Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
Wednesday, September 16, 2009
HOLSTEIN FRIESIAN - kinara wa utoaji maziwa duniani
ASILI YAKE
Uholanzi katika jimbo la friesland
UZALISHAJI KWA MWAKA
10,158 kg za maziwa
3.64% mafuta
3.05% protini
RANGI
nyeupe na nyeusi, mkia huwa na rangi nyeupe na kwenye paji la uso huwa na rangi nyeupe yenye umbo kama la pembe tatu ,mara chache (1/1000) huzaliwa ndama mwenye rangi nyekundu na nyeupe
UZITO
kilo 1200 majike
kilo 1400 madume
Huyu ndiye aina ya ng'ombe anayeshikilia rekodi ya uzalishaji maziwa kwa kiwango cha juu, maziwa yake hayana mafuta mengi. Nimeshuhudia akitoa maziwa zaidi ya lita 70 kwa siku kwa mikamuo mitatu lita 30 / 20 / 25 Madume yanatumika kwa kulimia na kukokota mikokoteni, Ni mkubwa kushinda nyati ambaye ana uzito wa kilo 800-1000, kama wanavyoonekana kwenye picha urefu wao ni sawa na kimo cha mtu mwenye urefu wa wastani. Kwa Tanzania wanapatikana zaidi Kitulo mkoani Iringa na Uyole (kituo cha utafiti wa kilimo) Mkoani Mbeya, aina hii ya ng'ombe hustawi zaidi katika mazingira yenye baridi kali.
Kama unataka mbegu hii wasiliana na maafisa ugani wa mifugo ili waje kupandisha ng'ombe wako kwa njia ya chupa, mbegu zinazotumika kwa njia hii hutoka kwa madume PURE BREED CLASS A na matokeo yake ni kupata ndama bora
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
14 comments:
Bei zake haw ng'ombe zikoje mkuu?
Itabidi niende Uyole ila ni kweli bei yake ikoje. Asante tena kwa uhabarishaji huu.
Ngoja niwasiliane na wadau walioko Mbeya niweze kupata bei zao, ingawa jamaa wanauza zaidi madume na kubakisha majike kwa ajili ya mbegu kwa sababu Ngombe sio wengi sana
Shukran ila tunasubiri kupata bei zake, ikiwezekana pamoja na usafiri kwenda mkoa mwingine
Uyole hawauzi, Kitulo wanauza Tsh 1,000,000 kwa DSm wanapatikana kwa Tsh 600,000 Tanga kituo cha utafiti 550,000 na pia kuna Mama anaitwa Ruth (Tanga)anauza 700,000. . Hawa wote ni ng'ombe wenye mimba
KIASI CHA UZALISHAJI (wastani)
kitulo - 50 litres
Ruth - 30 litres
Tanga utafiti - 17-20 litres
Dsm 10-15 litres
Asante Mkuu!
Shukran Mkuu
Jamani hao ng`ombe bado wanapatikana? Nijuze tafadhali - Mfugaji mdogo
Gratian Kasenene
0715009952
Mkubwa Benet nisaidie kupata ng`ombe bora nimfugaji wa kawaida kwa miaka 10 sasa ila nataka kuboresha mifugo iwe ya kisasa- pia nimesikia pale UDSM Engineering wanatengeneza mtambo rahisi wa kuchanganyia chakula cha ng`mbe je? nikweli
na mm nahitaji hiyo aina ya ngombe.nipo dar lakini nataka kumsafirisha kwenda songea.naomba mnijuze kama bado wanapatikana
na mm nahitaji hiyo aina ya ngombe.nipo dar lakini nataka kumsafirisha kwenda songea.naomba mnijuze kama bado wanapatikana
Natafuta ng'ombe wa maziwa wazuri wapi naweza kuwapata no 0718013034
NAOMBA MAWACLIANO KITULO HAO WATU TUNATAKA KUFUGA
Naomba namba zako kaka nahitaji toka kitulo
Post a Comment