Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
KURASA
▼
Friday, April 24, 2009
TANGO-Dawa ya kukausha maziwa mbwa anayenyonyesha
Hii le nitaongelea tunda la tango na madhumuni zaidi ni katika kumsaidia mbwa jike kukausha maziwa. Inaweza kutokea mbwa watoto wake wamekua na kuacha kunyonya au watoto wakafariki wakati bado wadogo mara baada ya kuzaliwa, na maziwa yake yasikauke yenyewe ingawa ni mara chache sana.
Maziwa yasipokauka yatamsababishia ugonjwa wa chuchu ujulikanao kama (mastitis)ambao husababisha maziwa kuvimba baada ya kushambuliwa na bakteria, tiba yake huwa ghari kiasi sana na mara chache husababisha vifo kwa mbwa.
Sasa basi kwa njia rahisi ukitaka kuepukana na hali hii inatakubidi kumsaidia mbwa wako kukausha maziwa, katika chakula chake msagie tango moja (1)ambalo limeondolewa maganda nusu na nusu kubakia kwa muda wa siku 3 mpaka 5 au mpaka maziwa yakauke.
BINADAMU
Kwa binadamu tango ni dawa la magonjwa mengi na kinga pia, inashauriwe liliwe likiwa na maganda yake kiasi yaani usimenye maganda yote. magonjwa yanayotibiwa na tango ni KUHARISHA magonjwa mengine ni kama presha ya kupanda na kushuka pia husaidia kurekebisha ngozi ya mwili
Asante sana kwa habari hii. Huwa nakula sana matango. Ila sikujua kama ni dawa ya kuzuia kuhara basi ntajaribu nikipata homa hii. Pia nachukua nafasi hii na kusema karibu sana ktk kibaraza changu naona umeingia kama mfuatiliaji.
ReplyDeleteNaendelea na utafiti wangu baada ya muda naona nitakuwa na uwezo wa kuandaa kitabu hata kama ni kidogo, nashukuru kwa kunikaribisha ingawa nilisha karibia mwenyewe
ReplyDeleteNakutakia maandalizi mema na najua kitakuwa kitabu kizuri sana.
ReplyDeleteHii ya kukukaribisha najua ulisha karibia.Ok
nimekufikia,nimekukaribia kumbe upo karibu tu hapa. habari yako mkuu.
ReplyDeletekaribu sana nyasa kwetu
markus karibu sana mkuu, huko nyasa huwa ninapita pita kila siku, lakini pia nina mpango wa kupanda basi nije kabisa ikiwezeka tuonane na nipate kujifunza mengi
ReplyDeleteAksante
Kaka, nimekukubali katika nyanja hii!Ni wachache sana wenye uwezo ulionao na kuwa katika nafasi ya kuwashibisha wengine!Endelea kutupa vitu adimu kaka!Hongera sana!
ReplyDelete