Hii ni aina ya mbuzi wa maziwa ambao asili yake ni uswizi
katika eneo la Obertoggenburg kama wanavyoitwa, hii ndio mbegu ya mbuzi wa
maziwa wa zamani zaidi kuliko zote. Kwa hapa Tanzania wanapatikana Uyole, SUA
na Tengeru (hivi vyote ni vyuo vya mifugo)
UZALISHAJI
Mbuzi hawa wanauwezo wa kuzalisha maziwa wastani wa lita
mbili kwa siku au zaidi, hawatoi maziwa mengi kama Saanen ila maziwa yao yana
kiasi cha mafuta kati ya 3% - 4%
MAUMBILE
Mbuzi hawa wana umbile la wastani lakini ni wakubwa kuliko
mbuzi wa kienyeji, kilo 55 kwa majike na kilo 75 kwa madume, wana rangi ya
kahawia (khaki) mpaka hudhurungi (brown)
pia wana mistari miwili usni yenye rangi ya maziwa au nyeupe kuanzia juu
mpaka kwenye pua (kama duma) huwa na viwele (udder) vikubwa na pia ni wazazi na
walezi wazuri, mara nyingi huweza kuzaa mapacha
HALI YA HEWA
Mbuzi hawa hawawezi kuhimili hali ya joto, bali hufanya
vizuri kwenye maeneo yanye baridi kama mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe,
Dodoma, Singida n.k. Wanahitaji chakula chakutosha ili kutoa maziwa mengi, pia
chakula kiwe na virutubisho kamili. Ingawa pia wanaweza kuchungwa kwenye maeneo
yenye ukame kiasi na wakaweza kufanya vizuri (good foragers)
TABIA
Mbuzi hawa huishi kwa makundi wakitoroka au kuingia kwenye
shamba la mazao basi huenda wote na hufundishika kirahisi sana hii husababisha
urahisi wa kuwafundisha kukamuliwa na mashine
Ahsante kwa dasara kakangu!!
ReplyDeleteVp hali ya hewa ya tanga hao mbuzi wanaweza kuishi nakuzaliana kama kawaida
ReplyDeleteVp hali ya hewa ya tanga hao mbuzi wanaweza kuishi nakuzaliana kama kawaida
ReplyDeleteTanga kuna hali za hewa kama tatu, maeneo ya Lushoto ni baridi mbuzi hawa wataishi vizuri, maeneo ya Amani, Kuze, Daluni ni wastani mbuzi hawa pia yatawafaa, ila huku pwani kwenye joto hawata kubali sana labda uwachanganye na wakienyeji kupata chotara
ReplyDeleteMawasiliano napatje?
Deleteahsantevipi kuhusu soko la maziwa ya mbuzi kuu.
ReplyDeleteNahitaji kununua mbuzi wa maziwa aina ya Saanen kama wanne hivi pamoja na mbuzi aina ya togenberg kama wanne hivi pamoja na madume yao hata moja moja,Is how much na je nitwapata wapi?
ReplyDeletemy phone numbers are +255 784 707 352 na +255 767 707 352
ReplyDeleteNawaitzj
ReplyDeleteNahitaji mbuz aina ya Alpine nitawapataje
ReplyDelete