VIFAA
1- Majani na mabua kama chakula cha mifugo
2- Molasses ambayo hupatikana kwenye viwanda nya miwa
3- Panga au mashine ya kukata kata majani
4- Maji
5- Mfuko mkubwa mweusi wa plastiki au shimo liliojengewa kuta zake
NAMNA YA KUTENGENEZA SILAGE
1- Katakata malisho yako katika vipande vidogo vodogo kwa kutumia panga au mashine maalum.
2- Changanya molasses kiasi cha kila lita moja kwa lita mbili za maji au lita mbili na nusu za maji kama malisho ni makavu kiasi na lita tatu za maji kama malisho ni makavu zaidi
3- Changanya mchanganyiko wa maji na molasses pamoja na malisho kiasi malisho yako yalowane kisasi tu
4- Weka kwenye mfuko wako au kwenye shimo lililo jengewa na shindilia vizuri
5- Funga vizuri mfuko wako na uuweke mahali pasipo na jua
6- Kama unatuma shimo lililojengewa lifunike vizuri na plastiki na unaweza kuweka udongo kiasi juu yake
7- Hakikisha kwamba hamna hewa inayoopenya kwenye mchanganyiko wako
SILAGE ILIYOTENGENEZWA KWENYE DUMU LA PLASTIKI
MATUMIZI
Silage huwa tayari baada ya miezi 3 - 4 kutegemeana na aina ya malisho yaliyotumika, umri wa malisho, ubora wa uchanganyaji na mengineyo. Baada ya kuwa tayari unaweza kuanza kulisha mifugo yako silage uliyotengeneza wakati wa mvua nyingi, silage inauwezo wa kukaa hadi miaka minne tangu kuanza kutengenezwa kwake
FAIDA
1- Hupunguza tatizo la chakula wakati wa kiangazi
2- Huongeza utoaji wa maziwa wakati wa kiangazi
3- Mifugo huwa na afya bora hata wakati wa jua kali na malisho duni
4- Mifugo yenye afya bora huzaliana vizuri wakati wote
5- hupunguza gharana ya mashudu kwani silage ina virutubisho vingi
6- Mayai ya minyoo hufa wakati wa kutengeneza silage
Tanzania nzima we ni mkali am proud of you,
ReplyDeleteAksante sana mkuu
ReplyDeleteSafii mkuu!
ReplyDeleteUnaiacha Kwa muda gani ndani ya plastic au kwe shinu?!Na je unapofunika kuna kingine cha kufanya au kufungua ndo maana miez 3 ipite mtaalam?
ReplyDeleteNimepata elimu ya kutosha
ReplyDelete