KURASA

Thursday, April 30, 2009

DESMODIUM





Huu ni mmea ambao hutambaa adhini kama vile maharage, unapatikana zaidi nyanda za juu na sehemu zisizo na joto, majani yake huwa yana kwaruza na yanaweza kuchana mikono. mbegu zake huzaliwa kwenye vikonyo kama mimea jamii ya kunde kwa wastani mbegu nne



MATUMIZI (FAIDA)
Huu ni mmoja ya mimea ambayo inafaida zaidi ya moja kwa mkulima kama ataamua kuutumia ipaswavyo;




Desmodium inaweza kupandwa katikati ya mistari ya mazao kama mahindi, mtama, alizeti n.k, ambapo mmea huu huweza kusaidia mazao kwa kuongeza kiasi cha nitrojeni kwenye udongo (nitrogen fixer)maua yake huwa yanafukuza baadhi ya wadudu shambani (insect repelent) na mwisho huua magugu mengine yasiweze kuota kwa sababu yenyewe hutambaa juu ya ardhi (runners)na hukua haraka.




Desmodium pia hutumika kama chakula cha mifugo kwa sababu ya protini kiasi cha 18% -22% kabla ya kukaushwa na hushuka hadi 15% yakikaushwa, kwa hiyo mfugaji anaweza kuchanganya na majani ya kawaida na kuwalisha wanyama wake kwa nia ya kuongeza ubora wa chakula.

4 comments:

  1. Asante sana nimejifunza mengi nitafanya hivyo na shamba langu Ruhuwiko. Kwa hiyo tutafaidika na pia wanyama watafaidi. Asante sana. Je hii mimea hununuliwa katika vitalu au nitapata vipi?

    ReplyDelete
  2. Hii ni mimea ambayo inaota tu yenyewe porini, ni mingi sana nyanda za juu kusini mikoa ya Iringa, Songea, mbeya na Rukwa. Unachotakiwa kufanya ni kukusanya mbegu zake zilizokauka (zinakuwa na rangi ya kijivu/kahawia) kisha unazipanda moja kwa moja shambani

    ReplyDelete
  3. Ahsante ntaangalia mara nyingine nitakapokuwa Songea.

    ReplyDelete
  4. Nipo Tunduru. Je, mmea huu hufaa hata katika hali ya joto yetu?

    ReplyDelete