Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
KURASA
▼
Tuesday, September 16, 2014
TRACTOR FOR SALE - TREKTA LINAUZWA
Tractor Massey Ferguson 3080, 2 wheel drive 90 HP kama mpya inauzwa kwa bei poa sana, na imewasili Tanzania tayari kutoka denmark, (serious buyers only) kwa mawasiliano zaidi na bei piga 004560248586 au 004553901576
Thursday, May 22, 2014
JINSI YA KUKATA MICHE YA MISOJI (MITIKI) marudio
MCHE KABLA YA KUKATWA (angalia mishale kujua sehemu za kukata)
Mche wangu niliukata na kuacha kiasi cha nchi mbili au pingili mbili za vidole kwa sehemu ya juu ya mzizi na kwenye mzizi niliondoa ile sehemu nyembamba ya chini, kwa kawaida hii sehemu ya chini hufa mara baada ya kupandwa kwa sababu sehemu nene/kubwa ya mzizi inayoachwa ndiyo huifadhi maji na chakula cha mmea, nadhani hapa nitakuwa nimemsaidia kama bado nipigie kwenye ile namba niliyokupa
KIPANDIKIZI TAYARI KWA KUPANDWA
Kumbuka wakati wa kupandwa lazima uweke kisahani ili kiweze kukusanya maji kwa ajili ya ukuaji mzuri, kama ni udongo unaotuamisha maji usiweke kisahani bali wekea kama tuta au mwinuko
WEKA KISAHANI KAMA UDONGO HAUTUAMISHI MAJI
WEKA TUTA KAMA UDONGO UNATUAMISHA MAJI
Tuesday, April 29, 2014
UANDAAJI WA MBEGU ZA MITIKI
Mbegu za mitiki ni lazima ziandaliwe kabla ya kusia kitaluni, hakikisha umeshaanda kitalu chako mapema na kiwe na udongo wenye rutuba ya kutosha, mwagia maji ya kutosha ili kama kuna magugu yaanze kuota na kung'olewa mapema, hii inasaidia kwa sababu mbegu za mitiki huchukua muda mrefu kuota, sasa ukianza kung'olea na mbegu hazijaota au miche ni midogo utakuwa unaing'oa na yenyewe
Kwa kila kilo moja ya mbegu ina hitaji ndoo ya maji lita 20, weka mbegu zako kwenye gunia au kiroba, kisha weka vitu vizito kama mawe ili kuhakikisha mbegu zako zinakuwa chini ya maji, kinyume na hapo zitaelea juu na hutapata matokeo mazuri katika uotaji, bila kufanya hivi mbegu zko hazitaota kwa wingi
Hili ni pipa la lita 200, linatosha kwa kilo 10, badilisha maji yako kila jioni na asubuhi kwa muda wa siku 7. kama utaweka maji mara mbili zaidi unaweza kubadilisha maji mara moja kwa siku, yaani kilo moja kwa maji lita 40. Kama kuna maji yanayotembea kama vijito vidogo basi unaweza kuloweka humo bila kuziondoa kwa siku 7.
Siku ya 8 anika mbegu zako juani, ni vizuri kama utaziweka kwenye bati ili zipasuke gamba lake na kusaidia uotaji
Panda mbegu zako kwa msitari, chora mfereji wenye kina cha sentimeta moja na uziweke kwenye huo mfereji mwanzo mpaka mwisho bila kuruka nafasi, acha nafasi ya sentimeta 18 - 20 kati ya fereji na mfereji kama inavyoonekena kwenye picha juu na chini
Baada ya wiki tatu mbegu zitaanza kuota na zitaacha kuota baada ya siku 65, uotaji ni kiasi cha 45% mpaka 50%, kilo moja ina wastani wa mbegu 800 mpaka 1000, kwa hiyo unaweza kupata mpaka miche 500 kwa kilo moja, Mbegu zinapatika kwa WAKALA WA MBEGU WA TAIFA kwa bei ya shilingi 9000/= kwa kilo, wanapatikana Morogoro mjini, eneo la Kihonda ukitokea msamvu kama unaelekea Dodoma ni kama kilometa 3, unaweza kupanda daladala, bodaboda au hata taxi na ukafika
Friday, March 28, 2014
TOGGENBURG - AINA BORA YA MBUZI WA MAZIWA
Hii ni aina ya mbuzi wa maziwa ambao asili yake ni uswizi
katika eneo la Obertoggenburg kama wanavyoitwa, hii ndio mbegu ya mbuzi wa
maziwa wa zamani zaidi kuliko zote. Kwa hapa Tanzania wanapatikana Uyole, SUA
na Tengeru (hivi vyote ni vyuo vya mifugo)
UZALISHAJI
Mbuzi hawa wanauwezo wa kuzalisha maziwa wastani wa lita
mbili kwa siku au zaidi, hawatoi maziwa mengi kama Saanen ila maziwa yao yana
kiasi cha mafuta kati ya 3% - 4%
MAUMBILE
Mbuzi hawa wana umbile la wastani lakini ni wakubwa kuliko
mbuzi wa kienyeji, kilo 55 kwa majike na kilo 75 kwa madume, wana rangi ya
kahawia (khaki) mpaka hudhurungi (brown)
pia wana mistari miwili usni yenye rangi ya maziwa au nyeupe kuanzia juu
mpaka kwenye pua (kama duma) huwa na viwele (udder) vikubwa na pia ni wazazi na
walezi wazuri, mara nyingi huweza kuzaa mapacha
HALI YA HEWA
Mbuzi hawa hawawezi kuhimili hali ya joto, bali hufanya
vizuri kwenye maeneo yanye baridi kama mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe,
Dodoma, Singida n.k. Wanahitaji chakula chakutosha ili kutoa maziwa mengi, pia
chakula kiwe na virutubisho kamili. Ingawa pia wanaweza kuchungwa kwenye maeneo
yenye ukame kiasi na wakaweza kufanya vizuri (good foragers)
TABIA
Mbuzi hawa huishi kwa makundi wakitoroka au kuingia kwenye
shamba la mazao basi huenda wote na hufundishika kirahisi sana hii husababisha
urahisi wa kuwafundisha kukamuliwa na mashine
FAYC KAY TRADING LTD - WAUZAJI WA MATREKTA NA ZANA ZA KILIMO
Hawa ni wajasiliamali wa kiTanzania waishio nchini Denmark, wanauza zana za kilimo zilizotumika (used) kama matrekta na majembe yake, matrailer, irrigation water pumps, Chemicals sprayer, harrows, planters, combining harvesters n.k
Unaweza kuwasiliana nao kwa namba zifuatazo wakiwa Denmark 0004560248586 au 0004527201580 unaweza kuwapigia au kwa kutumia whats up. pia wana email zifuatazo charlesurban00@hotmail.com au sweetfaydat@gmail.com
Wanazo brand za kimataifa zenye ubora wa hali ya juu kama Massey Ferguson, John Deere, New Holland, Ford na nyinginezi nyingi
Wednesday, March 26, 2014
KILIMO BORA CHA MDALASINI - CINNAMON
Mti wa mita 10 au zaidi. Hutoa machipukizi na kuota miti zaidi ya mmoja kwenye shina moja na kuongeza mavuno mengi, haya mashina mapya yasing'olewe bali yaachwe yakue na kuwa mti mkubwa.
AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)
HALI YA HEWA NA UDONGO
· Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
· Udongo wenye rutuba
· Joto kwa wingi
· Hewa yenye unyevunyevu
KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
· Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
· Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
· Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
· Panda miche wakati wa masika
· Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka
UTUNZAJI
· Acha machipukizi kwenye shina
· Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
· Weka shamba katika hali ya safi
· Zuia magonjwa kama.
- Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.
KUVUNA
· Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
· Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
· Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
· Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
· Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
· Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
· 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
· Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini
MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
· Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
· Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
· Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
· Dawa ya ngozi
JINSI YA KUTUMIA
· kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk
· Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula
MANUFAA
· Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
· Gharama ndogo ya uzalishaji
· Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
· Magonjwa na wadudu ni kidogo
· Rahisi kuchanganya na mazao mengine
· Nguvu kidogo, kipato kikubwa.