KURASA

Monday, November 2, 2009

BORAN - MBEGU BORA YA NG'OMBE WENYE ASILI YA AFRIKA MASHARIKI

Asili yake ni maeneo ya borana kusini mwa Ethiopia ambako alipatikana baada ya mbegu tatu za ng’ombe zilichanganyika kwa bahati mbaya kutoka kwa wafugaji wa kienyeji waliotoa ngombe wao kutoka pande tofauti za afrika, hiyo ilikuwa zaidi ya miaka 1300 iliyopita lakini sasa hivi kuna taasisi inayoitwa Boran cattle breeder’s society iliyopo nchini Kenya.

DUME BORA LA BORAN


Taasisi hii iliamua sasa itafute mbegu bora ya Boran kwa kutumia njia za kitaalam tofauti na hapo mwanzo ambako Boran alitokea tu bila hata wafugaji kujua kwamba wanatengeneza mbegu bora ya ng’ombe.

JIKE BORA LA BORAN


Waalamu wa kupandisha (breeders) waliamua kuangalia vinasaba bora zaidi na kumfanya Boran awe wa kisasa zaidi na kuweza kuhimili hali ya Afrika mashariki huku uzalishaji wa maziwa na nyama ukiongezeka zaidi kuliko ule wa ng’ombe wetu wa kienyeji, Boran wa kisasa ana damu za aina tatu katika uwiano ufuatao N’gombe wa ulaya wasio na nundu (european bos taurus) 24% Ng’ombe wa Afrika mashariki wenye nundu wajulikanao kama Zebu (bos indicus)64% na ngombe wafrika wasio na nundu (african bos taurus ) 12%



SIFA
-Ni mkubwa kuliko ng’ombe wa kienyeji
-Ana kiwele cha wastani na chuchu ni kubwa kidogo
-Anazaa ndama wa wastani (kilo 25 – 28) kwa hiyo hakuna matatizo wakati wa kujifungua lakini watoto hukua haraka na ni mara chache sana ndama kufariki
-Anahimili hali ya mazingira ya Afrika kuliko ng’ombe wa kisasa (joto na magonjwa)
-Ngombe jike anaweza kuzaa bila matatizo mpaka akiwa na miaka 15, madume yanauwezo wa kuzalisha mpaka miaka 16
-Majike hubalehe baada ya siku 385 (mwaka na siku chache)
-Ni wapole na wenye nguvu kwa hiyo hufaa kwa shughuli za kulima na kukokota mikokoteni (maksai)
-Anaongezeka uzito haraka hata kama anakula majani makavu, majike yanayo nyonyesha hupungua uzito kidogo sana kipindi cha kunyonyesha
-Wanakula kwa mshikamano na hawatawanyiki wakiwa machungoni kiasi kwamba inakuwa vigumu kumuiba mmoja au kumtenganisha na wenzake

BORAN WAKICHUNGWA KATIKA KUNDI LENYE MSHIKAMANO



Wafugaji wengine wamejaribu kuchanganya mbegu hii na mbegu nyingine za kisasa kutoka bara la ulaya ili kuongeza uzalishaji wa maziwa au nyama kama wanavyoonekana hapo chini kwenye picha

BORAN NA FRIESIAN (maziwa)


BORAN NA BEEFMASTER (nyama)



BORAN NA JERSEY (maziwa)


BORAN NA DRANKENSBERGER (nyama na maziwa)

10 comments:

  1. Sikujua kama Afrika kuna ngómbe wasio na nundu. Kaka Bennet ulipotea kidogo twafurahi kwa kurudi tena.

    ReplyDelete
  2. Hivi serekali yetu inatambua kwamba kuna watu kama nyinyi na inashindwa kuwatumia? nchi hii haitakiwi kuwa na njaa hata kidogo

    ReplyDelete
  3. Dada Yasinta hao ng'ombe wapo ila ki ukweli asili yao ni bara ulaya ila waliletwa miaka mingi na wakabadilika kidogo ili kulingana na mazingira yetu ya Afrika
    Anony serekali yetu inawataalamu wengi tu tena zaidi yangu wapo kwenye taasisi za utafiti, wizarani na hata kwenye wilaya, tatizo ni namna ya kutekeleza hiki KILIMO KWANZA maana kinahitaji mtaji kiasi na kujitolea

    ReplyDelete
  4. Nilikuwa najaribu kupitia mitandao nione elimu na namna ya kuwapata ng'ombe aina ya Borana wa kenya kwa hapa Tanzania. ndipo nikakutana na elimu hii nzuri. hongera sana kwa elimu hii. Ombi langu ni kuweza kuwapata hawa ng'ombe. Sijui nitawapata wapi ndugu kwa hapa Tanzania?

    ReplyDelete
  5. ng'ombe aina ya boran wanapatikana wapi

    ReplyDelete
  6. Naitaji kujua wapi ntapata mbegu bora ya ngombe wa maziwa mwenye kutoa maziwa mengi

    ReplyDelete
  7. Nawezaje kupata mbegu ya boran

    ReplyDelete
  8. Bennet Asante sana Kwa ufafanuzi uliotupa but Kwa mm ambaye naishi Mwanza naweza wapata wapi hawa Boran

    ReplyDelete
  9. Hizi borani naweza kuwapata wapi jamani? Mimi nipo kata ya Kapele - wilaya ya Momba - mkoa wa SONGWE.

    ReplyDelete