KURASA

Friday, April 10, 2009

UMUHIMU WA MITI

SEHEMU YA MSITU




Kuna usemi usemao MISITU NI UHAI ambao nina uhakika kila mtu anaujua vema, swala kubwa hapa ni jinsi ya kuitunza hii rasilimali ya asili tuliyopewa na mungu. Misitu yetu ambayo tunaitegemea kwa mambo mengi sana siku hizi imekuwa ikikatwa miti yake kwa ajili ya matumizi mbali mbali kama mbao na kuni, matumizi mengine kama dawa huwa hayana athari sana kwa misitu kwa sababu mtumiaji huchukua sehemu tu ya mti.

MTI WA MVULE


Kuna misitu ya asili na ile ya kupandwa, hii ya kupandwa iko ya aina mbili, kuna yenye miti ya asili ambayo madhumuni yake huwa ni kutunza mazingira au kurudisha hali ya uasilia (uoto wa asili) na kuna miti ya kigeni ambayo mara nyingi huwa kwa matumizi ya biashara au kipato, miti ya kigeni ni kama mikaratusi, mitiki (misoji), mipine, mivinje, migravilea n.k






Adui mwingine mkubwa wa misitu ni moto, vyanzo vya moto vinaweza kuwa shughuli za kilimo kwa maana ya kusafisha shamba, uwindaji ukiwa na nia ya kufukuza wanyama toka upande mmoja hadi mwingine, na urinaji wa asali ambapo moto huwashwa halafu majani mabichi ya aina fulani huchomwa ili kutoa moshi ambao huwalewesha nyuki.







VYANZO VYA MAJI

Vyanzo vingi vya maji huanzia kwenye misitu juu ya milima ambapo huanza kama chem chem kisha vijito halafu maji hutiririka kama mto. Kazi ya misitu ni kuzuia yale maji maji kuzama ardhini (mizizi) na pia majani ya miti huzuia maji maji yasichukuliwe kama mvuke

Chem chem nyingine hupita chini ya ardhi na kwenda kuibuka sehemu nyingine kama kisima cha asili, sehemu za misitu ambazo zimeharibiwa na ukataji miti kiasi cha kuathiri mfumo wa maji basi miti kama mikuyu na mikangazi hushauriwa kupandwa kwa wingi sehemu hizi, ingawa bado miti ya asili ya sehemu husika nayo pia inaweza kupandwa.Miti ya asili nchini kwetu ni kama mivule, mipodo, mininga, mikangazi, mikarambati n.k