A. Utangulizi
Chakula bora kwa Nguruwe ni moja ya suala muhimu sana kwenye dhana nzima ya
ufugaji wa Nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji. Chakula cha Nguruwe
kinagharimu kama asilimia sabini ya garama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya
matatizo mengi yanayosababisha tija na ufanisi duni wa uzalishaji wa Nguruwe
yanatokana na lishe duni. Lakini kama wakipatiwa lishe bora, tija na
ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.
B.
Baadhi ya faida za kulisha lishe bora kwa nguruwe
1. Lishe bora
huharakisha ukuaji wa haraka wa Nguruwe nahivyo kupata uzito unaohitajika kwa
kipindi kifupi.
2. Lishe bora
hupunguza gharama za ufugaji na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji kwa sababu
nguruwe atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua muda mfupi kupata
uzito mkubwa
3. Lishe bora
itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4. Lishe bora
huongeza kiasi cha mayai yatakayoivishwa na mama Nguruwe na hivyo kuongeza
idadi ya watoto watakaozaliwa
5. Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa
yatakayotengenezwa na mama Nguruwe kwa ajili ya watoto hivyo kuwafanya wawe na
afya bora itakayo wawezesha wakue haraka na kupunguza idadi ya vifo kwa watoto.
6. Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya Nguruwe na hivyo kuongeza uwezo wa kupanda
C.
Viini lishe muhimu
kwenye lishe ya nguruwe
Nguruwe wanauwezo wa
kula aina nyingi za vyakula lakini vyenye uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi. Chakula cha Nguruwe kilichokamilika kinahitaji kuwa na mchanganyiko wa viini lishe vitano,
navyo ni
1. Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini (vyakula
vyenye asili ya wanga) k.m
§
Pumba
za mchele, Pumba za mahindi, Pumba za ngano, Machicha ya pombe yaliyokaushwa, Mihogo, Viazi
vitamu, Viazi mviringo, Miwa, Ndizi mbichi, zilizoiva au zilizopikwa na makombo
ya vyakula vya asili vya wanga n.k.
2. Vyakula vya kujenga mwili (Vyakula vyenye
asili ya protini) k.m
§ Mashudu ya
alizeti, mashudu ya pamba na mawese, unga wa dagaa/samaki, damu iliyokaushwa,
soya n.k
3. Vyakula vya asili ya madini
§
Chumvi ya mezani, chokaa ya mifugo (Limestone),
mifupa iliyosagwa (bone meal), madini maalum ya nguruwe (Pig mix), madini
mchanganyiko (k.m. maklic), madini ya chuma (hasa kwa watoto wa nguruwe) n.k.
4. Vyakula vya asili ya vitamini k.m
§
Majani mabichi laini,
Mbogamboga, Matunda k.m parachichi, maembe, mapapai n.k, viungo mboga kama nyanya, bilinganya n.k.
Michanganyiko maalumu yenye viasilia vya vitamini k.m. Vitamini premix n.k.
5*. Maji
§ Hii ni lishe
muhimu kwenye chakula cha nguruwe, ila tofauti na viini lishe vingine vilovyotajwa
hapo juu ambapo nguruwe anapewa kwa vipindi/muda na kiwango maalum, maji
yanahitajika kwa nguruwe muda wote. Mahitaji ya maji ya kunywa kwa nguruwe ni
kama ifuatavyo:-
o
Nguruwe anayenyonyesha lita 20 kwa siku
o
Nguruwe aliyeachishwa kunyonyesha lita 5 kwa siku
o
Nguruwe wanaokuzwa na kunenepeshwa wenye kilo 20
hadi 90 lita 5 kwa siku
o
Watoto wa nguruwe lita 1 kila mmoja
D.
Jinsi ya kutengeneza chakula cha nguruwe
Wakati
wa kutengeneza chakula cha nguruwe inabidi kuzingatia yafuatayo:
·
Mchanganyiko wako uwe na viinilishe vinne
vilivyotajwa hapo mwanzo
· Chagua aina ya viinilishe vinavyoweza kupatikana
kwa urahisi na bei nafuu kwenye mazingira yako
· Aina ya mchanganyiko wa chakula ni muhimu
uzingatie mahitaji ya nguruwe kama umri (k.m. nguruwe wanaonyonya, waliochishwa
kunyonya, wanaokua, na wanaonyonyesha)
Mfano jedwali Na 1
linaonyesha michanganyiko mbalimbali ya vyakula vya nguruwe.
- Mchanganyiko namba 1: inapendekezwa kwa
wafugaji walioko kwenye mazingira
ambayo pumba za mahindi na mashudu ya alizeti yanapatikana kwa urahisi
- Mchanganyiko namba 2: kwa wale ambao pumba
za mahindi, za mpunga, machicha ya
pombe na mashudu ya alizeti
yanapatikana kwa urahisi.
- Mchanganyiko namba 3: kwa wale ambao
pumba za mpunga na mahindi yanapatikana kwa urahisi.
Jedwali namba 1: Michanganyiko
mbalimbali ya vyakula vya nguruwe
Na
|
Aina ya viinilishe
|
Michanganyiko
|
||
Namba 1
|
Namba 2
|
Namba 3
|
||
1
|
Vyakula vya wanga
|
|
|
|
1. Pumba za mahindi
|
70.25
|
32
|
30.00
|
|
2. Pumba laini za mpunga
|
-
|
25
|
33.00
|
|
3. Machicha ya pombe
yaliyokaushwa
|
-
|
21
|
-
|
|
4. Mahindi yaliyoparazwa
|
-
|
-
|
10.00
|
|
2
|
Vyakula vya protini
|
|
|
|
A. Protini ya nafaka
|
|
|
|
|
1. Mashudu ya alizeti
|
22.00
|
14
|
22.00
|
|
2.Mashudu ya michikichi
|
-
|
-
|
|
|
3. Soya iliyochemswa na
kuparazwa
|
-
|
-
|
-
|
|
B. Protini ya Wanyama
|
|
|
|
|
4.Unga wa dagaa/samaki
|
4.00
|
2.00
|
3.25
|
|
5.Damu iliyokaushwa
|
-
|
2.25
|
-
|
|
3
|
Vyakula viasili vya madini
|
|
|
|
|
1. Chumvi ya mezani
|
0.50
|
0.50
|
0.50
|
|
2. Chokaa ya mifugo
|
2.00
|
2.00
|
2.00
|
|
3. Unga wa mifupa
|
1.00
|
1.00
|
1.00
|
|
4. Madini na vitamini
mchanganyiko
|
0.25
|
0.25
|
0.25
|
|
Jumla
|
100.
|
100
|
100.
|
E. Kiasi na namna ya kulisha
·
Nguruwe wanahitajika kulishwa aina hii ya chakula
mara mbili (asubuhi na mchana) au zaidi kwa siku
·
Kiwango/kiasi cha kulisha kwa nguruwe wa aina na
rika tofauti kimeonyeshwa kwenye jedwali Namba 2
·
Pamoja na vyakula vilivyotajwa, wafugaji
wanashauriwa kuwapatia nguruwe vyakula vyao vya asili kama vyakula vya ziada
mfano, majani mabichi laini, majani ya maboga, mbogamboga, matunda kama
maparachichi, majani ya viazi n.k.
Jedwali na 2: Viwango vya kulisha Nguruwe wa uzito
mbalimbali
Na
|
Wakati
|
Uzito wa nguruwe (kilo)
|
kiasi cha chakula (kilo kwa siku)
|
1.
|
Baada
ya kuachishwa kunyonya hadi uzito kiasi
|
10
- 17
|
0.75
|
2.
|
Uzito
uliozidi kiasi kidogo
|
18
- 29
|
1.00
|
3.
|
Uzito
wa kawaida
|
30
- 40
|
1.50
|
4.
|
Uzito
mkubwa kiasi
|
41
- 60
|
2.00
|
5.
|
Uzito
mkubwa
|
61
- 80
|
2.5
|
6.
|
Uzito
mkubwa
|
81
- 100
|
3.00
|
Jinsi
ya kulisha makundi mbalimbali ya nguruwe
1.
Kipindi cha mamba, kuzaa hadi kuachisha kunyoyesha
1.1 Kipindi cha miezi mitatu baada ya kupandishwa
·
Apatiwe chakula kiasi k.m. kilo mbili kwa siku
·
Kiasi
hiki kiendelee hadi wiki 3 kabla ya kuzaa
1.2 Wiki tatu kabla ya kuzaa
·
Ongeza
chakula kufikia kilo 2½.
1.3
Wiki moja kabla ya kuzaa
·
Anza
kuopunguza chakula taratibu hasa vyakula vya nafaka (Concentrate rations).
·
Ongeza
vyakula vya mbogamboga, majani laini na
matunda (laxative meals).
1.4
Siku ya kuzaa
·
Usimpe
chakula chochote cha nafaka.
·
Mpe
vyakula vya mbogamboga,na vilaini kwa kiasi
kidogo tu
·
Mpatie
maji ya kutosha.
1.5 Siku ya 1 – 2 baada ya kuzaa
·
Mpe
½ kilo ya chakula kamilifu.
1.6
Siku ya 3 na kuendelea
·
Ongeza
chakula cha nafaka kwa kiasi cha kilo 1 kwa siku.
·
Ongeza
kufikia kiwango kinachohitajika kulingana na idadi ya watoto alionao mama
nguruwe.
Zingatia
·
Mama
nguruwe anahitaji kilo 3 za chakula kwa matumizi yake ya kawaida.
·
Atahitaji
kiasi cha theluthi moja (1/3)
ya kilo ya chakula kwa kila mtoto aliyenae
Mfano: kama mama ana watoto 9
atahitaji kiasi gani cha chakula?
Mahitaji
mama peke yake
|
Mahitaji
kutokana na watoto
|
Kiasi
cha chakula kwa siku
|
3kg
|
Theluthi moja x 9
|
Kilo
6 kwa siku
|
3
+ (1/3 x
9) = 6 Kg
·
Endelea
kumpa kiwango hicho cha chakula mpaka ifikapo wiki moja kabla ya kuwaachisha
watoto kunyonya.
·
Wiki
moja kabla ya kuwachisha punguza kiwango taratibu mpaka kufikia kilo 3½ kwa
siku.
Baada
ya kuachisha kunyonya
·
Mama
nguruwe apatiwe chakula bora kilicho na kiwango kikubwa cha madini
na vitamini kiwango cha kilo 2 –
3 kwa siku.
·
Hii
itamsaidia kuivisha mayai, hivyo kumsaidia kupata joto mapema.
Chakula kwa ajili ya
watoto wa nguruwe (Creep feed)
§ Hiki ni chakula
wapewacho nguruwe wachanga wakiwa
na umri wa wiki ya pili hadi wiki ya tatu.
§ Kipindi hiki mahitaji ya watoto
ni makubwa ambayo hayawezi kuteshelezwa na maziwa pekee ya mama yao.
§ Chakula hiki kitawasaidia watoto
kuzoea chakula kigumu, kutosheleza mahitaji yao, na hivyo huwawezesha watoto
kukua kwa haraka
§ Creep feed inaweza kutengenezwa
kwa kuchanganya viini lishe vifuatavyo
Aina ya viinilishe
|
Asilimia
|
Mahindi
yaliyobarazwa
|
30
|
Pumba
za mahindi
|
40
|
Mashudu
ya alizeti
|
18
|
Unga
wa Dagaa
|
10
|
Unga wa mifupa
|
0.5
|
Chokaa
ya mifugo (limestone)
|
0.75
|
Chumvi
ya mezani
|
0.5
|
Premix
|
0.25
|
Jumla
|
100
|
asante kwa maelekezo mazuri ....ningependa kujua zaidi juu ya chanjo muhimu na namna yake mana kuna maradhi kama homa ya nguruwe
ReplyDeleteNauliza, chakula(pumba) zichanganywe na maji au apewe kavu
ReplyDeleteApewe kavu
DeleteAsnte kwa maelezo mazuri
ReplyDeleteKwaiyo Mimi nnavowakorogea kwenye maji nakosea au
ReplyDeleteMbona mchanganyiko huo hauelezi ni nguruwe wa umri gani,je wa seizii ya Kati na wale wa kunenepeshwa wanakula aina moja?
ReplyDeleteBaada ya kuwalisha hivyo vyakula, je tutegemee idadi ngapi ya Watoto kuzaliwa kutoka kwa Nguruwe mmoja?
ReplyDeleteUkimpa mwanamke chakula vizuri ukimpanda ndo atazaa watoto wengi???
DeleteJe wastani wa mama Nguruwe mmoja kuzaa ni Watoto wangapi?
ReplyDelete12-14
DeleteJe mchanganyiko wenye konokono ni sawa kwa ngurue?
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeletenjema
ReplyDelete𝐴𝑠𝑎𝑛𝑡𝑒 𝑆𝑎𝑛𝑎 𝑘𝑎𝑧𝑖 𝑛𝑖𝑚𝑒𝑘𝑢𝑒𝑙𝑒𝑤𝑎 𝑠𝑎𝑛𝑎
ReplyDeleteAsante kwa kutupa MAARIFA. Baikiwa sana
ReplyDeleteAhsante kwa somo zuri ambalo limetufungua kiakiri,ubarikiwe
ReplyDeleteNguruwe umesema anakula mara2 kwa siku na kama nguruwe anakula kilo2 kwa siku je hizo kilo2 anapewa kwa kila mlo asubuhi kilo2 jioni kilo2 ambapo itakuwa jumla ya kilo4 au itakuwa asubuhi kilo1 na jioni kilo1 ipi ipo sahihi?
ReplyDeleteMaelezo mazuri. asante
ReplyDeleteKwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
ReplyDeleteAnasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
*Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159