KURASA

Friday, September 25, 2009

UFUGAJI WA NGURUWE - SEHEMU YA KWANZA

Kutokana na maombi ya Bw John Mwaipopo kuhusu ufugaji wa Nguruwe na kuku, leo nimeamua kuanza kumuelezea njia bora na sahihi

AINA ZA NGURUWE (baadhi)
LARGE WHITE


-Hii ndiyo aina kubwa zaidi ya nguruwe wa kufugwa nyumbani
-Kama jina lake lilivyo ana rangi nyeupe mwili mzima
-masikio yake yamesimama wima
-Ana sura iliyobonyea kwa ndani (dish faced)

LANDRACE


-Weupe mwili mzima
-masikio yamelala kabisa
-Wana ukubwa wa wastani

SADDLEBACK


-Ni wakubwa
-Wana rangi nyeusi na mstari mweupe kuzunguka shingo na miguu ya mblele
-Masikio yamelala kiasi


DUROC

Asili yao inatoka tangu mwaka 1812 katika majimbo ya New York na New Jersey ambako ndio walizalishwa kwa mara ya kwanza ingawa pia kuna tetesi kwamba waliletwa toka Uingereza

Wana rangi ya kahawia iliyooza mpaka iliyopauka na kutaka kuwa kama njano, wana masikio yaliyolala kwa mbele na sura ndefu ilyonyooka, wana nyama tamu sana na isiyo na mafuta mengi, ni Mbegu inayotumika Zaidi kwenye kuchanganya na Mbegu nyingine ili kupata uzao wenye nyama tamu na yenye mafuta kidogo, Madume ndio hutumika kwenye kupanda majike ya Mbegu nyingine kama Large White na Lamd race sababu ni kwamba majike ya Duroc hayazai watoto wengi

CAMBOROUGH

Hii ni Mbegu mpya ambayo inatokana na Mbegu za Large white na Land race ambao walichanganywa kitaalam  ili kupata sifa za uzazi wa watoto wengi, ukuaji wa haraka, kutumia chakula vizuri, uzalishaji maziwa wengi kwa ajili ya watoto, sifa ya kipekee ni uwezo wa majike kuendelea kuzaa kwa miaka mingi zaidi ukilinganisha na wengine.


Wana rangi nyeupe tupu, masikio yamelala kidogo kwa mbele na wana uso mrefu ulioonyooka, wana uzazi wa wastani watoto 14 na majike huanza kupandwa wakiwa na miezi 8 tu

13 comments:

  1. Ndugu umekosa mada ya kutuwekea ila hawa wanyama wachafu, nani anataka kufuga kama hawa elezea kuhusu kufuga ngombe na mbuzi, umechafua blog yako.

    ReplyDelete
  2. hii ndio yenyewe. viumbe hawa watamu balaa. tunaomba idadi ya wasiokula iongezeke ili tufaidi wachache. aliyelala usimwamshe.

    ReplyDelete
  3. Samahani Anony wa kwanza kama nimekukera nilichofanya mimi ni kukidhi matakwa ya wasomaji wangu, kama na wewe unahitaji kufahamu kitu basi usisite kuwasiliana nami
    Natanguliza shukurani zangu

    ReplyDelete
  4. Tunaomba Elimu Mheshimiwa, Huyu Jamaa anayeona kuwa unachafua blog,yeye inamkera nini? ajue tu ametawaliwa na imani aliyoletewa na Waarabu ambao waliwatesa ndugu zetu waliwafanyia mambo mabaya dada zetu na wanaume wengine.Namwomba aelewe mtazamo wake asiradhimishe wengine.Tunaomba Elimu Ndugu.

    ReplyDelete
  5. huyu wa kwanza anajua watuwote tuko kama yeye!!! we kijana hacha sisi tunaopiga hii kitu tuache tupate elim, we kaa na ushamba wako!!!!!!! na namshkru sana hall, aliposema na wengine wapungue ili tupate nyama nyingi ebu cheki sasa hivi kilo 7000, nyama gani hapa nchini inauzwa hivyo,lete kimooooooooooootoooooo

    ReplyDelete
  6. Huyu jamaa analeta udini kwenye kutafuta pesa. Hayo ni mawazo finyu sana ndo maana Wa Tz wengi tunakuwa maskini kwaajili ya kuzingatia hizi kasumba chafu tulizoletewa na wakoloni wa Kiarabu.

    ReplyDelete
  7. Kaka kwanza hongera kwa uliyoyafany. Mi ni mwanaharakati mwenzio kwenye kilimo na ufugaji. Nimejiajiri toka nilipo maliza chuo cha kilimo SUA. Beliv me Nakupongeza kwan najua umuhimu wa unacho fanya. Tumaini Mtei wa Dodoma(aka Mkulima)

    ReplyDelete
  8. Hongera kwa hi blog yako. Ningetaka kuongeza jambo kuhusu nguruwe.Nikianzia na Large white ningetaka kusema nguruwe jike yaani mama amedhibitishwa kuwa ni mtunzi bora ukilinganisha na Landrace ambaye hajali sana watoto wake ingwawa anazaa watoto wengi hadi kumi na wanee.Kwa hivyo ningewashauri wakulima wafanye 'cross' ya hawa aina ya nguruwe.

    ReplyDelete
  9. Huyu Jamaa anajifanya analeta udini wakati hijui dini. Namshauri aende Misri akajifunze dini halafu ataelimishwa kwa nini Misri ni nchi ya Kiislsmu lakini ni kati ya nchi duniani zinazoongoza kufuga nguruwe.

    ReplyDelete
  10. kwenye kutafuta pesa hakuna dini jaman kama hautaki pitakuleee kaka mbona kuna vitu vingi tuuu .......

    ReplyDelete
  11. Big up mkuu mwenyewe nimepata Eneo la kulima naomba mawasiliano yako mkuu

    ReplyDelete
  12. Mkuu nimeipenda sana hii elimu kama kuna mafundsho huwa yanatolewa basi naomba uniunge namm kwan natamani sana niwe mfugaji bora.

    ReplyDelete