KURASA

Wednesday, January 5, 2011

VIWAVI JESHI WAVAMIA MASHAMBA MASASI


Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imevamiwa na viwavi jeshi tangu mwisho wa mwaka 2010 na mwanzo wa mwaka huu na kuharibu zaidi ya Ekari 300 za mazao aina mbali mbali yalimwayo katika wilaya hiyo.

Viwavi hao wameonakena kwa wastani wa wiki mbili walionekana kwa wingi zaidi katika vijiji vya Mkaseka, Lulindi, Mbaju, Chigugu na Namalenga wilayani humo.

Wilaya za jirani ziliweza kuwasaidia wilaya ya masasi kwa kuwapa dawa za kuulia wadudu hao hatari kwa mazao, Wilaya ya Tandahimba ilitoa dawa kiasi cha lita 100 wakati wilaya yaNAnyumbu ilitoa kiasi cha lita 20 na kufanya kuwa na jumla ya lita 120. Mahitaji kamili baada ya makisio ya awali yalikuwa lita 150 kwa hiyo baada ya kupewa lita 120 kumekuwa na upungufu wa lita 30, hii ni kwa mujibu wa mkuu wa wilaya hiyo Nape Nnauye wakati akitoa taarifa hii.





Jitihada za kupiga dawa na mvua zinazoendelea kunyesha zimeonyesha matunda makubwa na sasa hivi wakulima wameanza tena kupanda mazao ya mtama, mahindi na mihogo.