KURASA

Sunday, January 3, 2010

MVUA NA MIUNDO MBINU YETU

Jamani heri ya mwaka mpya kwenu nyote, namshukuru MUNGU niko buheri wa afya, Leo nitawaonyesha baadhi ya picha zinazoonyesha tabu tunayopata tukiwa field kutokana na madhara ya mvua kwenye barabara ambazo si za lami, kwa kweli kuna sehemu hata gari ikiwa na 4wheel drive inaweza isipite, pia kunatakiwa uzoefu wa kuendesha kwenye barabara hizo, kama wewe ni dereva wa mjini kwenye lami tu basi kazi utakuwa nayo

TANGA







MANYARA


RUKWA





RUVUMA


Hivi mnategemea kwa kutumia barabara hizi mkulima ataweza kweli kusafirisha mazao yake na kuyapeleka mjini kwenye masoko au mazao hasa yale yanayooza haraka kama matunda na mboga mboga si yataharibikia shambani.

4 comments:

  1. Heri na wewe kakangu. Ahsante kwa taswira nzuri, Hiyo picha ya mwisho ya Ruvuma naikumbuka ni njia ya kwenda Mbamba-by. Duh sehemu hizo mtu unaenda kama ni lazima uenda la sivyo mmmmmhhhhh!!

    ReplyDelete
  2. Ndio tanzania yangu niipendayo. Wakati watu wanakufa njaa upande wa pili wa barabara, wengine wanaozewa na mazao. Niliwahi kuandika kuhusu jambo kama hili hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/02/tanzania-yangu-niipendayo-barabarani.html
    lakini kwa taswira hizi mwanana ntaomba kuziongeza kisha niirudie makala kwani makala zetu hazi[itwi na muda kama hazijatekelezwa.
    Blessings

    ReplyDelete
  3. Kweli mwenda kwao si mtoro Dada Yasinta unapajua kwenu hata kwa kupapasa tu,
    Mzee wa changamoto tumia tu hizi picha ndio maana sikuzipiga mihuri kwa sababu nilihisi zinaweza kutumika maradufu

    ReplyDelete
  4. Ukizikuta kwangu usishangae mkuu.
    Na mvua hizi za sasa, nafikiri kuna sehemu zitageuka visiwa vya muda

    ReplyDelete