1. SIKU 1.
Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku
moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika
maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa vitamins mfano ni
AMINOVIT na OTC plus
Pia hii huchanganywa na maji. Vifaranga wawekwe katika eneo lenye joto wastani na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifaranga wapewe
2. SIKU YA 7.
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii
huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kIsha kupewa vifaranga kwa
muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku
wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji
yenye mchanganyiko wa vitamini
3. SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD). Chanjo hii pia huchanganywa
katika maji na kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu, baada ya hapo
vifaranga wepewe mchanganyiko wa vitamin. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu unaweza kuwatambua kwa kuchana vifua vyao na hapo utaona vidoti vyekundu kama hapo pichani
4. Siku ya 21 (wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle (Kideri)
5. SIKU 28 (Mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD
6. SIKU 35 (Mwezi 1 na wiki 1)
Kipindi hiki kuku wapewe mchanganyiko wa vitamin ya kutosha.
7. WIKI YA 6-8
KUKU wapatiwe kinga ya Ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi
kwa mfugaji asiye na utaalam kuwapa kuku, tafuta mtaalum wa mifugo kwa kazi hii au upate
maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
8. WIKI YA 8
Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama Piperazzine na baada ya hapo unaweza
kurudia chanjo ya Newcastle
Ahsante kwa makala hii nzuri, ila hujafafanua huo utaratibu wa chanjo uliouainisha hapo juu kama ni maalum kwa kuku wa aina gani: kienyeji, chotara au kisasa?
ReplyDeleteswali zurii
Deletethanks for your good articles
ReplyDelete