KURASA

Sunday, April 12, 2009

MALARIA-Jinsi ya kuharibu mazalia ya mbu

MBU



Malaria limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa nchi kama Tanzania, ambazo ni masikini na uwepo wake katika ikweta kunifanya iwe na joto na hivyo uwepo wa mbu wengi sana. Makala nyingi na kampeni zimekuwa juu ya kutibu malaria na nyingine juu ya kukinga malaria kwa njia kama za kutumia vyandarua vyenye dawa, kumeza dawa kwa wale wanaotembelea maeneo yenye mbu wengi (hasa wanaotoka ughaibuni) ambako hamna malaria
Njia kubwa ya kujikinga na malaria ni kuharibu mazingira ya mbu kuzaana, kwenye mazingira mengi tunayoishi ndizo sehemu mbu wanakozaliana, kwa hiyo inatubidi kufanya yafuatayo kupunguza au kuondoa mazalia ya mbu.


MADIMBWI

Kufukia madmbwi yote yanayozunguka nyumba tunazoishi na mazingira tuliyopo ili kuhakikisha hamna maji yanayotuama jirani na makazi yetu. Hii pia inahusisha kuondoa vitu vyote vinavyoweza kuhifadhi maji mara mvua inaponyesha, vitu kama vifuu vya nazi, makopo, matairi ya magari n.k


MAJANI

Ni muhimu kufyeka au kulima majani yote na vichaka kuzunguka makazi yetu hasa vipindi vya mvua, pia maua ambayo ni urembo wa nyumba zetu nayo inabidi yapunguzwe kipindi hiki. Kwa kawaida mimea huwa na uwezo wa kutuamisha maji kidogo sana kwenye majani yake lakini mbu nao hutaga humo humo.


NJIA NYINGINE
Kuna baadhi ya mimea ambayo inauwezo wa kufukuza wadudu, kwa mfano mmea unaojulikana kama nyonyo (cast oil) ukipandwa karibu na makazi yetu una uwezo wa kufukuza mbu (repellent) na mbegu zake zikipondwa na kuchanganywa na maji na kisha kumwagwa sehemu basi huweza kufukuza wadudu kama mbu.

MMEA WA NYONYO (castor oil)



Kupulizia dawa za kuua wadudu (mf Icon) ni njia nyingine ya kuzuia mbu kuzaana, hii ni njia ya kemikali kwa hiyo iwe ya mwisho baada ya hizi za mwanzo zote kushindwa kufanya kazi au kutonyesha mafanikio.