KURASA

Wednesday, May 27, 2009

VUNJA - JUNGU




Huu ni msimu ambao huku kwetu wanakuwa wengi sana, hiki ni kipindi ambacho mvua zinaishia na kuelekea kwenye majira ya baridi (joto kupungua) hawa wadudu huzaana sana kipindi hiki na hujazana kwenye taa za majumbani na wakati mwingine huingia ndani

DUME



Kuna baadhi ya jamii huwakamata na kuwala kama vile kumbi kumbi na senene, lakini si wengi waliozoea kuona wakiliwa, ukimshika vibaya na anakapata nafasi anaweza kuku ng'ata ingawa hana sumu yoyote na kidonda chake ni kidogo kinachoweza kupona chenyewe.

JIKE



Kama una bustani ya maua na mboga mboga na unasumbuliwa na wadudu kuvamia mara kwa mara, basi unaweza kuwapandikiza wadudu hawa na wakakusaidia katika kuondoa wadudu waharibifu kwa njia ya kibaiolojia, kwa sababu wana tabia ya kula wadudu wengine kama chakula chao. ili kuweza kujua madume na majike angalia rangi zao, madume huwa na rangi zilizokooza na kijivu wakati majike huwa na rangi ya kijani kibichi


WAKIPANDANA

7 comments:

  1. Kamala! kazi kwelikweli. Haya bwana. Mi nilipokuwa mdogo tulikuwa tukiwaita hao wadudu SHETANI. Na nimekuwa nikijiuliza kwa nini? kweli shetani yupo hivi kama yupo? sijapata jibu. Msaada basi wadugu.

    ReplyDelete
  2. Dada Yasinta naona mlikosea kumuita huyu mdudu shetani maana muda wote amefumba mikono akisali au anatuzuga tu heheheh!

    ReplyDelete
  3. niliwakuta thailand wamekaangwa wanauzwa mida ya jioni meza zinatolewa barabarani wanauzwa kama vile dagaa wa kukaangwa pia kulikuwa na mende, lakini tulipokuwa wadogo tulikuwa tunamuita vunja jungu eti ukimshika utavunja vyombo

    ReplyDelete
  4. Du, kuuzwa kama dagaa.
    Mie nilipokuwa mdogo nilikuwa nawaogopa hao vunja jungu, maana tulikuwa tunaambiwa wanalenga pua na kuingia humo, halafu kivumbi utakiona. Lakini utoto.....

    ReplyDelete
  5. Nimepita hapa nikitoka kwa Yasinta. Kazi nzuri. Anaewaita hao wadudu shetani, anawaonea.

    ReplyDelete
  6. Karibu sana Fathy Mtanga kwenye baraza hili tupige soga, pia nashukuru kwa kupita kwako

    ReplyDelete