KURASA

Tuesday, May 8, 2012

N'DAMA - mbegu bora ya ng'ombe inayohimili ugonjwa wa ndorobo

Mbegu hii ya ng'ombe hupatikana zaidi kwenye nchi za Afrika ya magharibi, kaskazini na kati katika nchi za Guinea, Sierra Leone, Liberia, Mali na Ivory Coast ndiko wanakopatikana zaidi. Aina hii ya ng'ombe haina nundu tofauti na ng'ombe wetu wa asili nchini Tanzania, wana pembe kati ya wastani hadi kubwa kabisa na wana miili yenye misuli ya hii huwafanya wawe bora katika uzalishaji wa nyama ingawa hawana miili mikubwa. uzazi wa kwanza kwa majike ni baada ya kufikia miaka mitatu (3)

N'dama wanasifika duniani kote kutokana na uwezo wao wa kuhimili ugonjwa wa ndorobo (trypanosomiasis) unaosambaza wa mdudu ajulikanaye kama mbung'o (tse tse fly) ambaye pia husambaza ugonjwa wa malale kwa binadamu.

No comments:

Post a Comment