KURASA

Monday, February 8, 2010

DARAJA LINALOISHI



Huko nchini INDIA sehemu za CHERAPUNJEE ambako ni eneo tengefu lenye majimaji ambako wanapatikana watu jamii ya KHASIS huwa wanatumia mizizi ya miti jamii ya mipira kutengeneza madaraja kwa ajili ya matumizi ya kila siku.



Wanachofanya ni kuielekeza mimizi ya mti husika kukua kuelekea upende wa pili wa mto, kwa kawaida miti hii huwa na mizizi ya chini ya udongo na ile ambayo hutokea kwenye matawi na kuelea elea hewani, kwa hiyo mizizi hii inayoelea hewani huongozwa kukua kufuatana na matakwa ya watu hao mpaka upande wa pili na hapo huachiwa ikue kwa kuingia ardhini ili kupata uimara unaohitajika.



Ili kupata daraja kamili na lenye uimara unaohitajika zoezi hili huchukua kati ya miaka 10 hadi 15, na yapo madaraja yenye hadi refu wa futi 100 na huwa na uwezo wa kuhimili jumla ya watu 50 kwa pamoja kama wote watakaa juu ya daraja husika. Kati ya madaraja hayo lililo maarufu zaidi hujulikana kama UMSHIANG DOUBLE DECKER ROOT BRIDGE ambalo kama jina lake lilivyo lina njia mbili ya juu na chini

DARAJA LA UMSHIANG


3 comments:

  1. Aisee una bonge la jicho la taswira. nimependa blog yako Bennet. Keep it up

    ReplyDelete
  2. Ninaamini sasa kuwa hakuna binadamu mahali popote ni mjinga.

    ReplyDelete
  3. Naona jamaa wanatumia resources zinawazunguka kupata solutions za matatizo yao kama madaraja kwani sehemu zingine duniani kuwa na daraja kila mmoja anaisubiri serikali kuu.

    ReplyDelete