KURASA

Monday, December 22, 2008

MILONGE (moringa oleifera)



Hii ni miti ambayo haiwi mikubwa sana, inakuwa na maua meupe na kisha hutoa mbegu ndogo zinazokuwa kwenye magamba marefu kama kisu. miti hii hustawi zaidi ukanda wa pwani wenye mvua kiasi na joto, hustawi zaidi kwenye udongo usiotuamisha maji na inaweza kustawi kwenye udongo usio na rutuba nyingi na inahimili ukame kwa kiasi kikubwa.

MATUMIZI
Majani yake huweza kupikwa kama mboga na kuliwa, pia yanaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu bila ya kuathiri ubora wake wa virutubisho (nutritional value) majani yake yanavirutubisho vingi kuliko vyakula vingi tulivyozoea mfano


Ina vitamin A nyingi zaidi ya karoti
Ina Calcium nyingi zaidi ya Maziwa
Ina madini ya chuma zaidi ya spinach
Ina vitamin C nyingi zaidi ya Machungwa
Ina madini na pottasium zaidi ya Ndizi
ina protein nyingi zaidi ya nyama na mayai



MATUMIZI MENGINE
Maganda ya mbegu zake yanaweza kutumika kutibu maji(water treatment)unachukua maji yako ambayo unahisi si salama, unachanganya na maganda ya mbegu zilizopondwa pondwa kiasi, unayaacha kwa muda yatuame kisha unayachuja na yanakuwa salama kwa matumizi


Mbegu za milonge zinaweza kutumika kama dawa ya kupunguza sukari mwilini kwa wagonjwa wa kisukari, unachukua mbegu mbili au tatu unazipasua na kuchukua kokwa ya ndani na kutafuna mara 3 kwa siku, matumizi yanaweza kuongezeka au kuzidi kutegemeana na hali ya mgonjwa

Picha hapo chini inaonyesha mbegu za mlonge juu na kulia kwake ni baada ya kupasuliwa na kupata kokwa ya ndani (ambayo ni dawa ya kupunguza sukari mwilini), funguo imewekwa ili kujua ukubwa halisi wa mbegu


Sehemu yoyote ya mmea kama majani, magamba, mizizi, au maua yakipondwa pondwa na kupakwa kwenye sehemu yenye uvimbe ni dawa tosha ya kupunguza hali hiyo, pia dawa hii inauwezo mkubwa wa kupunguza sumu kama umeng'atwa na wadudu kama nyuki, manyigu/dondola, siafu, tandu, nge nk

Mbegu zake zinatoa mafuta (40%) yanayojulikana kama BEN OIL, ambayo hutumika kulainishia mitambo maalum kama saa za ukutani, pia mafuta haya ni dawa ya upele na harara

6 comments:

  1. Asante Kaka. Elimisha maana wapoeao ni wengi kuliko wasemao. Blessings

    ReplyDelete
  2. We mdau inaonekana una mambo mengi sana ya kuelimisha jamii hasa kuhusu vitu vya asili asili. Mimi huwa nasumbuliwa sana na malari kila baada ya miezi mitatu mpaka minne, je unaweza kunisaidia dawa gani ya asili nitumie au kama kuna mtu anajua aniambie

    ReplyDelete
  3. Blog yako nzuri inaelimisha, Good for you!

    ReplyDelete
  4. Kitas enterpprises LtdApril 28, 2009 at 2:53 PM

    Good information on Moringa

    Am aslo dealing with Moringa products and am selling locally and exporting abroad..from Moringa oil, soap, skin andmassage lotion, hair fertilizers and Moringa leaf powder

    Any one can contact me lawcheyo@gmail.com

    ReplyDelete
  5. Kilimo chake kikoje kibiashara? Mbegu zake zinapatikana vp? Miche mingapi Kwa heka/hekta?

    ReplyDelete
  6. Kilimo chake kikoje kibiashara? Mbegu zake zinapatikana vp? Miche mingapi Kwa heka/hekta?

    ReplyDelete