KURASA

Wednesday, October 14, 2009

TARATIBU NA MASHARTI YA MIKOPO YA KUNUNUA TREKTA JIPYA



1. Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatikana katika Ofisi za kilimo za Halmashauri za Wilaya na Makao makuu ya Mfuko wa Pembejeo, jijini Dar-es-salaam na katika tovuti ya wizara ya kilimo.

2. Fomu za maombi zilizojazwa na kuambatanishwa na vielelezo vinavyohitajika zitapitishwa/kuidhinishwa na Afisa Kilimo wa Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya husika na baadaye kutumwa mapema kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo.

3. Mikopo ya kununua matrekta inatolewa na Mfuko wa Pembejeo, baadhi ya benki na taasisi za fedha na SCCULT (T) Ltd. kwa niaba ya Mfuko, mwombaji sharti atimize yafuatayo:-

(A) Awe na dhamana yenye hati miliki isiyohamishika iliyoandikishwa kwa jina la mwombaji.
(B) Awe na shamba binafsi lisilopungua hekta 50 na awe tayari kutoa huduma ya kuwalimia wakulima wengine
(C)Awe tayari kutekeleza masharti yote ya Mfuko wa Pembejeo au taasisi ya fedha na SCCULT yanayohusu mkopo wa ununuzi wa trekta jipya.
(D)Awe tayari kulipa asilimia moja (1%) ya mkopo kama gharama za nyaraka za mkopo na kusajili trekta kwa pamoja kwa jina lake na Mfuko
(E) Riba inayotozwa ni asilimia nane (8%) na marejesho hufanyika kwa muda wa miaka mitatu kila baada ya miezi mitatu.

2 comments:

  1. Ni utaratibu mzuri ninapenda kuwa na matumaini kuwa hapo baadaye itakuwa hivyo nchi nzima itakuwa inarahishisha sana idara ya kilima na pia labda watu watakuwa na afya zaidi. Mana kulima kwa jembe ni kazi kweli.

    ReplyDelete
  2. Sasa bei ya trekta jipya ndio kiasi gani watu tuanze kujipanga!

    ReplyDelete