KURASA

Friday, June 26, 2009

NAZI

MNAZI



Tumezoea kwamba siri ya umri mrefu ni maji, lakini si maji peke yake ila yaambatane na ulaji mzuri, leo nawaletea siri ya NAZI ambazo ni zao la mti wa mnazi (cocos nicifera) ambao uko katika jamii ya mipama (palms) inayojumuisha miti kama michikichi, mitende na mingineyo tuyoitumia kama mapambo

NAZI KABLA YA KUFULIWA MAGANDA


Mti wa mnazi au MTI WA UHAI kama ninavyouita ni mmea unaostawi na kupatikana kanda za pwani na sehemu zenye joto, mikoa kama Tanga, Dar, Pwani, Mtwara, Lindi, Mafia na Zanzibar hupatikana kwa wingi. Kila sehemu ya mti huu inatumika katika maisha ya kila siku ya mwanadamu, makuti kuezekea na kutengenezea mafagio, tunda lake ni chakula, maganda ya nazi kwa ajili ya kuzuia upotevu wa maji kwenye bustani/shambani (mulching) magogo hutoa mbao na hutumika kutengenezea mitumbwi, na sehemu yoyote ya mnazi huweza kutumika kwa ajili ya kupikia kuanzia makuti, mahanda, vifuuu n,k

NAZI BAADA YA KUFULIWA


Jamii za watu wanaotumia sana nazi huwa hazishambuliwi na magonjwa kama kisukari, presha ya kupanda na magonjwa mengine ya moyo na kiasi kikubwa cha lehemu (cholesterol) mwilini ukilinganisha na jamii zinazotumia vyakula vyenye kupikwa na mafuta yanayotokana na mimea mingine kama karanga, alizeti, ufuta, mahindi n.k. kwa mfano mikoa kama Tanga na Zanzibar ambako kwa wastani mtu hutumia kiasi cha nazi 120 kwa mwaka katika vifo 1000 vya watu wazima ni vifo 1 – 2 vinavyohusiana na magonjwa ya moyo wakati mikoa ambayo hawatumii nazi karibu robo ya vifo hutokana na magonjwa ya moyo.

MAHANDA YA NAZI



Kuna taarifa kwamba nazi huongeza kiasi cha lehemu mwilini je ni vipi? Ukweli ni kwamba nazi inayotumika moja kwa moja yaani inakunwa na kupikiwa hapo hapo haina madhara ya lehemu, ila nazi inayohifadhiwa ndio huwa na tatizo hili kwa sababu huchanganyika na hewa ya haidrojeni (hydrogenation) na kuwa sawa na yale mafuta mengine ya viwandani KWA HIYO nazi iliyohifadhiwa baada ya kukunwa au tui lililohifadhiwa huweza kusababisha kuongezeka lehemu mwilini

NAZI ILIYOVUNJWA


Moja kati ya vyakula vichache duniani ambavyo walaji hawana mzio (allergy) nacho ni nazi, pia inasifika kwa kupunguza kiasi cha sukari mwilini, maji ya dafu husafisha figo na kibofu

NAZI ILIYOKUNWA TAYARI KUTENGENEZEWA TUI


MAHANDA YA NAZI YAKIZUIA UPOTEVU WA MAJI KWENYE CHUNGU CHA MAUA

5 comments:

  1. Nazi ni kiungo kizuri nilipokuwa Ruhuwiko nilipanda mbili. Mmhhh nimekumbuka wali wa nazi au maharage ya nazi we acha tu.

    ReplyDelete
  2. Hii ni elimu nzuri sana hakika toka kuanzishwa kwa blog watu tunaendelea kupeana elimu zaidi upo usemi usemao kuwa mabaya huonekana zaidi ya mazuri ila mimi nipo tofauti katika blog yako elimu unayotoa ni kubwa sana hongera sana kamanda wangu

    ReplyDelete
  3. umesasahau vifuu hutumika kama urembo kwa kutengeneza hereni, bangili na vibanio vya nywele na mapambo ya nyumba pia, ila sisi huku tuliko miti ya minazi hakuna isipokuwa tunapata tui linalouzwa kwenye makopo coconut milk au nazi ya unga coconut powder sasa hiyo lehemu mwangu!!!

    ReplyDelete
  4. Yasinta ukuaji wa miazi kwa hapo Ruhuwiko sidhani kama itamea vizuri sana sababu ya baridi

    Francis kama unaelimika na elimu yangu nashukuru sana kwani hata sisi pia huwa unatuelimisha

    Mumyhery ni kweli ilisahau kwamba vifuu vya nazi ni urembo wa kwa watu na nyumba zao ndio maana niliuita mti wa uhai kwa sababu una matumizi mengi kama vile unga wa ngano aksante sana

    ReplyDelete
  5. Ahsante baba, elimu tele tumepata

    ReplyDelete