Mtama ni kundi
la mbegu ndogo aina ya mazao ya nafaka au nafaka ambayo kwa jina la kisayansi unajulikana kama
(Sorghum bicolor), ni mazao yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe Mtama hutoa
mazao mengi hata kwenye hali ambayo haifai kwa kilimo cha aina nyingine za
mazao ya nafaka. Mtama una uwezo mkubwa wa kustahimili ukame.
Mtama
unaweza kutumika kwa kuchemshwa na kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa
uji, kutengenezea vinywaji kama vile bia, kuoka mikate, na aina nyinginezo za
vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile
hay na sileji. Mtama unastawis vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa
milimita 400 – 700 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu
zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi.
Mtaama
unafaa pia kwa sehemu kame zenye wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto
18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto 25-30°C ili kukua
vizuri. Mtama hauwezi kuvumilia barafu. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za
udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye
udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza
kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye
chumvi kuliko yalivyo mahindi.
Aina za
mtama
Kwa jumla kuna aina zaidi ya 30 za mtama zinazolimwa kama
chakula. Mtama hustawi vizuri kwenye joto ikivumilia pia ukame. Hivyo ni nafaka
muhimi kwenye maeneo yabisi za Afrika. Katika miaka ya nyuma kilimo chake
kiliachwa mara nyingi kwa ajili ya mahindi kwa sababu mahindi huleta mazao
makubwa zaidi kwa ekari. Lakini wakati wa ukame mahindi ni hasara na watu
hurudi-rudi kwenye kilimo cha mtama.
Aina za
mtama zinatofautiana kulingana na rangi zake, kuna nyeupe, nyekundu, na
kahawia. Mbegu za asili huwa zinachavushwa kwa urahisi zaidi lakini mavuno yake
huwa ni hafifu ukilinganisha na mbegu za kisasa. Hata hivyo, aina za kisasa
zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi zinapopandwa kwa kufuata kanuni za kilimo
bora.
Serena:
Ina punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na
hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara,
ambapo huweza kuzalisha kiasi cha kilo 3,000 kwa hekari moja. Ambapo
zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana
na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.
Seredo:
Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye
eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua
baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni
ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha kilo 5000 kwa hekari moja. Ina uwezo wa
kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya
kahawia kwenye majani.
Gadam: Inafanya
vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina
hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia
bungo na ugonjwa wa majani.
Hakika na
Wahi: Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo
cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba
yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa
aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.
Utayarishaji
wa shamba na kupanda
Kwa
kawaida mtama hupandwa kwa kutumia mbegu. Mbegu hupandwa shambani moja kwa moja
baada ya shamba kuandaliwa, lakini pia zinaweza kurushwa shambani, kasha
zikavurugwa pamoja na udongo. Unapaswa kutayarisha shamba la kupanda mtama, iwe
ni kwa ajili ya malisho au chakula kabla mvua za msimu hazijaanza. Zao hili
hufanya vizuri zaidi kwenye udongo ulio laini. Linaweza pia kupandwa kwenye
udongo ambao haukulimwa vizuri na bado ukaota vizuri.
Nafasi:
Mtama unaopandwa kwa ajili ya malisho, unaweza kupandwa kwa nafasi ya sentimita
75×10. Aina za mtama ambazo zinalengwa kwa ajili ya lishe kwa binadamu na
wanyama, zinahitaji nafasi kiasi cha sentimita 60×20. Nafasi hutoa mwanya wa
kuwa na kiwango kikubwa cha malisho. Mkulima anaweza kupanda mbegu za mtama
kiasi cha kilo 2.4-3.3 kwa hekari moja. Ni mara chache sana mbegu hupandwa
kwenye vitalu na kuhamishiwa shambani baadaye.
Kupanda:
Mtama hupandwa mvua zinapoanza kunyesha. Mbegu ni lazima zifukiwe ardhini usawa
wa sentimita 3 kwenda chini, hii itasaidia kuepuka kuota wakati ambao si msimu
kamili wa mvua. Pia zinaweza kufukiwa kiasi cha sentimita 2 wakati ardhi
inapokuwa na unyevu. Mtama unahitaji rutuba ya hali ya juu wakati wa kupanda na
wakati wa kuota. Ni vizuri kutumia samadi au mboji iliyooza vizuri wakati wa
kuandaa shamba.
Mseto:
Unaweza kupanda mtama mseto na mazao jamii ya mikunde, na kuongeza mboji
shambani mwako. Hii inaweza kuwa njia nzuri zaidi ya kupata virutubisho
vinavyohitajika. Mseto wa mazao jamii ya mikunde inashauriwa iwe ni kama vile
maharagwe, kunde, n.k
Uangalizi
na utunzaji
Ni lazima
kung’oa baadhi ya mimea inapokuwa na urefu wa sentimita 30, au siku 30 baada ya
kupanda, ili kuwa na uhakika wa nafasi ya sentimita 10 kati ya mstari na mstari
kwa mtama unaokusudiwa kwa ajili ya malisho, na nafasi ya sentimita 20 kati ya
mstari kwa mtama uliokusudiwa kwa ajili ya chakula na lishe ya mifugo.
Palizi ya
mkono ifanyike walau mara mbili. Shamba la mtama ni lazima liwekwe katika hali
ya usafi na kutokuruhusu magugu wakati wote hasa katika kipindi cha mwanzoni.
Ile mbegu ya mtama yenye Rangi nyekundu kwa Jina la kienyeji inaitwa bukula!! Inafaa sana kwa Uji na hata ugali unga wake ukichanganywa na ungwa wa muhogo!! Je? Maeneo ya pwani hayafai kwa kilimo cha mtama!? Na hii mbegu inajulikana kitalaamu? Au hapana!!
ReplyDeleteKweli mtama hutibu maradhi ya sukari
ReplyDelete