KURASA

Thursday, December 19, 2013

NDIKANA KALI - EAST COAST FEVER

Ugonjwa huu hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi na kondoo na husababishwa na vimelea vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo vusambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanavyo kama Rhepicephalus Appendiculatus, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine


KUPE WEKUNDU KWENYE MASIKIO YA NG'OMBE

DALILI ZA UGONJWA HUU
Homa kali, mnyama kushindwa kupumua vizuri,  kukohoa pamoja na kutoa makamasi, kuharisha na kuvimba matezi

MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za  PARVAQUONE au BUTALEX kiasi cha ml 20 (soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada  ya siku moja kupita, yaani ukuchoma leo unarudia dozi kesho kutwa, pia mnyama achomwe dawa ya OTC20% kipindi chote cha matibabu



KINGA
Kinga kubwa ya ugonjwa huu ni kuhakikisha kwamba mifugo yako inaoga mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo

NG'OMBE WAKIOGESHWA KWENYE DAWA

KUPUNGUZIA MATAWI MITI YA MITIKI - PRUNING TEAK TREES

 

Umuhimu wa zoezi hili ni kuhakkisha miti yako inanyooka, kukua kwa haraka na kuwa na mbao bora, miti inapokuwa na matawi haikui kwa haraka maana chakula kinagawanywa pamoja na matawi, lakini kama mti hauna matawi mengi basi hunenepa na kurefuka kwa haraka, pia kwa kuondoa matawi yakiwa machanga unoaongeza ubora wa mbao maana hazitakuwa na vidonda vinavyo sababishwa na matawi

Tuesday, November 26, 2013

IVOMEC / IVERMECTIN

Hii ni dawa inayukuja na majina kadhaa kama Ivomec, Ivermectin, Zimectin, Iverhart au Tri-heart kutegemea na iana ya mtengenezaji wa dawa hii.


 Dawa hii imeonesha mfanikio makuwa katika kupambana na minyoo duara, minyoo bata, minyoo ya moyo, viroboto na ukurutu.Dawa hii huweza kutumika kwenye wanyama kama Mbuzi, Ng'ombe na Nguruwe na kutokomeza kabisa minyoo, ukurutu na hata kuua viroboto wanaonyonya damu kwenye wanyama hawa.






Dawa hii pia huweza kuja katika namna mbali mbali za matumizi kama sindano (injectable), ya kunywa (oral drench) na ya kupaka (pour/spot on) na mfugaji anaweza kuamua kununua kwa kadri ya mahitaji yake, urahisi au namna anavyopendelea yeye

Kwa njia ya sindano hupigwa chini ya ngozi (subcutaneous) ambapo kwa Ng'ombe na Mbuzi unaweza kupiga mahala popote ila kwa Nguruwe inapigwa nyuma ya sikio sababu ndio sehemu pekee mbayo haina mafuta

Friday, November 15, 2013

Tuesday, October 1, 2013

FARASI WANAUZWA - HORSES FOR SALE

 
 Jumla kuna farasi watano, wote bado vijana hakuna aliyezeeka, 1. jike mweusi wa miaka minne ana mimba bei Tsh 5,500,000/=  2. jike mweupe wa miaka miwili Tsh 4,200,000/= 3. Jike wa miaka miwili rangi ya hudhurungi isiyokooza bei Tsh 4,200,000/= 4. Dume wa miaka miwili rangi ya kahawia bei Tsh 4,200,000/= kwa mawasiliano zaidi piga simu namba +255 786 763 265


 
5 Young horses for sale. 1. Black pregnant female 4 years old. - 5, 500, 000 TSHS 2. White female horse 2 years old. 3. Greyish white male for sale 2 years old. 4. A light brown mixed white foal of 2 months Contact: : +255 786 763 265 All others are for $2500 0r 4, 200 000 Tsh

Friday, September 27, 2013

NG'OMBE - KWA TAARIFA YAKO

 Ng'ombe mwenye afya kwa kawaida pua yake huwa na unyevu unyevu au kama vile inatoa jasho jembamba sana.Ukiona ng'ombe wako ana pua iliyokauka na haina unyevuunyevu basi ujue hiyo ni dalili kwamba kuna tatizo katika mwili wake, hii inaweza pia kuwa dalili ya maambukizi au magonjwa
 Pua ya ng'ombe inauwezo wa kunusa umbali wa kilometa 8 au maili 5, ndio maana wanaweza kukimbia machungoni au hata kuvunja banda na kufuata mazao mashambani sababu ya harufu, msimu wa membe tatizo la kutoroka ndio huwa kubwa hasa maembe yapaoanza kuiva
Kwa siku hutumia masaa 6 kula chakula na hutumia masaa 8 kucheua na na kutafuna tena na hunywa maji kiasi cha lita 12 mpaka 25 kutegemeana na ukubwa na hula kiasi cha kilo mpaka 45 kwa ng'ombe wakubwa
Ng'ombe mwenye kilo 1000 huweza kuzalisha kiasi cha tani 10 za mbolea kwa mwaka
Ng'ombe aina ya friesian (pichani juu)ambao ni kinara wa uzalishaji wa maziwa duniani wana rangi nyeupa na mabaka meusi ambapo haya mabaka meusi hayafanani kama zilivyo alama za vidole kwa binadamu. ng'ombe anauwezo wa kusikia sauti ndogo na kubwa zaidi ya binadamu

Mpwapwa breed ni mbegu ya ng;ombe iliyo patikana nchini Tanzania baada ya tafiti kadhaa za kitaalam

Thursday, September 19, 2013

MBWA - KWA TAARIFA YAKO



 Kama unafuga mbwa na umemzoea basi kila mara unapokaa naye mchunguze namna macho yake yanavyo jaribu kuwasiliana na wewe kila mara, mara zote macho haya hofuatana na lugha ya mwili (body language)
 Anapokuwa na furaha, anahitaji kitu, kuna hatari, joto au baridi sana au hata anaumwa  ishara ya macho pia huonekana
 Kama umemzoea mbwa wako unaweza kuanza kuhisi kama kuna kitu hakiko sawa kwa kumuangalia kwenye macho, cha muhimu ni kujua akiwa kwenye hali ya kawaida macho yake yanakuwa kwenye hali gani au huwa anakuangalia vipi?

 Mbwa hunywa maji kwa kuukunja ulimi wake kwa nyuma na kuyachota kisha kuyaingiza mdomoni, tofauti na wengi wanavyojua kwamba huwa analamba maji
 Mbwa haonyeshwi upendo kwa kukumbatiwa, kama ulikuwa unafanya hivyo acha mara moja maana mbwa hutafsiri kukumbatiwa kawa kuonyesha utawala wako, mbwa anayetawala ndio hukumbatia wenzake kama ishara ya ukuu
 Mikanda ya mbwa ya shingoni iligunduliwa zama za ugiriki ya zamani, nia kuu ilikuwa kuwalinda mbwa dhidi ya mashambulizi ya wanyama wengine kama mbweha na fox


Tuesday, September 10, 2013

KILIMO BORA CHA MATANGO - KWENYE VYOMBO

Kilimo hiki kinaweza kufanyika kwa watu wanaoishi ghorofani au sehemu yenye ardhi ambayo haifai kwa kilimo, mfano mchanga mwingi hasa sehemu ambazo zipo karibu na bahari au ardhi yenye mawe mawe

 Nimetumia boksi la mbao (upana sentimeta 25) ambalo lilitumika kujengea nguzo za nyumba, baada ya hapo lilikuwa limekaa bila kazi yoyote. nikatoa mbao ya juu, nikaziba pembeni na keweka udongo wenye rutuba ndani yake nikichanganya na mbole vunde, nikaweka nguzo mbili na kuweka nyavu ya vibox box ambayyo imeondolewa kwenye ukarabati wa nyumba, wewe unaweza kutumia waya za kawaida na kuzishona shona, hakikisha chini ya box lako kuna matundu ya kupitisha maji ili maji yasituame.




Matango ni vizuri kama mbebu zake ukapanda moja kwa moja, sia mbegu moja kiasi cha sentimita moja chini ya udongo na umbali kati ya mbegu na mbegu usipungue sentimeta 30 na zaidi, Sehemu ya kupandia iwe na jua la kutosha kwani matango huhitaji kiasi cha jua kisichopngua masaa 6 - 8 kwa siku, mwagia maji ya kutosha angalau mara moja kwa siku hasa nyakati za jioni


 Baada ya wiki moja mbegu zako zitaanza kuota, endelea kumwagia maji kila siku, baada ya wiki mbili mpaka tatu mimea itakua na kuanza kutaka kutambaa, hakikisha haitambai sehemu moja na kuanza kubanana, itenganishe na ikue kwa kupeana nafasi


 Hakikisha matawi yote unayaondoa kwa kuyavunja na mikono yakiwa madogo, mmea wenye mayawi mengi utakupa mazao dhaifu kwa sababu ya kutumia rutuba nyingi na mimea itabanana na kuanza kugombea nish ti ya jua

 Mmea wa matango huwa na majani, kamba za kujishikiza, maua na matawi, kabla ya kuondoa matawi ni lazima ujue kutofautisha kati ya maua na matawi maana hufanana sana yakiwa madogo na huota sehemu moja kati ya tawi na jani, kama huna uhakika lipi ni tawi na lipi ni ua subiri siku moja au mbili na utaona tofauti maana matawi hukua haraka sana kuliko maua






 MAUA YAKIWA YAMEBAKI YENYEWE BILA YA MATAWI