KURASA

Friday, September 25, 2009

UFUGAJI WA NGURUWE - SEHEMU YA PILI

Sehemu ya pili ya maelezo kuhusu ufugaji wa nguruwe tuaangalia nguruwe dume ambaye ndiye atakuwa natumika kwa ajili ya kupandishia majike kwenye mradi wa nguruwe, wengine huwa wanatumia madume ya kukodi, lakini kama utakuwa na majike zaidi ya 10 utahitaji kuwa na dume kwenye mradi wako,

UCHAGUZI WA DUME
Dume litoke kwenye kizazi ambacho hakina historia ya magonjwa na wana historia ya kuzaa watoto wengi ,wenye afya bora, na ukuaji mzuri, angalia kizazi/ukoo wake uwe na chuchu nyingi zisizopungua 14 zikiwa 18 ni nzuri zaidi

BANDA LA DUME
Liwe na ukubwa usiopungua 3 m * 2.5m geti liwe lachuma na linafunguka kuelekea kwa ndani na nje pande zote mbili, siku zote majike ya pelekwe kwa dume na si kinyume chake.

CHAKULA
Dume alishwe kilo 2 – 3 za mlo kamili wenye kiasi cha wastani cha protini, epuka kumlisha mashudu mengi kwa sababu yana kuwa na kemikali inayojulikana kama omega 3 fatty acids ambayo hupunguza kiasi cha manii kwa nguruwe, tumia mimea kama lukina na desmodiam au dagaa kama chanzo cha protini

UPANDISHAJI
dume aina ya saddle back akimpanda jike aina ya landrace


Madume huanza kupanda yakifikisha umri wa miezi 12 – 14 hupanda jike moja mara 2 kwa siku na hupanda majike 6 kwa kila siku 8 na majike yasifululize kwa zaidi ya siku mbili zinazofuatana, majike yapelekwe asubuhi mapema kabla ya dume kula chakula
Dume linaweza kuendelea kutumika kwa upandishaji mpaka likifikisha miaka 3 – 4 ndipo unaweza kuanza kutumia dume lingine, uzoefu unaonyesha nguruwe chotara huwa na uwezo wa kupanda mara nyingi na kwa muda mrefu zaidi. Dume moja huweza kuhudumia majike 20 lakini kwa matokeo mazuri tumia dume moja kwa kila majike 15 – 18

8 comments:

  1. Umenikumbusha mbali mpaka Peramiho kule kuna nguruwe wengi wa ufugaji bora

    ReplyDelete
  2. asante mkuu. ninaprint sasa hivi. naona wengine wameanza kuosha vinywa, ntakuwa nakusumbua kwa maswali mengine

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kila mtu ana itikadi yake na mapenzi yake, lakini kwangu mimi wanyama wote ni sawa kwani hata kwenye ilani ya KILIMO KWANZA inayosimamiwa na Raisi Nguruwe pia wapo

    ReplyDelete
  4. Nimependa sana hii blog yako. Sikuwahi kufikiri kuwa naweza pata blog ya kiswahili inayotoa mafunzo ya jinsi ya kufuga nguruwe. Hongera sana, unafanya kazi nzuri

    ReplyDelete
  5. Asante sana. Hivi kwa nguruwe wadogo wanatakiwa kuachishwa kunyonya wakiwa na umri gani?

    ReplyDelete
  6. Nguruwe wadogo huachishwa kunyonya wakiwa na umri wa miezi miwili hivi( siku hasini na sita 56 )

    ReplyDelete
  7. MR ELIMU YAKO NIME IKUBALI NAHITAJI KUJUA KUHUSU AINA ZA VYAKULA VYA NGURUWE.

    ReplyDelete
  8. Naomba kuuliza hivi sababu zinazopelekea watoto wa nguruwe kufia tumboni kwa mama yao ni mini? Maana nguruwe wangu kazaa watoto kumi wawili wazima nane wametoka wamekufa tayari tumboni kwa mamayao.naomba msaada je tatizo ni mini?

    ReplyDelete