KURASA

Tuesday, January 24, 2017

SALT WATER SHRIMPS












Hi kaka Bennet habari za siku na pirika za hapa na pale Ben naomba msaada wako katika kujipanga nimejaribu kufunguwa mradi wa shrimp farms tatizo linalonikabili hadi hivi sasa nimekosa vifaranga wa kamba ambao nimejaribu kufatiliya DAR muhusika ambaye anauza amesafiri JEE WAPI NAWEZA KUWAPATA SALT SHRIMP aina yoyote naomba unipatiye tel no ya wahusika kila pond lina ukubwa wa haktar 1 jee naweza kuhitaji vifaranga wangapi kila pond najaribu kaka ben wapi naweza kupata chakula cha kuwalisha ?jee naweza kuwalisha cha kuku ? pole kwa usumbufu

CHAKULA CHA SUNGURA

Tunafuga na Kuuza Mayai ya Kuchi na Bata Mzinga . Pia tunauza bata Kwa Wakulima bei inapungua akinunua wengi. Tunaweza kutoa 100 Kwa mwezi!  
Tuna Shamba la Sungura wa Nyama. Tunazalisha na Kuuza Mbegu ya Sungura wa Nyama.
Dr swai . Box 6448, Moshi . 0784 29 08 08 : eliafieswai@gmail.com





KUKATA PEMBE NA KUZUIA PEMBE KUOTA

Mnyama asiye na pembe hasa ng’ombe hupunguza uwezekano wa wanyama kuumizana na hata kuwadhuru binadamu, wanyama wadogo kama miezi miwili hadi mitatu ni vizuri wakachomwa ili kuzuia pembe kuota (disbudding) lakini kama pembe zimetokeza hamna jinsi ila kuzikata kwa kutumia msumeno au waya maalum (phatetomi wire)

Zoezi la kuzuia pembe kuota hufanyika kwa kutumia vyuma maalum (disbudding iron) ambavyo hupashwa moto na kuwa vyekundu, ndama huandaliwa kwa kulazwa chini na kisha kupunguzwa manyoya sehemu itakayochomwa ambapo ni pale pembe zinakoota, unaweza kuitambua sehemu hii kwa kupapasa na utaona kama pembe ndogo ndani ya ngozi. Sehemu husika isafishwe kwa spirit au eusol kabla ya zoezi kuanza.

Mtaalamu wa mifugo ndiye atakaye fanya zoezi hili kwa kufuata kanuni za kitaalam, kabla ya kuanza zoezi ni muhimu mnyama kupigwa sindano ya ganzi, kisha sehemu husika huchomwa na chuma cha moto, na chuma kuzungushwa kila upande na mwisho kama anazibua ataondoa kile kipande kinachoota na kumalizia kwa kukausha sehemu iliyobaki kwa kutumia chuma kile kile, baada ya hapo dawa za kupulizia za vidonda, iodine tincture au dawa za kufukuza wadudu hupakwa sehemu husika na mnyama huachiwa huru

Kuhusu ukataji wa pembe ambayo imeshaota, baada ya mnyama kufungwa na kulazwa chini huchomwa ganzi na ukataji huanza. Kama utatumia msumeno lazima damu nyingi itatoka, zuia damu hii kwa kuunguza sehemu ndogo ya pembe iliyobaki kwa kuichoma na disbudding iron au chuma chochote cha moto. Inashauriwa kutumia phatetomi wire kwa sababu wakati unakata pembe waya huu huunguza pembe na kufanya damu isitoke kabisa.

Kuna baadhi ya aina za ngombe wa kisasa hazina pembe kabisa mfano Hereford na mbegu kama Friesian baadhi yao huwa hawana pembe, kwa mbegu za kienyeji kama zebu (SHZ)huwa na pembe fupi fupi