Hii ni njia inayotumika kumuandaa mnyama kabla ya kuchinjwa, nia kuu ya stuning ni kumpunguzia mnyama maumivu wakati wa kuchinjwa, pia huondoa uwezekano wa mnyama kumuumiza mchinjaji na mwisho ni kuongeza ubora wa nyama.
Zipo njia nyingi au vifaa vingi vya kumuandaa mnyama kabla ya kuchinjwa lakini leo nitaongelea kifaa kijulikana cho kitaalam kama CAPTIVE BOLT PISTOL/GUN. Hiki ni kifaa kama bunduki ndogo ambapo ndani huwekwa baruti maalum au hutumia nguvu ya upepo ambayo ukifyatua kuna chuma imara chenye ncha kali mbele (bolt)kina toka mara moja na kurudi ndani.
Boriti hii inakazi moja tu ya kutoboa sehemu ya mbele ya ubongo wa mnyama na kumfanya abung'ae na kupoteza fahamu, hii hurahisisha zoezi la uchinjaji na kufanya mnyama achinjwe bila kusikia maumivu yoyote. Kila mnyama anasehemu maalum ya kufanya stunning kama inavyoonyeshwa hapo kwenye michoro ya makala hii
http://www.youtube.com/watch?v=nr00arV2XIw kwenye link hii ya you tube unaweza kuona jinsi zoezi hili linavyofanyika kwa kutumia mashine maalum ya upepo