yai na baada ya wiki wanaweza kula watoto wa dagaa uduvi ambao nao utawazalisha (somo kuja baadae)Samaki wako wakifikia ukubwa wa kutosha utawaingiza kwenye bwawa lako na kuendelea kuwalisha mpaka kufikia umri wa kuvuna.
Kama una mabwawa tayari na samaki wako wanapandana , ukienda ule upande wenye kina kifupi utakuta samaki dume amechimba vishimo vya kutagia, mara baada ya watoto kutolewa mdomoni na mama yao, unatakiwa kuwawahi na kuwahamishia kwenye sehemu salama ili wasiliwe na samaki wakubwa.

SAMAKI AKITOA WATOTO MDOMONI


Upandishaji wa samaki wa urembo ni kama huu sema wenyewe tofauti inakuja kwamba samaki kama gold fish hutaga popote pale hawachimbi vishimo na baada ya kutaga dume hurutubisha mayai, ili kujua mayai yamerutubishwa maji hubadilika rangi na kuwa kama ukungu, basi hapo utawatoa jike na dume na kuyaacha mayai, mayai yao huwa hayaatamiwi kwenye mdomo wa samaki jike.

SAMAKI BAADA YA KUVUNWA

4 comments:

  1. nimewatamani kweli hao samaki. kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  2. Hehehe najua wamekukumbusha mbali sana, tuombe uzima ukifika kule Likuyu Fusi najua wapo na utafaidi sana.

    ReplyDelete
  3. Ha ha hahaaa Asante kwa kunipa moyo si afadhali niende Nyasa nikale mpaka kusaza

    ReplyDelete
  4. nashukuru sana kwa darasa unalotoa hapa na kuspecialize kwenye hii sekta.

    tutafika tu kamanda

    ReplyDelete