KURASA

Thursday, January 6, 2011

DALILI ZA PANYA ZAONEKANA KILOMBERO

Dalili za kuwepo wanyama waaribifu aina ya panya zimeoneka wilayani kilombero na hivyo wakulima kutahadhariswa juu ya kuibuka kwa panya, panya hao wameanza kuonekana maeneo ya Mlimba, ifakara, Mgeta, na Mangula wilayani humo.



Pia kumekuwa na dalili ya kuibuka kwa viwavi jeshi baada ya mitego iliyotegwa katika vijiji vya Kiberenge, Mpanga na Mikoleko kuwanasa Nondo ambao ni dalili ya kuibuka viwavi jeshi

Dalili za panya hao na viwavi jeshi kushambulia mahindi na mpunga zimeoneka kiasi cha wiki kadhaa na kumfanya mkuu wa wilaya ya Kilombero Bw Evarist Ndikilo kuwasiliana na mkurugenzi wa wilaya hiyo ili kupata viuatilifu (dawa za kuua wadudu) ili kukabiliana na panya pamoja na nondo hao kabla madhara hayajawa makubwa.


Bw Ndikilo amewataka maafisa tarafa wote kutoa taarifa kwa Wakulima ili juhudi za kupambana na panya na viwavi jeshi ziwe za kushirikiana pamoja na Wakulima ambao ndio wadau wakuu wanaoufanya mkoa wa Morogoro kuwa ghala la Taifa

No comments:

Post a Comment