KURASA

Thursday, August 23, 2012

SILAGE - CHAKULA BORA CHA MIFUGO WAKATI WA KIANGAZI

Silage ni chakula maalum kinachotengenezwa kwa kutumia aina yoyote ya malisho yanayofaa kwa mifugo kama majani, nyasi, mabua ya mahindi, mtama na ufuta. Kwa kawaida silage hutengenezwa wakati wa mvua ambapo majani hukua kwa haraka na kukatwa tena na tena mpaka kiangazi kitakapoanza, kama una shamba binafsi la majani ya napier unaweza ukawa unayaka kila baada ya wiki sita katika kipindi cha mvua. Silage utokea baada ya majani kuozeshwa na vimelea katika mfumo usiotumia oxijeni (anaerobic fermentation)

VIFAA
1- Majani na mabua kama chakula cha mifugo
2- Molasses ambayo hupatikana kwenye viwanda nya miwa
3- Panga au mashine ya kukata kata majani
4- Maji
5- Mfuko mkubwa mweusi wa plastiki au shimo liliojengewa kuta zake

NAMNA YA KUTENGENEZA SILAGE
1- Katakata malisho yako katika vipande vidogo vodogo kwa kutumia panga au mashine maalum.
2- Changanya molasses kiasi cha kila lita moja kwa lita mbili za maji au lita mbili na nusu za maji kama malisho ni makavu kiasi na lita tatu za maji kama malisho ni makavu zaidi
3- Changanya mchanganyiko wa maji na molasses pamoja na malisho kiasi malisho yako yalowane kisasi tu
4- Weka kwenye mfuko wako au kwenye shimo lililo jengewa na shindilia vizuri
5- Funga vizuri mfuko wako na uuweke mahali pasipo na jua
6- Kama unatuma shimo lililojengewa lifunike vizuri na plastiki na unaweza kuweka udongo kiasi juu yake
7- Hakikisha kwamba hamna hewa inayoopenya kwenye mchanganyiko wako

SILAGE ILIYOTENGENEZWA KWENYE DUMU LA PLASTIKI



MATUMIZI
Silage huwa tayari baada ya miezi 3 - 4 kutegemeana na aina ya malisho yaliyotumika, umri wa malisho, ubora wa uchanganyaji na mengineyo. Baada ya kuwa tayari unaweza kuanza kulisha mifugo yako silage uliyotengeneza wakati wa mvua nyingi, silage inauwezo wa kukaa hadi miaka minne tangu kuanza kutengenezwa kwake

FAIDA
1- Hupunguza tatizo la chakula wakati wa kiangazi
2- Huongeza utoaji wa maziwa wakati wa kiangazi
3- Mifugo huwa na afya bora hata wakati wa jua kali na malisho duni
4- Mifugo yenye afya bora huzaliana vizuri wakati wote
5- hupunguza gharana ya mashudu kwani silage ina virutubisho vingi
6- Mayai ya minyoo hufa wakati wa kutengeneza silage