KURASA

Thursday, July 7, 2011

MATIKITI MAJI - water melon




Ili kulima matikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha, matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano Matango, maboga na maskwash.
Kwa mtu ambaye anaanza kilimo yatampa tabu kidogo tofauti na Yule ambaye ana ujuzi kidogo na mambo ya kilimo kwa sababu yanahitaji umakini kiasi.

HALI YA HEWA
Mimea hii haihimili hali ya joto kali sana, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu, inastawi vizuri kwenye kuanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa machi mpaka wa septemba .

UPANDAJI
Panda kwa kutumia Mbegu zinazouzwa madukani, ukitumia Mbegu kutoka kwenye tikiti ulilonunua linaweza likawa ni hybrid na matokeo yake matikiti yatakayozaliwa hayatakuwa bora kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Panda Mbegu yako moja kwa moja kwenye shamba, usinunue miche au kupanda Mbegu kwenyemifuko ya plastiki halafu ndi uhamishie shambani, panda Mbegu mbili sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 2 - 3 kutoka mstari hadi mstari, baada ya siku chache Mbegu zitaanza kuota, baada ya kama wiki 2 katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi, angalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Unaweza kupandishia udongo kwenye mashina na hii itasaidia kupunguza maji yasituame kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa matunda yenye, na wakati wa kuanza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe mimea kwa kuielekezea kwenye waya na kufungia

MCHE ULIOCHIPUA


UANGALIZI
Miche ikiwa imetambaa kiasi unaweza kuweka matandazo kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu, unaweza kuweka samadi au mbolea za viwandani, mimea ikiwa midogo tumia zaidi mbolea zenye nitrojen na utumie zaidi mbolea za potasiam mara baada ya maua kutokeza hadi matunda kukomaa, matawi yakifikia urefu wa mita 2 kata mbele ilikuruhusu kutoa matawi na hivyo kupata maua mengi zaidi hatimaye mavuno zaidi

MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja, maua dume ambayo ni madogo zadi hutoka kwanza yakifuatiwa na maua jike ambayo ni makubwa zaidi, usipoona maua dume na jike kuna tatizo mfano maji kidogo yalimwagiliwa, upungufu wa viritubisho kwenye udongo, hali ya hewa ni joto/baridi sana n.k
Uchavushaji kwenye matikiti hufanyika na wadudu, kama huwaoni wakifanya kazi yao unaweza kufanya mwenyewe, muda mzuri ni wa asubuhi, unakata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi

UCHAVUSHAJI KWA MKONO


UVUNAJI MATIKITI
Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi

MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kjupata dawa sahii, dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia kwa mashambulizi ya fangasi

39 comments:

  1. Mkuu tunda hili bwana, sijui nikuambie nini, safi saana ...TUPO PAMOJA MKUU KWA HAYA UNAYOTUPA, YANATUSAIDIA SANA, SHUKURANI!

    ReplyDelete
  2. Asante sana Mkuu, Nadhani kila nilichohitaji kama Muongozo wa zao hili Nimeshaupata...
    Ntakupa mrejesho pale nitakapoanza kupanda mpaka navuna...
    Umesema wakati mzuri kupanda ni March- Septemba, je kwa kilimo cha umwagiliaji?? Wakati wowote katika mwaka unafaa??

    Asante sana,
    Abdul Latif

    ReplyDelete
  3. Kaka nimeanza kulima tikiti ila nimekatishwa tamaa na wadudu wanaokata majani angali mche unaanza kuota nitumie dawa gani? Pili naweza tumia njia gani ili kuzuia tikiti lisiingize njano pale linapo lalia zaidi ya kuweka waya au net ambozo gharama yake kubwe na inawezekana kwa sehemu ndogo?

    ReplyDelete
  4. wadau mimi nimelima matikiti hapa dodoma..hii ni wiki ya kukamilisha siku 90..matunda yametoka vizuri ila yanapasuka...naona kama 1/4 ya shamba yanazidi kupasuka...hapa nini shida

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kupasuka kwa matiki maji ni kwa sababu yamekunywa maji mengi sana,tikiti maji hua linahitaji maji mengi pindi linapokua dogo,ila kadili linavyozidi kukua unapunguza maji

      Delete
  5. nimelibenda darasa la kilimo sana
    sana kwa hili tunda ya tikiti

    je nikitaka elimu zaidi za vitendo na mwalimu
    nawezaje kukupata iliunisaidie kwa hili swala?
    na je katika soko tikiti linaweza kukuingizia kiasi gani kwa shamba la eka moja ukilima vizuri

    JOSEPH MSAFIRI
    +255 713 466 691

    ReplyDelete
  6. Asante kwa elimu nzuri uliyotupa ni nzuri sana sana ila inabidi tuweke kwenye vitendo. Nina swali,Je inahitaji kiasi gani ili niweze kuanza kilimo hiki cha matikiti?

    ReplyDelete
  7. Asante kwa ujuzi wako. lakini naswali kidogo hivi kuna ukweli wowote kupunguza matikiti ya mwanzo ni kukuza mengine?

    ReplyDelete
  8. Ambele Rimbert

    Kwa kweli matikiti ni dili hata mimi nimeanza kilimo hiki. Wandugu tuamke hususani vijana.

    0713 871203

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka naomba unijuze unatumia bei gani kulima mpaka kuvuna kwa ekari moja na Mimi nataka kulima

      Delete
  9. ni kilimo kizuri sana ila mnaolima jaribuni kutoa mrejsho basi tusaidien tunaotaka anza lima,mm nimelima wiki tatu zijazo navuna ntarud kutoa mrejesho tuombeane tu mambo yaende kama matumaini yalivo sasa

    ReplyDelete
  10. ni kilimo kizuri sana ila mnaolima jaribuni kutoa mrejsho basi tusaidien tunaotaka anza lima,mm nimelima wiki tatu zijazo navuna ntarud kutoa mrejesho tuombeane tu mambo yaende kama matumaini yalivo sasa

    ReplyDelete
  11. hongera kwa kazi ya kuelimisha jamii juu ya setor muhimu yakilimo. namba mawasiliono yako kupitia.E-MAIL socialesungrand@gmail.com

    ReplyDelete
  12. Nahitajikufahamu jinsi yakuandaa shamba kwasababu sijawahi kulima ila kwasasa nahitaji kuingia kwenye kilimo cha matikiti

    ReplyDelete
  13. Nataka nianze Kama kijana fursa ndo izo

    ReplyDelete
  14. Jamani zasaiz! Natakakulima kibaha tikiti maji, naweza kutegemea mvua peke yake kwakilimo hiki?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hey samahan.. Vp ushaanza kulima pandeza kibaha na zinakubal

      Delete
  15. Na mimi pia nataka lima Kibaha mwaka unaoamza 2016 tunahitaji data wadau

    ReplyDelete
  16. Jaman mm sijawahi kulima hata mara moja lakini nataka kuanza kulima, sasa naombeni mnisaidie ni wakati gani mzuri, jinsi ya kuandaa shamba na upandaji wake pia jinsi ya kutunza shamba wakati yako shambani. Jinsi yanavyo zaa kwa kila shina moja, na je kwa hekari moja unaweza kutoa matunda mangapi km yakistawi vizuri? Contacts 0712647555 plz I need help for it.

    ReplyDelete
  17. Thanks blog yako nzuri na hasa content kwenye suala la kilimo,mifugo na uvuvi

    ReplyDelete
  18. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  19. Nimekupata vyema sana mtaalamu wa matunda na mimea.

    Asante sana, lakini vipi kuhusu kilimo cha mbogamboga kama vile
    Kale
    Spinach
    Sukuma week
    Mchicha na kadhalika.

    ReplyDelete
  20. mkuu vp kuhusu dawa za kuzuia magonjwa yaanayoshambulia matikiti

    ReplyDelete
  21. ahsante kwa somo zuri! vipi kwa maeneo ya nyanda za juu kusini especial Iringa naweza kulima pia?

    ReplyDelete
  22. Kwa Iringa huwezi kulima matikiti sababu ya baridi, matikiti kupasuka maana yake umemwagia maji mengi, huwa hayataki maji mengi wakati wa kukomaa, kuhusu magonjwa kata majani yaliyoathiriwa na uende nayo duka la dawa ili wajue ugonjwa gani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hello Naweza pata namba yako? Yangu ni 0716 684272 erica

      Delete
    2. Utaacha muda gan kumwagia il yasipasuje

      Delete
  23. nashukuru blogger kwa status nzuri,,,,,hii shughuli ya zao hili kwa ukanda wa rufiji kulima heckta 1-2 inagharimu kiasi gani kwa kilimo cha umwagiliaji/cha cha mvua,,,,vipi demand kwa soko la nnje ya dar na nnchi likoje,,,naona mwitiko ni mkubwa kwa vijana kufanya kilimo

    ReplyDelete
  24. Mkuu, mie nataka kulima maeneo yakisanga Kisarawe, nipe mwongozo mkuu.

    ReplyDelete
  25. mkuu matikiti yangu yanakaribia kukomaa, tatizo sijui soko liko wapi mi nipo maeneo ya Hai-kilimanjaro

    ReplyDelete
  26. mkuu matikiti yangu yanakaribia kukomaa, tatizo sijui soko liko wapi mi nipo maeneo ya Hai-kilimanjaro

    ReplyDelete
  27. msimu wa mwezi wa Tisa( ni kiangazi kwa mkoa wa Singida) na mwezi wa 12 na 1 ni mazima.... Swali je? Ninaweza kupata mavuno mazur kama ntavuna kipind cha masika?

    ReplyDelete
  28. Je unawez kuanzisha kilimo cha matikiti kisarawe?

    ReplyDelete