KURASA

Saturday, January 23, 2010

VODACOM NA WAATHIRIKA WA MAFURIKO



Katika kuthamini waliopatwa na maafa ya mafuriko pote nchini kampuni ya simu ya VODACOM imeanzisha kampeni inayojulikana kama RED ALERT itakayowawezesha wateja wake kuchangia kadri wawezavyo ili kuwasaidia waathirika wa mvua na mafuriko pote nchini

Kwa ufupi ni kwamba ukitaka kuchangia waliopatwa na maafa pote hapa nchini kama Kilosa, Same, Tanga na Dodoma basi tuma neno MAAFA kwenda namba 15599 na hapo utakatwa shilingi 250/= (PAMOJA NA KODI) kama mchango wako kwa waathirika wa mvua na mafuriko.

Serekali imefanya tathmini na kutangaza kwamba kiasi cha shilingi billioni 10 zinahitajika ili kuweza kuwasaidia wale walioathirika mpaka hali itakapo tengemaa, na kampeni hii ni kuanzia tarehe 24th January 2010 paka 30th January 2010 (wiki moja tu)

3 comments:

  1. Unaweza kukuta nusu ya hizo bilioni ni allowances za wakubwa kwenda kukagua maendeleo ya mafuriko!! :-(

    ReplyDelete
  2. Afadhali kidogo. Niliwahi kuwalalamikia hawa (kimakosa) kwa kukomalia mashindano ya urembo tu na kutojali mambo ya msingi. Wameamka!

    Tazama hapa: http://matondo.blogspot.com/2010/01/makampuni-yetu-na-jinamizi-la.html

    ReplyDelete
  3. Chib ni kweli wanatumia wenyewe zaidi maana uzinduzi ulikuwa mkubwa sana na watu kibao walipewa fulana za bure, sasa hizo hela zote si wangepeleka tu kule moja kwa moja na hii kampeni wangeizindulia kule

    Masangu (prof) nahisi walikusikia maana na wao pia wanasoma hizi blog zetu lakini wao kama kampuni wametoa kiasi gani maana kule ndiko kwenye wateja wao pia

    ReplyDelete