Huu ni ugonjwa wa mifugo unaoshambulia ng'ombe, kondoo na mara chache farasi. Unasababishwa na vijidudu ina ya Clostridium chauvoei ambavyo hushambulia bila uwepo wa oksijeni ya kutosha (anaerobic) na kuzalisha sumu kwenye mwili wa myama na kusababisha kifo.
KUSAMBAA
Vijidudu husambaa kwa kupitia kwenye udongo ambapo mnyama huvipata anapokula majani, pia huweza kusambazwa kwa njia ya vidonda na mate toka kwa mnyama mwenye ugonjwa huu.
DALILI
-homa kali
-Misuli ya miguu ya nyuma huvimba na kuwa na joto kali, inauma ikiguswa na rangi ya sehemu hiyo ya ngozi hubadilika
-Ukigusa sehemu iliyoshambuliwa inatoa sauti ya kama majani makavu
-Mnayama huchechemea mguu wa nyuma sababu ya maumivu
UCHUNGUZI
Uchunguzi ufanyike na maafisa ugani wa mifugo kwa kufuatilia dalili na historia ya sehemu husika
-Kipande cha msuli na majimaji toka sehemu iliyoathiriwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara
-Uchunguzi wa mwili wa myama aliyefariki (post Mortem)
MATIBABU
-Penicilin inasaidia kutibu ugonjwa kama matibabu yataanza katika hatua za mwazo, ukichelewa hutaweza kmtibu mnyama wako.
-Tumia b-complex, na dawa za kupunguza uvimbe kama visaidizi vya tiba
-Kupachana sehemu iliyoathirika ilikutoa majimaji na kuingiza hewa ili kuharibu mazingira ya kuishi vijidudu
KINGA
-Chanjo ya mara moja kwa mwaka kwa wanyama wakubwa.
-Wanyama wadogo wachanjwe mara wafikishapo umri wa miezi mitatu
-kwa sehemu ambayo kuna mlipuko wa ugonjwa huu wanyama wote wachanjwe kisha wapigwe dozi kubwa ya penicilin (kama ugonjwa hautaibuka ndani ya siku 14 wanyama wako watakuwa salama)
-Miili ya wanyama walikufa ichomwe na kuzikwa kwenye shimo refu sana