Mbwa aliambukizwa ugonjwa huu hutoa virusi hivi kwa njia ya kinyesi, mkojo, mafua na chafya na njia ya hewa ndio njia kuu ya kusambaza ugonjwa huu kwenda kwa mbwa wengine. Maabukizi makubwa zaidi ni kwenye watoto wasiochanjwa ambao wenye umri kati ya wiki 6 - 12 ambapo kinga toka kwa mama waliyozaliwa nayo hupungua sana na kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi.
Mbwa walioambukizwa ugonjwa huu nusu yao wataonyesha dalili kidogo sana au wasionyeshe dalili za ugonjwa huu kabisa na wanaoathirika zaidi ni mbwa ambao hawapati lishe bora na kuwekwa kwenye mazingira mazuri na afya kwa ujumla.Virusi vya ugonjwa huu hushambulia ubongo, sehemu za ndani ya ngozi, macho na utando wa mfumo wa hewa na chakula na dalili za wazi huweza kuonekana baada ya siku 6 - 9 tangu kupata maambukizi
Hatua ya kwanza ya ugonjwa huu joto hupanda kufikia sentigredi 39.4 - 40.5 mbwa hupoteza hamu ya kula, hutoa machozi na majimaji puani, lakini dalili hizi ni kama za ugonjwa wa kawaida wa mafua (colds) kwenye mbwa kwa hiyo zinaweza kukuchanganya kidogo. baada ya siku chache macho huwa na matongo tongo na sio machozi tena na puani atatoa makamasi mazito na sio majimaji tena, mbwa huwa na kikohozi kikavu, hutapika, kuharisha na hii husababisha upungufu wa maji mwilini. ndani ya wiki moja au zaidi mbwa ataonekana kupata nafuu na hii hutokea zaidi kwa mbwa waliotibiwa na dawa za antibaiotiki kama OTC na Gentamycin, lakini hali hubadilika baada ya mashambulizi ya juu kutokea kwenye njia ya hewa na mfumo wa chakula
Hatua ya pili ni baada ya wiki mbili au tatu mbwa wengi wataonyesha dalili za magonjwa ya akili, kushambulia ghafla, kutingisha kichwa, kutafuna kama vile anatafuna bazoka/chewing gum, kukimbia kwa kujizungusha mduara na kuanguka chini, kupiga mateke miguu yote minne, kuona aibu na wakati mwingine anakua haoni vitu vizuri sababu ya kushambuliwa macho. Dalili nyingine ni kuvimba kwa pua na nyayo za mbwa ingawa hii haitokei sana
MATIBABU
Matibabu yanakuwa ya uhakika zaidi kama mbwa atatibiwa mapema wakati wa dalili za mwanzo kabisa, antibaiotiks husaidia sana kupunguza mashambulizi ya juu (secondary infections) ingawa hazitaua virusi vinavyosababisha ugonjwa huu, Mbwa pia watahitaji drip ya maji ili kufidia upungufu mkubwa wa maji uliosababishwa na kutapika/kuharisha, pia apewe dawa za kuzuia kuharisha na kutapika pamoja na dawa za usingizi ili apumzishe ubongo wake vya kutosha
KINGA
Hii ndio njia sahihi ya kupambana na ugonjwa huu, siku hizi kuna chanjo moja kwa ajili ya magonjwa manne DHPP (distemper, hepatitis, parvovirus, and parainfluenza combination) ambapo chanjo hii wapigwe watoto wa mbwa kabla ya kufikisha wiki 8 toka wazaliwe au wapigwe kabla kama mama yao hakuchanjwa kabisa
hongera kaka kwa kutoa mafunzo mazuri,ni mara ya kwanza kuingia blog yako hakika nimeipenda.samahani naomba nikurudishe nyuma kidogo kwenye somo la samaki, je inawezekana kufuga samaki aina ya tilapia kwenye vyombo vikubwa tofauti na mabwawa??? nitashukuru nipata kujua hili. Asante
ReplyDeleteUnaweza kuwafuga kwenye hivyo vyombo, ila unatakiwa uzingatie ubora wa maji, mzunguko wa hewa kwenye maji unaweza kuwasiliana nami kwa kupitia email yangu kwa maelezo zaidi
ReplyDeletenina mbwa kumi na moja leo ni siku ya tatu wanalala lala wengine wamevimba eneo la shingo
ReplyDeletehawali na wana dalili hizo je nifanyeje
HABARI ZA LEO MTAALAMU
ReplyDeleteMIMI MBWA WANGU WANA MIEZI MIWILI NA SIKU 21 SASA MATUMBO YAO YAMEJAA MAJI WANAKUWA KAMA WANA PREG NA LEO HII NIMEONA WANA KUNYA KINYESI CHENYE DAMU SHIDA NI NN