Nilibahatika kutembelea vituo vya ufugaji na uzalishaji wa samaki huko Morogoro mjini barabara ya boma na Kingolwira, mwenyeji wangu alikuwa ni Bwana Melton Kalinga ambapo tulishinda karibia kutwa nzima akinionyesha vitu mbali mbali huku tukibadilishana uzoefu na utaalamu wa kuzalisha samaki, wakati yeye alikuwa akinifundisha namna ya kuzalisha Sato na Kambale, mimi nilimfundisha namna ya kuzalisha samaki wa mapambo hasa Gold fish na Angels
HAPA NI MOROGORO MJINI BOMA ROAD kwenye kituo cha kufugia samaki, kuna mabwawa ambapo samki hufugwa baada ya kuzalishwa katika kituo cha Kingolwira
CHANZO CHA MAJI ni kutoka katika kisima cha kuchimbwa na maji huvutwa kwa pampu ya umeme
BANDA LA BATA kinyesi chao chakula cha samaki, pia wakiogelea husaidia kuingiza hewa kwenye bwawa (aeration)
SEHEMU YA KUWEKEA CHAKULA CHA SAMAKI sehemu hii imejengwa kwa kutumia miti na inahamishika
SEHEMU YA KUWEKEA CHAKULA CHA SAMAKI imejengwa kwa saruji, ni sehemu ya kudumu
BATA pia hufukuza ndege wanaokula samaki na kuwala vyura wala samaki
NDEGE MLA SAMAKI naye alikuwepo
Mambovipi kaka shidayangu kubwa ni kuweza kuwazalisha goldfish tafadhali naomba msaadawako
ReplyDeleteMambovipi kaka shidayangu kubwa ni kuweza kuwazalisha goldfish tafadhali naomba msaadawako
ReplyDeleteJe inamchukua mda gani mfugaji kubadili maji katika bwawa la kufugia samaki?
ReplyDelete