Kilimo hiki kinaweza kufanyika kwa watu wanaoishi ghorofani au sehemu yenye ardhi ambayo haifai kwa kilimo, mfano mchanga mwingi hasa sehemu ambazo zipo karibu na bahari au ardhi yenye mawe mawe
Nimetumia boksi la mbao (upana sentimeta 25) ambalo lilitumika kujengea nguzo za nyumba, baada ya hapo lilikuwa limekaa bila kazi yoyote. nikatoa mbao ya juu, nikaziba pembeni na keweka udongo wenye rutuba ndani yake nikichanganya na mbole vunde, nikaweka nguzo mbili na kuweka nyavu ya vibox box ambayyo imeondolewa kwenye ukarabati wa nyumba, wewe unaweza kutumia waya za kawaida na kuzishona shona, hakikisha chini ya box lako kuna matundu ya kupitisha maji ili maji yasituame.
Matango ni vizuri kama mbebu zake ukapanda moja kwa moja, sia mbegu moja kiasi cha sentimita moja chini ya udongo na umbali kati ya mbegu na mbegu usipungue sentimeta 30 na zaidi, Sehemu ya kupandia iwe na jua la kutosha kwani matango huhitaji kiasi cha jua kisichopngua masaa 6 - 8 kwa siku, mwagia maji ya kutosha angalau mara moja kwa siku hasa nyakati za jioni
Baada ya wiki moja mbegu zako zitaanza kuota, endelea kumwagia maji kila siku, baada ya wiki mbili mpaka tatu mimea itakua na kuanza kutaka kutambaa, hakikisha haitambai sehemu moja na kuanza kubanana, itenganishe na ikue kwa kupeana nafasi
Hakikisha matawi yote unayaondoa kwa kuyavunja na mikono yakiwa madogo, mmea wenye mayawi mengi utakupa mazao dhaifu kwa sababu ya kutumia rutuba nyingi na mimea itabanana na kuanza kugombea nish ti ya jua
Mmea wa matango huwa na majani, kamba za kujishikiza, maua na matawi, kabla ya kuondoa matawi ni lazima ujue kutofautisha kati ya maua na matawi maana hufanana sana yakiwa madogo na huota sehemu moja kati ya tawi na jani, kama huna uhakika lipi ni tawi na lipi ni ua subiri siku moja au mbili na utaona tofauti maana matawi hukua haraka sana kuliko maua
MAUA YAKIWA YAMEBAKI YENYEWE BILA YA MATAWI