KURASA

Monday, December 15, 2008

MAGONJWA YA SAMAKI NA TIBA

Kuna magonjwa mengi ya samaki yanayosababishwa na fangasi, bacteria, protozoa, parasites, virus na mazingira yenyewe. Hapa nitajaribu kuongelea magonjwa machache ambayo mimi ninauzoefu nayo yaani yameshanitokea na nikapambana nayo

Ichthyosporidium (WHITE SPOTS)
Huu ugonjwa kwa kifupi hujulikana kama ICHI, husababishwa na fungus ambao huingia kwa kupitia ngozi na kisha kushambulia maini na figo.




Dalili zake ni samaki kuogelea kwa kupindapinda au kivivu, tumbo kuonekana kama halina kitu (hollow) na alama nyeupe nyeupe kwenye mwili wa samaki

Tiba yake ni pottasium per manganate kwenye maji, Phenoxethol 1% kwenye chakula na Chloromycetin kwenye chakula, dawa zote zinapatikana kwenye maduka (pet shops). kwa kawaida ICHI wana miznguko miwili ya maisha, akizaliwa anaogelea na kujishikiza kwenye mwili wa samaki, kisha anashuka chini kwenda kuzaana (replitications)na kurudi kwenye mwili wa samaki tena. Kwenye hatua hii pottasium per manganate ndio inafanya kazi ya kuzuia ICHI kurudi tena kwenye mwili wa samaki


LEECHES
Ugonjwa huu husababishwa wadudu wa nje (external parasites)ambao hujishikiza kwenye mapezi na mikia ya samaki. Dalili yao ni kuwaona wakiwa wamejishikiza kwenye sehemu zilizotajwa na ndani ya ngozi, huwa na umbo la kama moyo na rangi ya kijivu/nyeupe



Kwa sababu dalili zinaonekana wazi kwa macho, mara nyingi ugonjwa huu huingia kwenye tank lako kwa njia ya konokono na majani

Matibabu ni kuwaweka samaki ndani ya maji yenye chumvi kiasi cha asilimia 2.5, baada ya dakika 15 leeches wengi watakuwa wamedondoka chini na wale watakaobaki unaweza kuwatoa kwa kutumia kibanio (forceps)
Tiba nyingine ni kwa kutumia Trichlorofon kiasi cha 0.25m/l (robo miligram kwa lita moja ya maji) majani yanaweza kuondolewa ugonjwa kwa kutumia potassium permanganate kiasi cha 5mg/l (miligram 5 kwa lita moja ya maji)

KUOZA MKIA NA MAPEZI
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria, dalili zake kubwa ni kuwa na rangi nyekundu au rangi ya udongo (hudhurungi) kama damu imevilia kwenye kona za mapezi na mkia na kisha baadae sehemu hizi hunyofoka na kubakia kibubutu.




Sababu kubwa ni kuumia kunakosababishwa na kujigonga au madume kupigana, TB pia inaweza kusababisha hali hii

Tiba yake ni kwa kutumia antibiotics kama tetracycline au chloramphenicol kiasi cha 20-30mg/l (miligramu 20-30 za dawa kwa lita moja ya maji)au mili gramu 250 (1 capsule) kwa chakula cha gramu 25

ingawa magonjwa mengi yanasababishwa na vimelea lakini mazingira nayo pia yanachangi katika kuongeza kasi ya magonjwa, ukizingatia yafuatayo unaweza kuwakinga samaki wako.
(a)Nunua samaki wako toka kwa mtu mwenye uzoefu wa kufuga na ambaye unauhakika samaki wake hawana magonjwa

(b)Samaki wapya watengwe kwa muda kwenye chombo kingine (hospital tank0 kwa siku kadhaa kabla ya kuchanganywa na wengine

(c)hakikisha samaki wako hawali zaidi ya kiwango chao na kuvimbiwa, lisha kwa kipimo sahihi

(d)Epuka kuwaweka samaki kwenye mazingira mabaya kama maji machafu, kuweka samaki wasiopatana pamoja, kuwasumbua kwa kuwashikashika na kugonga gonga tanki

(e)Samaki wagonjwa watengwe kwenye tank lingine (hospital tank)

(F)Nyavu zilizotumika kutolea samaki wagonjwa ziwekwe dawa (disinfection) zikaushwe juani na zioshwe vizuri hii ni pamoja na tank na vitu vyake

(g)hakikisha tank halina kitu chochote cha chuma (metal) na maji ya hospital tank yasiingie kwenye tank kuu

4 comments:

  1. Ni faraja saana kuona mtu anafanya kile ajuacho, awezacho na apendacho. Hii husaidia kuleta uelimishaji sahihi kwa kuwa kitendekacho si bahatishi na ikitokea kukawa na maswali basi hujibiwa kiufasaha zaidi. Kwa sasa wapo wanaoangalia saana idadi ya watembeleaji na pia reactions zao, lakini pia twatambua kuwa jamii yetu (kwa bahati mbaya) imekuwa ikipendelea mambo yasiyofikirisha na yenye urahisi wa kutenda na kuamua na ndio maana kwenye uelimishaji halisi hakuonekani kuwa na wafuasi. Lakini muda waja na wenye kuhitaji wataendelea kupata yale mema yatokanayo na blogs njema kama hii.
    Kazi nzuri na japo sikukufahamu mpaka nilipokuona kwenye maoni kwa Mkongwe Mjengwa, nimefurahi kutembelea "jamvini" mwako.
    Blessings

    ReplyDelete
  2. Nilifurahi nilipoigundua blogu hii, wiki kadhaa zilizopita. Inatoa elimu muhimu sana. Kuielewa mimea, miti, na mazingira kwa ujumla, na kufahamu namna ya kuitunza na kuiboresha, ni elimu ambayo tunaihitaji sana, hasa wakati huu ambapo uharibifu wa mazingira umekithiri.

    ReplyDelete
  3. Nashukuru wadau kwa mchango wenu, na mimi naahidi kuendelea kuwapatiaq kile kidogo nilichonacho kichwani mwangu. Mungu awabariki

    ReplyDelete
  4. Nimependa ushauri kuhusu ufugaji wa samaki.lakini naomba kuuliza samaki wakiwa na vidonda nje miili yao inakuwa inasababishwa na nni?naombeni msaada wangu

    ReplyDelete