JSFoundation-flyer

JSFoundation-flyer

KURASA

Thursday, December 22, 2016

SOKO LA SUNGURA

Watu wengi wangependa kuingia kwenye ufugaji wa sungura kwa sababu ni rahisi kuwafuga na hawahitaji muda mwingi wa kuwaangalia na zile kazi maalum zinaweza kufanyika siku za mwisho wa wiki. Lakini tatizo limekuwa soko la uhakika mfano leo unataka kuwauza au kupeleka nyama nani ananunua?


Kama una soko la uhakika la Sungura weka contact zako humu kila mtu ajue namna ya kukupata?


Tuesday, July 12, 2016

AGRI-HUB TANZANIA

Agri-Hub Tanzania ilizinduliwa rasmi Oktoba 2012. Uzinduzi huo ulikuwa tukio lenye maana kubwa kwa wote waliokuwepo, ikizingatiwa kwamba ipo haja kubwa ya kushrikiana na kuunganisha juhudi katika uimarishaji wa kilimo. Serikali ilifurahishwa na hatua hii ambayo pia iliungwa mkono na sekta binafsi, jumuiya za wakulima na asasi za kijamii. Wanachama wa Agri-Hub wameunda vikundi-kazi 5 ambavyo vitakuwa na shughuli zifuatazo: uhamasishaji, mafunzo, kuratibu utendaji na mbinu za kibunifu kwa lengo la kuimarisha uzalishaji endelevu wa chakula na kuboresha maisha ya wakulima wa Mkoa wa Arusha.


Shughuli za awali

Kundi la uchanganuzi lililopendekezwa na wanachama kadhaa wa Agri-ProFocus na wadau wengine nchini lilileta msukumo uliowezesha kuanzishwa Agri-Hub Tanzania. Hadi kufikia sasa, tayari jumuiya zipatazo 25 zimeshajiunga na taasisi hii, ikiwa ni pamoja na: SNV, RijkZwaan, TRIAS, Cordaid, Hivos, Agriterra, Farm Africa na Faida Mali. Taasisi zote zina dhamira moja: kuunga mkono shughuli za Agri-Hub Tanzania kwa kujitolea kwa hali na mali katika kuendeleza Agri-Hub. Arusha, jiji lililo kaskazini mwa Tanzania ambalo lina umuhimu mkubwa katika shughuli za kilimo likiwa pia ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), liliteuliwa kuwa makao makuu anzilishi ya Agri-Hub.

Upangaji wa agenda: Warsha wa wadau wa sekta mbalimbali

Hafla ya kikazi iliyofanyika tarehe 5, Oktoba ilitayarishwa kwa lengo la kuwaarifu wadau wa kilimo na wengineo wenye ushirika na kilimo katika Mkoa wa Arusha, juu ya mikakati iliyokuwa ikitayarishwa na pia, juu ya warsha wa mipango.

Warsha wa Wadau wa Sekta Mbalimbali (22 – 23 Oktoba, 2012) ilitoa fursa kwa wanachama wa Agri-Hub kupanga Agenda.

Wakati wa warsha, wanachama waliunda vikundi-kazi vifuatavyo:

- Upatikanaji wa Ardhi

- Upatikanaji wa Mitaji

- Upatikanaji wa Pembejeo

- Upatikanaji wa Masoko

- Mtazamo wa Kibiashara kwa Wakulima

Upatikanaji wa ardhi

Ijapokuwa sheria za Tanzania zinatambua haki ya wakulima wadogo kumiliki ardhi na kufanya shughuli za kilimo kwenye ardhi hiyo, wakazi wengi wa vijijini hawajaelimishwa juu ya manufaa mengi wawezayo kuyapata kutokana na ardhi yao.

Kikundi-kazi hiki kina lengo la kuboresha hali ya wakulima kwa kuwapa mafunzo na wadau wengine wa ardhi jinsi ya kutumia kwa manufaaa yao Sheria za Ardhi zilizopo.

Upatikanaji wa mitaji

Huduma za kifedha kwa wakulima ni suala muhimu kwa jamii inayotegemea kilimo kama Tanzania. Kikundi-kazi cha mitaji kimetayarisha mlolongo wa shughuli kwa minajili ya kuunga mkono harakati za utafutaji wa mitaji kwa miaka mingi ijayo. Kikundi hiki kinatazamia kupanga na kujenga ushirikiano na mikakati ambayo tayari ipo (kama vile like Maonyesho ya Kilimo-Biashara, nk) kwa lengo la kuongeza utelekelezaji na utendaji wa kiwango cha juu iwezekanavyo.

Upatikanaji wa Pembejeo

Kulingana na mtazamo wa kikundi-kazi cha pembejeo, upatikanaji na uwepo wa taarifa kamili juu ya pembejeo ni jukumu la pamoja la wakulaima, makampuni mbalimbali na serikali.

Kikundi hiki kimetayarisha shughuli mbalimbali zenye lengo la kuunganisha hawa wadau wote ili waweze kufikia lengo hili:kuwaelekeza wakulima wajue ni wapi pa kupatia pembejeo na waweze kufanya uteuzi sahihi wa pembejeo hizo na jinsi ya kuzitumia.

Upatikanaji wa Masoko

Maudhui ya kipengele hiki yanajumuisha maudhui mengine kadhaa madogovidogo, kama vile: Mfumo wa taarifa za masoko, kukutana na wanunuzi, kilimo cha mkataba na mengineyo. Hatua inayofuata ni kuangalia ni nini ambacho kila mwanachama wa kikundi-kazi anaweza kuchangia katika majadiliano. Aidha, kunakuwepo na uchunguzi kuona ni jumuiya gani ambazo zingepaswa kuhusishwa lakini bado hazipo, ili ziweze kuunaginshwa na Agri-Hub.

Mtazamo wa kijasiriamali kwa wakulima

Kujengea wakulima mtazamo wa kijasiriamali ndio lengo kuu la Agri-ProFocus. Lakini je, ni kwa vipi tutaweza kutekeleza azma hii katika kiwango cha kimkoa? Kikundi-kazi hiki kinalenga kuwahamasisha wakulima wenye upeo wa juu kuliko wenzao, waweze kuthibitisha wazi kuwa kilimo biashara yenye tija kama biashara zingine, iwapo itaendeshwa kwa njia sahihi.

Je, ungependa kujiunga?

Shughuli za Agri-Hub zimo katika matayarisho na utekelezaji wake utaanza hivi karibuni. Iwapo una nia ya kuingiza mada yako katika agenda, basi jiunge na vikunndi-kazi vilivyoorodheshwa hapo juu mapema iwezekanavyo. Agri-Hub Tanzania itakuwezesha kupata washirika ambao, kwa kujiunga nao, utaweza kufanikiwa katika malengo yako!

Kwa maelezo zaidi:

Apollo Muyanja Mbazzira (SNV)

Mratibu wa Agri-Hub Tanzania

Baruapepe: amuyanja.agrihub@gmail.com

Simu: +255 22 260 0340

Marjolein de Bruin

Mwezeshaji mtandao: mdebruin@agri-profocus.nl

Simu: +31 (0)26 3542056

Jiunge na jukwaa la Intaneti:

http://apf-tanzania.ning.com/   Agri-Hub Tanzania, Plot 1124, Chole Road, Msasani Peninsular, P.O. Box 3941, Dar es Salaam, Tanzania

Agri-ProFocus, Willemsplein 43-II / P.O. Box 108 – 6800 AC ARNHEM (NL)

T: +31 (0)26 354 2074 / E: info@agri-profocus.nl / www.agri-profocus.nl

Tuesday, September 15, 2015

KILIMO BORA CHA MTAMA

Mtama ni kundi la mbegu ndogo aina ya mazao ya nafaka au nafaka ambayo kwa jina la kisayansi unajulikana kama (Sorghum bicolor), ni mazao yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe Mtama hutoa mazao mengi hata kwenye hali ambayo haifai kwa kilimo cha aina nyingine za mazao ya nafaka. Mtama una uwezo mkubwa wa kustahimili ukame.

Mtama unaweza kutumika kwa kuchemshwa na kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa uji, kutengenezea vinywaji kama vile bia, kuoka mikate, na aina nyinginezo za vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile hay  na sileji. Mtama unastawis vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa milimita 400 – 700 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi.

Mtaama unafaa pia kwa sehemu kame zenye wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto 18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto 25-30°C ili kukua vizuri. Mtama hauwezi kuvumilia barafu. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye chumvi kuliko yalivyo mahindi.

Aina za mtama

Kwa jumla kuna aina zaidi ya 30 za mtama zinazolimwa kama chakula. Mtama hustawi vizuri kwenye joto ikivumilia pia ukame. Hivyo ni nafaka muhimi kwenye maeneo yabisi za Afrika. Katika miaka ya nyuma kilimo chake kiliachwa mara nyingi kwa ajili ya mahindi kwa sababu mahindi huleta mazao makubwa zaidi kwa ekari. Lakini wakati wa ukame mahindi ni hasara na watu hurudi-rudi kwenye kilimo cha mtama.

Aina za mtama zinatofautiana kulingana na rangi zake, kuna nyeupe, nyekundu, na kahawia. Mbegu za asili huwa zinachavushwa kwa urahisi zaidi lakini mavuno yake huwa ni hafifu ukilinganisha na mbegu za kisasa. Hata hivyo, aina za kisasa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi zinapopandwa kwa kufuata kanuni za kilimo bora.

Serena:  Ina punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha kilo 3,000 kwa hekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.

Seredo:  Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha kilo 5000 kwa hekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye majani.

Gadam: Inafanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.

Hakika na Wahi:  Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.

Utayarishaji wa shamba na kupanda

Kwa kawaida mtama hupandwa kwa kutumia mbegu. Mbegu hupandwa shambani moja kwa moja baada ya shamba kuandaliwa, lakini pia zinaweza kurushwa shambani, kasha zikavurugwa pamoja na udongo. Unapaswa kutayarisha shamba la kupanda mtama, iwe ni kwa ajili ya malisho au chakula kabla mvua za msimu hazijaanza. Zao hili hufanya vizuri zaidi kwenye udongo ulio laini. Linaweza pia kupandwa kwenye udongo ambao haukulimwa vizuri na bado ukaota vizuri.

Nafasi:  Mtama unaopandwa kwa ajili ya malisho, unaweza kupandwa kwa nafasi ya sentimita 75×10. Aina za mtama ambazo zinalengwa kwa ajili ya lishe kwa binadamu na wanyama, zinahitaji nafasi kiasi cha sentimita 60×20. Nafasi hutoa mwanya wa kuwa na kiwango kikubwa cha malisho. Mkulima anaweza kupanda mbegu za mtama kiasi cha kilo 2.4-3.3 kwa hekari moja. Ni mara chache sana mbegu hupandwa kwenye vitalu na kuhamishiwa shambani baadaye.

Kupanda:  Mtama hupandwa mvua zinapoanza kunyesha. Mbegu ni lazima zifukiwe ardhini usawa wa sentimita 3 kwenda chini, hii itasaidia kuepuka kuota wakati ambao si msimu kamili wa mvua. Pia zinaweza kufukiwa kiasi cha sentimita 2 wakati ardhi inapokuwa na unyevu. Mtama unahitaji rutuba ya hali ya juu wakati wa kupanda na wakati wa kuota. Ni vizuri kutumia samadi au mboji iliyooza vizuri wakati wa kuandaa shamba.

Mseto:  Unaweza kupanda mtama mseto na mazao jamii ya mikunde, na kuongeza mboji shambani mwako. Hii inaweza kuwa njia nzuri zaidi ya kupata virutubisho vinavyohitajika. Mseto wa mazao jamii ya mikunde inashauriwa iwe ni kama vile maharagwe, kunde, n.k

Uangalizi na utunzaji
Ni lazima kung’oa baadhi ya mimea inapokuwa na urefu wa sentimita 30, au siku 30 baada ya kupanda, ili kuwa na uhakika wa nafasi ya sentimita 10 kati ya mstari na mstari kwa mtama unaokusudiwa kwa ajili ya malisho, na nafasi ya sentimita 20 kati ya mstari kwa mtama uliokusudiwa kwa ajili ya chakula na lishe ya mifugo.

Palizi ya mkono ifanyike walau mara mbili. Shamba la mtama ni lazima liwekwe katika hali ya usafi na kutokuruhusu magugu wakati wote hasa katika kipindi cha mwanzoni.

Monday, September 7, 2015

PATA USHAURI WA BURE KUPITIA SIMU YAKO

Pata ushauri wa bure kuhusiana na kilimo kwa njia ya simu kupitia mtandao wa ushauri kwa wakulima (MUWA). 

MUWA inaratibiwa na mradi wa EPINAV - 'MOBILE FOR IMPROVING AGRICULTURE EXTENSION SERVICE'(http://ushaurikilimo.org/) uliopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

MUWA inawawezesha wakulima kupata ushauri katika mambo mbalimbali yanayohusu kilimo kama vile ukulima, uvunaji, ufugaji wa wanyama, utuzaji wa misitu, maendeleo ya jamii, masoko na msaada wa kiuchumi katika kuendeleza kilimo.


Kama unapenda kupewa ushauri kupitia simu yako ya mkononi unaweza kutuma swali lako kupitia namba 0688099408  na mabwana na mabibi shamba watakujibu mara moja! 


NB: Huduma hii ni bure ila mkulima utalipia gharama ya ujumbe mfupi wa simu kwa kampuni husika ya simu. Mradi utalipia gharama ya ujumbe mfupi wa simu wenye majibu ya swali la mkulima.


TOVUTI: http://ushaurikilimo.org/

 Bofya hapa chini kuona maswali na majibu yaliyokwisha jibiwahttp://ushaurikilimo.org/maswalimajibu.php

Monday, April 27, 2015

JINSI YA KUANDAA MBEGU ZA MITIKI

Hizi ni mbegu kutoka kwa wakala wa mbegu wa taifa (TTSA) wanaopatikana eneo la Kihonda Morogoro Mjini

Nilinunua jumla ya kilo 4 kwenye mifuko ya kilo mojamoja kwa kila mfuko
Nilifungua mifuko yangu na kuweka mbegu zote kwenye kiroba kimoja
Nikaweka mawe ndani ya kiroba ili kukipa uzito utakao nihakikishia mbugu kuzama zitakapo kuwa ndani ya maji
wekw kwemye pipa na utie maji, kilo moja ya maji inahitaji kama lita 20 ambazo utabadilisha kila baada ya masaa 12 yaani asubuhi na jioni kwa muda wa siku 7 kisha utazitoa na kuzianika kwa siku moja kabla ya kuzipanda kwe ye kitalu
video

Tuesday, September 16, 2014

TRACTOR FOR SALE - TREKTA LINAUZWA


t
Tractor Massey Ferguson 3080, 2 wheel drive 90 HP kama mpya inauzwa kwa bei poa sana, na imewasili Tanzania tayari kutoka denmark, (serious buyers only) kwa mawasiliano zaidi  na bei piga 004560248586 au 004553901576

Thursday, May 22, 2014

JINSI YA KUKATA MICHE YA MISOJI (MITIKI) marudio

Hii post niliwahi kuituma siku za nyuma (Friday, March 26, 2010) kutokana na maombi ya baadhi ya wasomaji ninaiweka tena. Kwa kawaida miche ya misoji mara baada ya kutolewa kwenye kitalu huitaji kukatwa, mjasiliamali aliyeko jijini Mwanza aitwae NAYMA aliniomba nimwelekeze kwa picha na mimi bila hiyana nilikwenda shamba na kung,oa mche mmoja na kuukata na kuupiga picha kabla ya kuukata na baada ya kuukata ili kupata kipandikizi

MCHE KABLA YA KUKATWA (angalia mishale kujua sehemu za kukata)


Mche wangu niliukata na kuacha kiasi cha nchi mbili au pingili mbili za vidole kwa sehemu ya juu ya mzizi na kwenye mzizi niliondoa ile sehemu nyembamba ya chini, kwa kawaida hii sehemu ya chini hufa mara baada ya kupandwa kwa sababu sehemu nene/kubwa ya mzizi inayoachwa ndiyo huifadhi maji na chakula cha mmea, nadhani hapa nitakuwa nimemsaidia kama bado nipigie kwenye ile namba niliyokupa

KIPANDIKIZI TAYARI KWA KUPANDWA


Kumbuka wakati wa kupandwa lazima uweke kisahani ili kiweze kukusanya maji kwa ajili ya ukuaji mzuri, kama ni udongo unaotuamisha maji usiweke kisahani bali wekea kama tuta au mwinuko

WEKA KISAHANI KAMA UDONGO HAUTUAMISHI MAJI


WEKA TUTA KAMA UDONGO UNATUAMISHA MAJI

Tuesday, April 29, 2014

UANDAAJI WA MBEGU ZA MITIKI


 Mbegu za mitiki ni lazima ziandaliwe kabla ya kusia kitaluni, hakikisha umeshaanda kitalu chako mapema na kiwe na udongo wenye rutuba ya kutosha, mwagia maji ya kutosha ili kama kuna magugu yaanze kuota na kung'olewa mapema, hii inasaidia kwa sababu mbegu za mitiki huchukua muda mrefu kuota, sasa ukianza kung'olea na mbegu hazijaota au miche ni midogo utakuwa unaing'oa na yenyewe


 Kwa kila kilo moja ya mbegu ina hitaji ndoo ya maji lita 20, weka mbegu zako kwenye gunia au kiroba, kisha weka vitu vizito kama mawe ili kuhakikisha mbegu zako zinakuwa chini ya maji, kinyume na hapo zitaelea juu na hutapata matokeo mazuri katika uotaji, bila kufanya hivi mbegu zko hazitaota kwa wingi

 Hili ni pipa la lita 200, linatosha kwa kilo 10, badilisha maji yako kila jioni na asubuhi kwa muda wa siku 7. kama utaweka maji mara mbili zaidi unaweza kubadilisha maji mara moja kwa siku, yaani kilo moja kwa maji lita 40. Kama kuna maji yanayotembea kama vijito vidogo basi unaweza kuloweka humo bila kuziondoa kwa siku 7.

 Siku ya 8 anika mbegu zako juani, ni vizuri kama utaziweka kwenye bati ili zipasuke gamba lake na kusaidia uotaji

 Panda mbegu zako kwa msitari, chora mfereji wenye kina cha sentimeta moja na uziweke kwenye huo mfereji mwanzo mpaka mwisho bila kuruka nafasi, acha nafasi ya sentimeta 18 - 20 kati ya fereji na mfereji kama inavyoonekena kwenye picha juu na chini


Baada ya wiki tatu mbegu zitaanza kuota na zitaacha kuota baada ya siku 65, uotaji ni kiasi cha  45% mpaka 50%, kilo moja ina wastani wa mbegu 800 mpaka 1000, kwa hiyo unaweza kupata mpaka miche 500 kwa kilo moja, Mbegu zinapatika kwa WAKALA WA MBEGU WA TAIFA kwa bei ya shilingi 9000/= kwa kilo, wanapatikana Morogoro mjini, eneo la Kihonda ukitokea msamvu kama unaelekea Dodoma ni kama kilometa 3, unaweza kupanda daladala, bodaboda au hata taxi na ukafika
Friday, March 28, 2014

TOGGENBURG - AINA BORA YA MBUZI WA MAZIWA


Hii ni aina ya mbuzi wa maziwa ambao asili yake ni uswizi katika eneo la Obertoggenburg kama wanavyoitwa, hii ndio mbegu ya mbuzi wa maziwa wa zamani zaidi kuliko zote. Kwa hapa Tanzania wanapatikana Uyole, SUA na Tengeru (hivi vyote ni vyuo vya mifugo)

UZALISHAJI
Mbuzi hawa wanauwezo wa kuzalisha maziwa wastani wa lita mbili kwa siku au zaidi, hawatoi maziwa mengi kama Saanen ila maziwa yao yana kiasi cha mafuta kati ya 3% - 4%

MAUMBILE
Mbuzi hawa wana umbile la wastani lakini ni wakubwa kuliko mbuzi wa kienyeji, kilo 55 kwa majike na kilo 75 kwa madume, wana rangi ya kahawia (khaki) mpaka hudhurungi (brown)  pia wana mistari miwili usni yenye rangi ya maziwa au nyeupe kuanzia juu mpaka kwenye pua (kama duma) huwa na viwele (udder) vikubwa na pia ni wazazi na walezi wazuri, mara nyingi huweza kuzaa mapacha 

HALI YA HEWA
Mbuzi hawa hawawezi kuhimili hali ya joto, bali hufanya vizuri kwenye maeneo yanye baridi kama mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe, Dodoma, Singida n.k. Wanahitaji chakula chakutosha ili kutoa maziwa mengi, pia chakula kiwe na virutubisho kamili. Ingawa pia wanaweza kuchungwa kwenye maeneo yenye ukame kiasi na wakaweza kufanya vizuri (good foragers)

TABIA
Mbuzi hawa huishi kwa makundi wakitoroka au kuingia kwenye shamba la mazao basi huenda wote na hufundishika kirahisi sana hii husababisha urahisi wa kuwafundisha kukamuliwa na mashine

FAYC KAY TRADING LTD - WAUZAJI WA MATREKTA NA ZANA ZA KILIMO


Hawa ni wajasiliamali wa kiTanzania waishio nchini Denmark, wanauza zana za kilimo zilizotumika (used) kama matrekta na majembe yake, matrailer, irrigation water pumps, Chemicals sprayer, harrows, planters, combining harvesters n.k


Unaweza kuwasiliana nao kwa namba zifuatazo wakiwa Denmark 0004560248586 au 0004527201580 unaweza kuwapigia au kwa kutumia whats up. pia wana email zifuatazo charlesurban00@hotmail.com au sweetfaydat@gmail.comWanazo brand za kimataifa zenye ubora wa hali ya juu kama Massey Ferguson, John Deere, New Holland, Ford na nyinginezi nyingi


Wednesday, March 26, 2014

KILIMO BORA CHA MDALASINI - CINNAMON


Mti wa mita 10 au zaidi. Hutoa machipukizi na kuota miti zaidi ya mmoja kwenye shina moja na kuongeza mavuno mengi, haya mashina mapya yasing'olewe bali yaachwe yakue na kuwa mti mkubwa.

AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)

HALI YA HEWA NA UDONGO
· Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
· Udongo wenye rutuba
· Joto kwa wingi
· Hewa yenye unyevunyevu

KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
· Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
· Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
· Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
· Panda miche wakati wa masika
· Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka

UTUNZAJI
· Acha machipukizi kwenye shina
· Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
· Weka shamba katika hali ya safi
· Zuia magonjwa kama.
- Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.

KUVUNA
· Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
· Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
· Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
· Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
· Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
· Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
· 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
· Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini

MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
· Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
· Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
· Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
· Dawa ya ngozi

JINSI YA KUTUMIA
· kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk
· Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula

MANUFAA
· Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
· Gharama ndogo ya uzalishaji
· Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
· Magonjwa na wadudu ni kidogo
· Rahisi kuchanganya na mazao mengine
· Nguvu kidogo, kipato kikubwa.

Thursday, December 19, 2013

NDIKANA KALI - EAST COAST FEVER

Ugonjwa huu hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi na kondoo na husababishwa na vimelea vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo vusambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanavyo kama Rhepicephalus Appendiculatus, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine


KUPE WEKUNDU KWENYE MASIKIO YA NG'OMBE

DALILI ZA UGONJWA HUU
Homa kali, mnyama kushindwa kupumua vizuri,  kukohoa pamoja na kutoa makamasi, kuharisha na kuvimba matezi

MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za  PARVAQUONE au BUTALEX kiasi cha ml 20 (soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada  ya siku moja kupita, yaani ukuchoma leo unarudia dozi kesho kutwa, pia mnyama achomwe dawa ya OTC20% kipindi chote cha matibabuKINGA
Kinga kubwa ya ugonjwa huu ni kuhakikisha kwamba mifugo yako inaoga mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo

NG'OMBE WAKIOGESHWA KWENYE DAWA

KUPUNGUZIA MATAWI MITI YA MITIKI - PRUNING TEAK TREES

 

Umuhimu wa zoezi hili ni kuhakkisha miti yako inanyooka, kukua kwa haraka na kuwa na mbao bora, miti inapokuwa na matawi haikui kwa haraka maana chakula kinagawanywa pamoja na matawi, lakini kama mti hauna matawi mengi basi hunenepa na kurefuka kwa haraka, pia kwa kuondoa matawi yakiwa machanga unoaongeza ubora wa mbao maana hazitakuwa na vidonda vinavyo sababishwa na matawi

Tuesday, November 26, 2013

IVOMEC / IVERMECTIN

Hii ni dawa inayukuja na majina kadhaa kama Ivomec, Ivermectin, Zimectin, Iverhart au Tri-heart kutegemea na iana ya mtengenezaji wa dawa hii.


 Dawa hii imeonesha mfanikio makuwa katika kupambana na minyoo duara, minyoo bata, minyoo ya moyo, viroboto na ukurutu.Dawa hii huweza kutumika kwenye wanyama kama Mbuzi, Ng'ombe na Nguruwe na kutokomeza kabisa minyoo, ukurutu na hata kuua viroboto wanaonyonya damu kwenye wanyama hawa.


Dawa hii pia huweza kuja katika namna mbali mbali za matumizi kama sindano (injectable), ya kunywa (oral drench) na ya kupaka (pour/spot on) na mfugaji anaweza kuamua kununua kwa kadri ya mahitaji yake, urahisi au namna anavyopendelea yeye

Kwa njia ya sindano hupigwa chini ya ngozi (subcutaneous) ambapo kwa Ng'ombe na Mbuzi unaweza kupiga mahala popote ila kwa Nguruwe inapigwa nyuma ya sikio sababu ndio sehemu pekee mbayo haina mafuta