Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
KURASA
▼
Thursday, November 12, 2009
KASUKU - DONDOO ZA KUMFUNDISHA KUONGEA
Watu wengi wamekuwa wakipenda kufuga kasuku lakini utakuta wanalalamika kwamba kasuku wake haongei, nimeamua kuweka vidokezo muhimu ili mfugaji aweze kuzingatia wakati wa kumfundisha
Kuna aina nyingi za kasuku duniani wengine wakiwa na rangi za kawaida na wengine wakivutia sana, kwa kawaida huwa hawaishi sehemu zenye baridi kali kwani hupendelea hali ya joto wastani
UCHAGUZI WA KASUKU
Mbegu kubwa ni waongeaji wazuri, mbegu ndogo ni wavivu kujifunza,
Akiwa mdogo anajifunza vizuri zaidi, ukiweza mpate yule anayetoka kulelewa kwenye kiota na ndio anajifunza kuruka/kupaa
Kasuku muoga hawezi kujifunza vizuri.
Kasuku mwenye tabia ya kung'ata anauwezo mkubwa wa kujifunza kungea.
MAZINGIRA
Kumbuka kasuku hujifunza maneno machache tu hawezi kuongea kama mtu.
Sehemu nzuri ya kumuweka nyumbani ni jikoni, kwa sababu kuna shughuli nyingi.
Huanza kuongea katika umri wa miezi 4-6.
UFUNDISHAJI
Wakati wa kumfundisha zima radio na TV (kusiwe na kelele)
Muda mzuri wa mafunzo ni asubuhi na jioni.
Mfundishe kupiga miluzi baada ya kuweza kuongea baadhi ya maneno na si kabla ya hapo.
Kumbuka kasuku hujifunza vizuri zaidi kwa vitendo mfano unamtoa nje ya kibanda chake huku unamwambia " toka nje mmmh" ukirudia rudia, jitahidi kutumia Mmmh kila baada ya neno, hii humsaidia kujifunza kwa urahisi.
Hakikisha anapata mlo kamili maji na matibabu
Ahsante kwa habari hii ila nikiwa na kasuku huyu basi tutakuwa akina kasuku waengi:-)
ReplyDeletekwani na wewe yasinta ngonyani ni kasuku? au sijakuelewa? LOL
ReplyDeleteKumfundisha mtu tu ni kazi, sasa ije iwe kasuku.....
ReplyDeleteInaonekana kweli Dada Yasinta ni kasuku kama alivyosema mwenyewe, sasa kwake yeye itakuwa kazi kumfundisha maana inatakiwa uwe unatamka maneno taratibu kiasi.
ReplyDeleteChib ukiamua inakuwa rahisi mbona we jaribu utaona
Asante kwa hii!
ReplyDeleteNilikuwa najiuliza hili kwa kuwa rafiki yangu kumfunza kasuku ilimshinda na sikujua hata ni kwanini.Alim-adapti sehemu na nimepata mwangaza ni kwanini kasuku kikongwe anaweza kukununia.
Kuna hadithi moja inayosema Mama mmoja wa alikwenda kununua kasuku akamkuta anayejua kuongea tayari, lakini muuzaji akamuonya kwamba kasuku huyo alikuwa anafugwa na machangudoa fulani
ReplyDeleteBasi yule Mama akang'angania kumnunua sababu alikuwa anaweza kuongea, basi alivyofika naye nyumbani kasuku akawa anasema sema kwa kurudia NYUMBA MPYA na MAMA MPYA,
watoto walivyorudi shule akawa anasema NYUMBA MPYA, MAMA MPYA na WATOTO WAPYA mama akaendelea kufurahia, wakati wote huo mumuwe alikuwa safarini, siku aliporudi Mama akiwa na watoto nyumbani baadas ya kupokea zawadi za safari
akaamua na yeye akamwonyeshe mumuwe kasuku, basi kufika kule kasuku alipomuona tu mumewe akasema AAAHH BWANA JUMA
Ina maana jamaa alikuwa anaenda sana kwenye ile nyumba ya machangudoa mpaka kasuku kamzoea na kumjua jina lake
Ninae Napa wa kijivu mkia una Rangi nyekundu ana mwezi mmoja tokea hatoke porini lakini ajaanza Kuo
ReplyDelete