Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
KURASA
▼
Thursday, April 30, 2009
DESMODIUM
Huu ni mmea ambao hutambaa adhini kama vile maharage, unapatikana zaidi nyanda za juu na sehemu zisizo na joto, majani yake huwa yana kwaruza na yanaweza kuchana mikono. mbegu zake huzaliwa kwenye vikonyo kama mimea jamii ya kunde kwa wastani mbegu nne
MATUMIZI (FAIDA)
Huu ni mmoja ya mimea ambayo inafaida zaidi ya moja kwa mkulima kama ataamua kuutumia ipaswavyo;
Desmodium inaweza kupandwa katikati ya mistari ya mazao kama mahindi, mtama, alizeti n.k, ambapo mmea huu huweza kusaidia mazao kwa kuongeza kiasi cha nitrojeni kwenye udongo (nitrogen fixer)maua yake huwa yanafukuza baadhi ya wadudu shambani (insect repelent) na mwisho huua magugu mengine yasiweze kuota kwa sababu yenyewe hutambaa juu ya ardhi (runners)na hukua haraka.
Desmodium pia hutumika kama chakula cha mifugo kwa sababu ya protini kiasi cha 18% -22% kabla ya kukaushwa na hushuka hadi 15% yakikaushwa, kwa hiyo mfugaji anaweza kuchanganya na majani ya kawaida na kuwalisha wanyama wake kwa nia ya kuongeza ubora wa chakula.