Zao la muhogo ni muhimu sana
kwa Tanzania
zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya
zao la muhogo na mazao mengine kama vile
kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na
wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu
ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani
Muhogo hustawi vizuri katika
maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile
vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm
750 - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi
vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali
ya ukame.
TEKNOLOJIA ZILIZOPO
- Mbegu bora za
muhogo
Mpaka sasa hivi
kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato
na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
- Naliendele
- Kiroba
Huzaa tani 25 –
30 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa
kuanzia miezi 9 toka ipandwe.
- Mbinu bora za
kilimo cha muhogo
- Uandaaji wa shamba
Shamba
liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
-
Kufyeka shamba
- Kung’a na kuchoma visiki
- Kulima na kutengeneza matuta
·
Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
Mbegu
zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa
vizuri.
·
Upanadaji
Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
-
Kulaza ardhini (Horizontal)
-
Kusimamisha wima (Vertcal)
-
Kuinamisha ( Inclined/Slunted)
Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
Inashauriwa
urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya
macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).
Nafasi ya
kupanda:
Kwa upandaji wa
shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine,
inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na
shina hadi shina ni mita 1.
·
Palizi:
-
Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya
kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha.
Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka
ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na
magugu.
-
Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya
kuuwa magugu.
-
Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa
kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
-
Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.
·
Uvunaji:
Mihogo inaweza
kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika
katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo
hupungua.
· Usindikaji bora
Usindikaji bora
wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
-
Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
-
Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za
mihogo
-
Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.
Njia bora za usindikaji
-
Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa
chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa
kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii
hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
-
Kwa kutumia mashine aina ya chipper
-
Mashine
hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa
ajili ya mihogo mitamu/baridi.
Matumizi ya Muhogo
-
Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama
chakula au kutengeneza unga
-
Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama
vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile
biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
-
Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa
nyingine kama vile wanga.
iii MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
·
Magonjwa
Kuna magonjwa
mawili ambayo ni muhimu sana
na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.
a)
Ugonjwa
wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia
katika
muhogo
Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye
miinuko iliyo na urefu chini ya mita 300
na unapatikana kidogo sana
kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei
kabisa.
Visababishi:
Matokeo ya uchunguzi wa awali
unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweuupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.
Dalili za Ugonjwa
Sehemui
zote za muhogo zinaweza kuonyesha
dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni
kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa
kulinganisha.
-
Kwenye majani
Dalili ya
kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae
huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.
Dalili ya pili:
Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya
mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya
lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea
kwa muda wa wiki kadhaa.
-
Kwenye shina
Huonekana
kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza
kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la
nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni
kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea
chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.
-
Kwenye mizizi
Kwa kawaida
hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na
kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za
mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kama
kizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.
Tishu inayo
zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi
huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila
kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.
Uambukizaji na ueneaji
Ugonjwa wa CBSD
unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa
vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa.
Kwa kuwa muhogo
kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye
sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
Kwa aina
zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni,
dalili mbaya sana
hutokea wakati ugonjwa ukigundulika
katika hatua za mwanzo.
Uchunguzi
umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana
na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha nzi weupe
(White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.
Udhibiti/Kuzuia
ü
Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa
CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa.
ü
Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa
kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa
kuchipua.
ü
Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za mhogo
ambazo zinastahimili uambukizo wa magonjwa.
ü
Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya
kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.
ü
Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya
kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
ü
Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora
zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana .
ü
Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya
kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD
b)
Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani
Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwamara ya
kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine
nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa
unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika.
Katika viwango
vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana
kutokana na CMD ni kati ya 15% – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18
zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.
Visababishi
Tangu ugonjwa
wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana
kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na
matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na nzi mweupe (white fly).
Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha
utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:
·
Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya
Africa cassava mosaic virus
· Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya
Afrika mashariki (East
Africa cassava mosaic virus)
·
Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya
India (Indian cassava mosaic virus)
Dalili za ugonjwa wa
batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
Dalili
hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri
Sehemu zisizokunjamana za
kutolea hewa na hufahamika katika hatua za
Awali za ukuaji wa jani.
Sehemu za
kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unaji-
tokeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au
majani madogo yaliyoharibika.
Majani
yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa
Sehemu zenye rangi
ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
Mmea hudumaa na
majani machanga hupatwa na uvimbe.
Kloritiki ya
jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe
yenye kijani kidogo au
kupauka kuliko ilivyo kawaida.
Uambukizaji na uenezaji
Ukoma wa mhogo huambukizwa
kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida
hutumika kuzalishia mmea.
Pia huenezwa na inzi mweupe
(white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi au
Mbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius
disperses R) pia huambukiza mihogo
katika nchi za
Afrika na India
Usambazaji wa
vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa CMD katika
Maeneo
mapya.
UHIBITI NA KUZUIA
-Hatua ya
msingi ya kuzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa
Mmea ambao hauna uambukizo
wowote.
-Ubora wa mashina
unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile
Mihogo iliyoambukizwa ambayo
inaonekana wakati wa kuchipua
-Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna
mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMD
inaangamizwa kwa kuchomwa
moto.
-Hakikisha kuwa unatunza shamba na kuwa safi ili kupunguza wadudu
waenezao CMD.
-Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya
dalili za ugonjwa wa CMD>
·
WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU
-
Cassava Mealy Bug (CMB)
Wadudu hawa
hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake
ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa
mmea kwa ujumla. Vile vile urefu
kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.
-
Cassava Green Mites (CGM)
Wadudu hawa
hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.
-
White Scales
Hawa ni weupe
na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili
vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.
-
Mchwa
Hawa
hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
-
Wanyama waharibifu
Hawa
hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama
vile nguruwe, panya, wezi, n.k
Udhibiti/Kuzuia
Kwa upande wa
wadudu wanweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:
ü
Kutumia dawa za kuulia wadudu
ü
Kutumia wadudu marafiki wa wakulima
Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.
nilifurahi kuona mihogo maana ndicho chakula nilichokulia wakati naishi Nyasa/Lundo..na baada ya kusoma na kuona gojnjwa na kila kitu nimeogopa kweli..Ahsante kwa hili kaka Bennet nitawaambia ndugu zangu wa nyasa wawe macho.
ReplyDeleteDaaaaah safiiii sanaaaaa
ReplyDeleteNimependa maelezo yako kuhusiana na magonjwa ya muhogo na udhibiti wake.
ReplyDeleteAsante sana.
Asante kwa elimu ya kilimo cha mihogo. Napenda kuuliza hizo aina za mihogo kama Naliendele naweza kuzipata wapi kwa hapa Mwanza???
ReplyDeleteAsante kwa elimu ya kilimo cha mihogo. Napenda kuuliza hizo aina za mihogo kama Naliendele naweza kuzipata wapi kwa hapa Mwanza???
ReplyDeleteumejitahidi lakini hujazingatia uhalisia wa eneo mfano mnama ya kuzuaia mchwa eleza bayana
ReplyDelete