KURASA

Saturday, September 12, 2009

MAZIWA - Jinsi ya kufahamu kama yameongezewa maji

Ubora wa maziwa hupimwa kwa njia nyingi, kwa mfano harufu ilikugundua kama ng’ombe alitumia dawa yoyote, pia kwa kuangalia unaweza kujua kama maziwa hayana rangi ya kawaida, na kwa vipimo maalum zikiwemo kemikali ili kujua kama maziwa yana ubora usio faa (maziwa hayapimwi kwa kuonja)



Mara kadhaa wafugaji wamekuwa wakiongeza maji kwenye maziwa ili kuweza kujipatia kipato zaidi na hii huwa ni hasara kwa mlaji. Kwa kawaida kuna kipimo kinachojulikana kama LACTOMETER, hiki ni kipimo ambacho kinaweza kutambua kama maziwa yameongezwa maji. Lactometer hutumiwa kwa kuweka maziwa kwenye chombo maalum cha maabara kama test tube na beaker , koroga ili kuyeyusha mafuta ya kwenye maziwa na kisha lactometer hutumbukizwa kwenye maziwa, maziwa mazuri lactometer itasoma kati ya 1.026 – 1.036 tofauti na hapo maziwa yatakuwa yameongezwa maji au kitu kingine, kwa kawaida kwenye maziwa huwa kuna protini, mafuta, maji , chumvi chumvi na sukari (lactose)

Kifaa hiki kinaweza kudanganywa kwa kuongeza sukari, ngano au maziwa ya kopo na kikasoma kwamba maziwa hayajatiwa maji, kwa sababu jinsi lactometer inavyoelea zaidi ndivyo maziwa yanaonekana bora zaidi (hayaongezewa maji)
Kama huna kipimo cha lactometer wala usiwe na wasiwasi wa kuyapima maziwa maana kuna njia za kienyeji ambazo zitakupa matokeo mazuri tu kama au zaidi ya lactometer

NJIA YA KWANZA


Chukua kibiriti toa njiti moja na uichovye kwenye maziwa (haraka) na kisha kuiwasha haraka haraka, kama maziwa hayajaongezwa maji njiti itawaka kama kawaida na kama kuna maji njiti haitawaka au itawaka kidogo na kuzimika hapo hapo kutegemeana na kiasi cha maji yaliyongezwa.


NJIA YA PILI



Mwaga tole la maziwa kwenye mkono wako kasha liache lile tone litirike na kumwagika chini, ukiangalia mule yalikotiririka maziwa utoana yameacha njia yenye rangi nyeupe, hii ni kwa maziwa halisi, na maziwa yaliyoongezwa maji yataacha njia nyeupe ambayo imepauka. Njia hii inahitaji uzoefu kidogo na unaweza kujizoesha kwa kununua maziwa ukayagawanya sehemu mbili na kisha sehem u moja kuyachanganya kiasi na maji, halafu mimina maziwa kutoka sehemu zote mbili na uangalie tofauti yake



TAHADHARI

Kwa wale wanaofuga ng'ombe aina ya Friesian (pure breed) wakati wa mvua nyingi kama ngombe wako utamlisha majani machanga tu bila ya majani makavu na pumba zenye virutubisho, basi maziwa atakayotoa yakipimwa kwa kutumia vipimo hivi yataonekana kama yameongezwa maji, ingawa ki ukweli ni kwamba hayaongezwa kitu chochote

7 comments:

  1. Mkuu hapo nimekufuatilia kwa makini sana. taabu ni pale kama ng'ombe ndo huyo, ambaye akilishwa majani machanga maziwa yakuwa maji nitashindwa kujua kama nimeliwa au nimeula.
    Somo hili ni kiboko.

    ReplyDelete
  2. Dada Yasinta nashukuru sana kwa kunitembele humu
    Chib huyu ngombe niliye mtaja (Friesian) ni wachache sana utakuta ni pure breed kwa hata nchini kwetu Tanzania wanapatikana Kwenye shamba la Kitulo na kituo cha utafiti cha Uyole Mkoani Mbeya. Ngombe huyu huwa na uwezo wa kutoa zaidi ya Lita 70 kwa siku kwa mikamuo mitatu na wengine hufikia hadi lita 100 na zaidi

    ReplyDelete
  3. Mkuu naomba kufahamu bei ya kimea (culture) kwajili ya kugandisha maziwa na mahali zinapopatikana

    ReplyDelete