Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
Wednesday, March 26, 2014
KILIMO BORA CHA MDALASINI - CINNAMON
Mti wa mita 10 au zaidi. Hutoa machipukizi na kuota miti zaidi ya mmoja kwenye shina moja na kuongeza mavuno mengi, haya mashina mapya yasing'olewe bali yaachwe yakue na kuwa mti mkubwa.
AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)
HALI YA HEWA NA UDONGO
· Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
· Udongo wenye rutuba
· Joto kwa wingi
· Hewa yenye unyevunyevu
KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
· Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
· Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
· Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
· Panda miche wakati wa masika
· Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka
UTUNZAJI
· Acha machipukizi kwenye shina
· Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
· Weka shamba katika hali ya safi
· Zuia magonjwa kama.
- Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.
KUVUNA
· Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
· Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
· Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
· Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
· Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
· Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
· 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
· Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini
MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
· Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
· Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
· Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
· Dawa ya ngozi
JINSI YA KUTUMIA
· kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk
· Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula
MANUFAA
· Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
· Gharama ndogo ya uzalishaji
· Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
· Magonjwa na wadudu ni kidogo
· Rahisi kuchanganya na mazao mengine
· Nguvu kidogo, kipato kikubwa.
Thursday, December 19, 2013
NDIKANA KALI - EAST COAST FEVER
Ugonjwa huu hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi na kondoo na husababishwa na vimelea vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo vusambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanavyo kama Rhepicephalus Appendiculatus, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine
Homa kali, mnyama kushindwa kupumua vizuri, kukohoa pamoja na kutoa makamasi, kuharisha na kuvimba matezi
MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za PARVAQUONE au BUTALEX kiasi cha ml 20 (soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada ya siku moja kupita, yaani ukuchoma leo unarudia dozi kesho kutwa, pia mnyama achomwe dawa ya OTC20% kipindi chote cha matibabu
KINGA
Kinga kubwa ya ugonjwa huu ni kuhakikisha kwamba mifugo yako inaoga mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo
KUPE WEKUNDU KWENYE MASIKIO YA NG'OMBE
DALILI ZA UGONJWA HUUHoma kali, mnyama kushindwa kupumua vizuri, kukohoa pamoja na kutoa makamasi, kuharisha na kuvimba matezi
MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za PARVAQUONE au BUTALEX kiasi cha ml 20 (soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada ya siku moja kupita, yaani ukuchoma leo unarudia dozi kesho kutwa, pia mnyama achomwe dawa ya OTC20% kipindi chote cha matibabu
KINGA
Kinga kubwa ya ugonjwa huu ni kuhakikisha kwamba mifugo yako inaoga mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo
NG'OMBE WAKIOGESHWA KWENYE DAWA
KUPUNGUZIA MATAWI MITI YA MITIKI - PRUNING TEAK TREES
Umuhimu wa zoezi hili ni kuhakkisha miti yako inanyooka, kukua kwa haraka na kuwa na mbao bora, miti inapokuwa na matawi haikui kwa haraka maana chakula kinagawanywa pamoja na matawi, lakini kama mti hauna matawi mengi basi hunenepa na kurefuka kwa haraka, pia kwa kuondoa matawi yakiwa machanga unoaongeza ubora wa mbao maana hazitakuwa na vidonda vinavyo sababishwa na matawi
Tuesday, November 26, 2013
IVOMEC / IVERMECTIN
Hii ni dawa inayukuja na majina kadhaa kama Ivomec, Ivermectin, Zimectin, Iverhart au Tri-heart kutegemea na iana ya mtengenezaji wa dawa hii.
Dawa hii imeonesha mfanikio makuwa katika kupambana na minyoo duara, minyoo bata, minyoo ya moyo, viroboto na ukurutu.Dawa hii huweza kutumika kwenye wanyama kama Mbuzi, Ng'ombe na Nguruwe na kutokomeza kabisa minyoo, ukurutu na hata kuua viroboto wanaonyonya damu kwenye wanyama hawa.
Dawa hii pia huweza kuja katika namna mbali mbali za matumizi kama sindano (injectable), ya kunywa (oral drench) na ya kupaka (pour/spot on) na mfugaji anaweza kuamua kununua kwa kadri ya mahitaji yake, urahisi au namna anavyopendelea yeye
Kwa njia ya sindano hupigwa chini ya ngozi (subcutaneous) ambapo kwa Ng'ombe na Mbuzi unaweza kupiga mahala popote ila kwa Nguruwe inapigwa nyuma ya sikio sababu ndio sehemu pekee mbayo haina mafuta
Dawa hii imeonesha mfanikio makuwa katika kupambana na minyoo duara, minyoo bata, minyoo ya moyo, viroboto na ukurutu.Dawa hii huweza kutumika kwenye wanyama kama Mbuzi, Ng'ombe na Nguruwe na kutokomeza kabisa minyoo, ukurutu na hata kuua viroboto wanaonyonya damu kwenye wanyama hawa.
Dawa hii pia huweza kuja katika namna mbali mbali za matumizi kama sindano (injectable), ya kunywa (oral drench) na ya kupaka (pour/spot on) na mfugaji anaweza kuamua kununua kwa kadri ya mahitaji yake, urahisi au namna anavyopendelea yeye
Kwa njia ya sindano hupigwa chini ya ngozi (subcutaneous) ambapo kwa Ng'ombe na Mbuzi unaweza kupiga mahala popote ila kwa Nguruwe inapigwa nyuma ya sikio sababu ndio sehemu pekee mbayo haina mafuta
Friday, November 22, 2013
Friday, November 15, 2013
Tuesday, October 8, 2013
Tuesday, October 1, 2013
FARASI WANAUZWA - HORSES FOR SALE
Jumla kuna farasi watano, wote bado vijana hakuna aliyezeeka, 1. jike mweusi wa miaka minne ana mimba bei Tsh 5,500,000/= 2. jike mweupe wa miaka miwili Tsh 4,200,000/= 3. Jike wa miaka miwili rangi ya hudhurungi isiyokooza bei Tsh 4,200,000/= 4. Dume wa miaka miwili rangi ya kahawia bei Tsh 4,200,000/= kwa mawasiliano zaidi piga simu namba +255 786 763 265
5 Young horses for sale. 1. Black pregnant female 4 years old. - 5, 500, 000 TSHS 2. White female horse 2 years old. 3. Greyish white male for sale 2 years old. 4. A light brown mixed white foal of 2 months Contact: : +255 786 763 265 All others are for $2500 0r 4, 200 000 Tsh
Friday, September 27, 2013
NG'OMBE - KWA TAARIFA YAKO
Ng'ombe mwenye afya kwa kawaida pua yake huwa na unyevu unyevu au kama vile inatoa jasho jembamba sana.Ukiona ng'ombe wako ana pua iliyokauka na haina unyevuunyevu basi ujue
hiyo ni dalili kwamba kuna tatizo katika mwili wake, hii inaweza pia
kuwa dalili ya maambukizi au magonjwa
Pua ya ng'ombe inauwezo wa kunusa umbali wa kilometa 8 au maili 5, ndio maana wanaweza kukimbia machungoni au hata kuvunja banda na kufuata mazao mashambani sababu ya harufu, msimu wa membe tatizo la kutoroka ndio huwa kubwa hasa maembe yapaoanza kuiva
Kwa siku hutumia masaa 6 kula chakula na hutumia masaa 8 kucheua na na kutafuna tena na hunywa maji kiasi cha lita 12 mpaka 25 kutegemeana na ukubwa na hula kiasi cha kilo mpaka 45 kwa ng'ombe wakubwaNg'ombe mwenye kilo 1000 huweza kuzalisha kiasi cha tani 10 za mbolea kwa mwaka
Mpwapwa breed ni mbegu ya ng;ombe iliyo patikana nchini Tanzania baada ya tafiti kadhaa za kitaalam
Thursday, September 19, 2013
MBWA - KWA TAARIFA YAKO
Kama unafuga mbwa na umemzoea basi kila mara unapokaa naye mchunguze namna macho yake yanavyo jaribu kuwasiliana na wewe kila mara, mara zote macho haya hofuatana na lugha ya mwili (body language)
Anapokuwa na furaha, anahitaji kitu, kuna hatari, joto au baridi sana au hata anaumwa ishara ya macho pia huonekana
Kama umemzoea mbwa wako unaweza kuanza kuhisi kama kuna kitu hakiko sawa kwa kumuangalia kwenye macho, cha muhimu ni kujua akiwa kwenye hali ya kawaida macho yake yanakuwa kwenye hali gani au huwa anakuangalia vipi?
Mbwa hunywa maji kwa kuukunja ulimi wake kwa nyuma na kuyachota kisha kuyaingiza mdomoni, tofauti na wengi wanavyojua kwamba huwa analamba maji
Mbwa haonyeshwi upendo kwa kukumbatiwa, kama ulikuwa unafanya hivyo acha mara moja maana mbwa hutafsiri kukumbatiwa kawa kuonyesha utawala wako, mbwa anayetawala ndio hukumbatia wenzake kama ishara ya ukuu
Mikanda ya mbwa ya shingoni iligunduliwa zama za ugiriki ya zamani, nia kuu ilikuwa kuwalinda mbwa dhidi ya mashambulizi ya wanyama wengine kama mbweha na fox
Tuesday, September 10, 2013
KILIMO BORA CHA MATANGO - KWENYE VYOMBO
Kilimo hiki kinaweza kufanyika kwa watu wanaoishi ghorofani au sehemu yenye ardhi ambayo haifai kwa kilimo, mfano mchanga mwingi hasa sehemu ambazo zipo karibu na bahari au ardhi yenye mawe mawe
Nimetumia boksi la mbao (upana sentimeta 25) ambalo lilitumika kujengea nguzo za nyumba, baada ya hapo lilikuwa limekaa bila kazi yoyote. nikatoa mbao ya juu, nikaziba pembeni na keweka udongo wenye rutuba ndani yake nikichanganya na mbole vunde, nikaweka nguzo mbili na kuweka nyavu ya vibox box ambayyo imeondolewa kwenye ukarabati wa nyumba, wewe unaweza kutumia waya za kawaida na kuzishona shona, hakikisha chini ya box lako kuna matundu ya kupitisha maji ili maji yasituame.
Matango ni vizuri kama mbebu zake ukapanda moja kwa moja, sia mbegu moja kiasi cha sentimita moja chini ya udongo na umbali kati ya mbegu na mbegu usipungue sentimeta 30 na zaidi, Sehemu ya kupandia iwe na jua la kutosha kwani matango huhitaji kiasi cha jua kisichopngua masaa 6 - 8 kwa siku, mwagia maji ya kutosha angalau mara moja kwa siku hasa nyakati za jioni
Baada ya wiki moja mbegu zako zitaanza kuota, endelea kumwagia maji kila siku, baada ya wiki mbili mpaka tatu mimea itakua na kuanza kutaka kutambaa, hakikisha haitambai sehemu moja na kuanza kubanana, itenganishe na ikue kwa kupeana nafasi
Hakikisha matawi yote unayaondoa kwa kuyavunja na mikono yakiwa madogo, mmea wenye mayawi mengi utakupa mazao dhaifu kwa sababu ya kutumia rutuba nyingi na mimea itabanana na kuanza kugombea nish ti ya jua
Mmea wa matango huwa na majani, kamba za kujishikiza, maua na matawi, kabla ya kuondoa matawi ni lazima ujue kutofautisha kati ya maua na matawi maana hufanana sana yakiwa madogo na huota sehemu moja kati ya tawi na jani, kama huna uhakika lipi ni tawi na lipi ni ua subiri siku moja au mbili na utaona tofauti maana matawi hukua haraka sana kuliko maua
MAUA YAKIWA YAMEBAKI YENYEWE BILA YA MATAWI
Subscribe to:
Posts (Atom)