Sehemu ya pili ya maelezo kuhusu ufugaji wa nguruwe tuaangalia nguruwe dume ambaye ndiye atakuwa natumika kwa ajili ya kupandishia majike kwenye mradi wa nguruwe, wengine huwa wanatumia madume ya kukodi, lakini kama utakuwa na majike zaidi ya 10 utahitaji kuwa na dume kwenye mradi wako,
UCHAGUZI WA DUME
Dume litoke kwenye kizazi ambacho hakina historia ya magonjwa na wana historia ya kuzaa watoto wengi ,wenye afya bora, na ukuaji mzuri, angalia kizazi/ukoo wake uwe na chuchu nyingi zisizopungua 14 zikiwa 18 ni nzuri zaidi
BANDA LA DUME
Liwe na ukubwa usiopungua 3 m * 2.5m geti liwe lachuma na linafunguka kuelekea kwa ndani na nje pande zote mbili, siku zote majike ya pelekwe kwa dume na si kinyume chake.
CHAKULA
Dume alishwe kilo 2 – 3 za mlo kamili wenye kiasi cha wastani cha protini, epuka kumlisha mashudu mengi kwa sababu yana kuwa na kemikali inayojulikana kama omega 3 fatty acids ambayo hupunguza kiasi cha manii kwa nguruwe, tumia mimea kama lukina na desmodiam au dagaa kama chanzo cha protini
UPANDISHAJI
dume aina ya saddle back akimpanda jike aina ya landrace
Madume huanza kupanda yakifikisha umri wa miezi 12 – 14 hupanda jike moja mara 2 kwa siku na hupanda majike 6 kwa kila siku 8 na majike yasifululize kwa zaidi ya siku mbili zinazofuatana, majike yapelekwe asubuhi mapema kabla ya dume kula chakula
Dume linaweza kuendelea kutumika kwa upandishaji mpaka likifikisha miaka 3 – 4 ndipo unaweza kuanza kutumia dume lingine, uzoefu unaonyesha nguruwe chotara huwa na uwezo wa kupanda mara nyingi na kwa muda mrefu zaidi. Dume moja huweza kuhudumia majike 20 lakini kwa matokeo mazuri tumia dume moja kwa kila majike 15 – 18
Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
KURASA
▼
Friday, September 25, 2009
UFUGAJI WA NGURUWE - SEHEMU YA KWANZA
Kutokana na maombi ya Bw John Mwaipopo kuhusu ufugaji wa Nguruwe na kuku, leo nimeamua kuanza kumuelezea njia bora na sahihi
AINA ZA NGURUWE (baadhi)
LARGE WHITE
-Hii ndiyo aina kubwa zaidi ya nguruwe wa kufugwa nyumbani
-Kama jina lake lilivyo ana rangi nyeupe mwili mzima
-masikio yake yamesimama wima
-Ana sura iliyobonyea kwa ndani (dish faced)
LANDRACE
-Weupe mwili mzima
-masikio yamelala kabisa
-Wana ukubwa wa wastani
SADDLEBACK
-Ni wakubwa
-Wana rangi nyeusi na mstari mweupe kuzunguka shingo na miguu ya mblele
-Masikio yamelala kiasi
AINA ZA NGURUWE (baadhi)
LARGE WHITE
-Hii ndiyo aina kubwa zaidi ya nguruwe wa kufugwa nyumbani
-Kama jina lake lilivyo ana rangi nyeupe mwili mzima
-masikio yake yamesimama wima
-Ana sura iliyobonyea kwa ndani (dish faced)
LANDRACE
-Weupe mwili mzima
-masikio yamelala kabisa
-Wana ukubwa wa wastani
SADDLEBACK
-Ni wakubwa
-Wana rangi nyeusi na mstari mweupe kuzunguka shingo na miguu ya mblele
-Masikio yamelala kiasi
DUROC
Asili yao inatoka tangu mwaka 1812 katika majimbo ya New York na New Jersey ambako ndio
walizalishwa kwa mara ya kwanza ingawa pia kuna tetesi kwamba waliletwa toka Uingereza
Wana rangi ya kahawia
iliyooza mpaka iliyopauka na kutaka kuwa kama njano, wana masikio yaliyolala
kwa mbele na sura ndefu ilyonyooka, wana nyama tamu sana na isiyo na mafuta
mengi, ni Mbegu inayotumika Zaidi kwenye kuchanganya na Mbegu nyingine ili
kupata uzao wenye nyama tamu na yenye mafuta kidogo, Madume ndio hutumika
kwenye kupanda majike ya Mbegu nyingine kama Large White na Lamd race sababu ni
kwamba majike ya Duroc hayazai watoto wengi
CAMBOROUGH
Hii ni Mbegu mpya ambayo inatokana na Mbegu za Large white
na Land race ambao walichanganywa kitaalam
ili kupata sifa za uzazi wa watoto wengi, ukuaji wa haraka, kutumia
chakula vizuri, uzalishaji maziwa wengi kwa ajili ya watoto, sifa ya kipekee ni uwezo wa majike kuendelea kuzaa kwa miaka mingi zaidi ukilinganisha na wengine.
Wana rangi nyeupe tupu, masikio yamelala kidogo kwa mbele na
wana uso mrefu ulioonyooka, wana uzazi wa wastani watoto 14 na majike huanza
kupandwa wakiwa na miezi 8 tu