KURASA

Wednesday, September 16, 2009

HOLSTEIN FRIESIAN - kinara wa utoaji maziwa duniani



ASILI YAKE

Uholanzi katika jimbo la friesland

UZALISHAJI KWA MWAKA
10,158 kg za maziwa
3.64% mafuta
3.05% protini

RANGI
nyeupe na nyeusi, mkia huwa na rangi nyeupe na kwenye paji la uso huwa na rangi nyeupe yenye umbo kama la pembe tatu ,mara chache (1/1000) huzaliwa ndama mwenye rangi nyekundu na nyeupe

UZITO
kilo 1200 majike
kilo 1400 madume



Huyu ndiye aina ya ng'ombe anayeshikilia rekodi ya uzalishaji maziwa kwa kiwango cha juu, maziwa yake hayana mafuta mengi. Nimeshuhudia akitoa maziwa zaidi ya lita 70 kwa siku kwa mikamuo mitatu lita 30 / 20 / 25 Madume yanatumika kwa kulimia na kukokota mikokoteni, Ni mkubwa kushinda nyati ambaye ana uzito wa kilo 800-1000, kama wanavyoonekana kwenye picha urefu wao ni sawa na kimo cha mtu mwenye urefu wa wastani. Kwa Tanzania wanapatikana zaidi Kitulo mkoani Iringa na Uyole (kituo cha utafiti wa kilimo) Mkoani Mbeya, aina hii ya ng'ombe hustawi zaidi katika mazingira yenye baridi kali.

Kama unataka mbegu hii wasiliana na maafisa ugani wa mifugo ili waje kupandisha ng'ombe wako kwa njia ya chupa, mbegu zinazotumika kwa njia hii hutoka kwa madume PURE BREED CLASS A na matokeo yake ni kupata ndama bora

14 comments:

  1. Itabidi niende Uyole ila ni kweli bei yake ikoje. Asante tena kwa uhabarishaji huu.

    ReplyDelete
  2. Ngoja niwasiliane na wadau walioko Mbeya niweze kupata bei zao, ingawa jamaa wanauza zaidi madume na kubakisha majike kwa ajili ya mbegu kwa sababu Ngombe sio wengi sana

    ReplyDelete
  3. Shukran ila tunasubiri kupata bei zake, ikiwezekana pamoja na usafiri kwenda mkoa mwingine

    ReplyDelete
  4. Uyole hawauzi, Kitulo wanauza Tsh 1,000,000 kwa DSm wanapatikana kwa Tsh 600,000 Tanga kituo cha utafiti 550,000 na pia kuna Mama anaitwa Ruth (Tanga)anauza 700,000. . Hawa wote ni ng'ombe wenye mimba

    KIASI CHA UZALISHAJI (wastani)
    kitulo - 50 litres
    Ruth - 30 litres
    Tanga utafiti - 17-20 litres
    Dsm 10-15 litres

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba namba zako kaka nahitaji toka kitulo

      Delete
  5. Jamani hao ng`ombe bado wanapatikana? Nijuze tafadhali - Mfugaji mdogo

    Gratian Kasenene
    0715009952

    ReplyDelete
  6. Mkubwa Benet nisaidie kupata ng`ombe bora nimfugaji wa kawaida kwa miaka 10 sasa ila nataka kuboresha mifugo iwe ya kisasa- pia nimesikia pale UDSM Engineering wanatengeneza mtambo rahisi wa kuchanganyia chakula cha ng`mbe je? nikweli

    ReplyDelete
  7. na mm nahitaji hiyo aina ya ngombe.nipo dar lakini nataka kumsafirisha kwenda songea.naomba mnijuze kama bado wanapatikana

    ReplyDelete
  8. na mm nahitaji hiyo aina ya ngombe.nipo dar lakini nataka kumsafirisha kwenda songea.naomba mnijuze kama bado wanapatikana

    ReplyDelete
  9. Natafuta ng'ombe wa maziwa wazuri wapi naweza kuwapata no 0718013034

    ReplyDelete
  10. NAOMBA MAWACLIANO KITULO HAO WATU TUNATAKA KUFUGA

    ReplyDelete