Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyofanana sana na vile vinavyosababisha surua kwa binandamu, distemper hushambulia wanyama jamii ya mbwa
(canine) kana simba, mbwa mwitu, fisi, mbweha na mbwa wa kawaida tunaowafua majumbani mwetu. Huu no ugonjwa unaoua zaidi mbwa duniani ingawa hapa nchini haujasababisha madhara makubwa kama kichaa cha mbwa
(rabies)
Mbwa aliambukizwa ugonjwa huu hutoa virusi hivi kwa njia ya kinyesi, mkojo, mafua na chafya na njia ya hewa ndio njia kuu ya kusambaza ugonjwa huu kwenda kwa mbwa wengine. Maabukizi makubwa zaidi ni kwenye watoto wasiochanjwa ambao wenye umri kati ya wiki
6 - 12 ambapo kinga toka kwa mama waliyozaliwa nayo hupungua sana na kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi.
Mbwa walioambukizwa ugonjwa huu nusu yao wataonyesha dalili kidogo sana au wasionyeshe dalili za ugonjwa huu kabisa na wanaoathirika zaidi ni mbwa ambao hawapati lishe bora na kuwekwa kwenye mazingira mazuri na afya kwa ujumla.Virusi vya ugonjwa huu hushambulia ubongo, sehemu za ndani ya ngozi, macho na utando wa mfumo wa hewa na chakula na dalili za wazi huweza kuonekana baada ya siku
6 - 9 tangu kupata maambukizi
Hatua ya kwanza ya ugonjwa huu joto hupanda kufikia sentigredi
39.4 - 40.5 mbwa hupoteza hamu ya kula, hutoa machozi na majimaji puani, lakini dalili hizi ni kama za ugonjwa wa kawaida wa mafua
(colds) kwenye mbwa kwa hiyo zinaweza kukuchanganya kidogo. baada ya siku chache macho huwa na matongo tongo na sio machozi tena na puani atatoa makamasi mazito na sio majimaji tena, mbwa huwa na kikohozi kikavu, hutapika, kuharisha na hii husababisha upungufu wa maji mwilini. ndani ya wiki moja au zaidi mbwa ataonekana kupata nafuu na hii hutokea zaidi kwa mbwa waliotibiwa na dawa za antibaiotiki kama
OTC na Gentamycin, lakini hali hubadilika baada ya mashambulizi ya juu kutokea kwenye njia ya hewa na mfumo wa chakula
Hatua ya pili ni baada ya wiki mbili au tatu mbwa wengi wataonyesha dalili za magonjwa ya akili, kushambulia ghafla, kutingisha kichwa, kutafuna kama vile anatafuna bazoka/chewing gum, kukimbia kwa kujizungusha mduara na kuanguka chini, kupiga mateke miguu yote minne, kuona aibu na wakati mwingine anakua haoni vitu vizuri sababu ya kushambuliwa macho. Dalili nyingine ni kuvimba kwa pua na nyayo za mbwa ingawa hii haitokei sana
MATIBABU
Matibabu yanakuwa ya uhakika zaidi kama mbwa atatibiwa mapema wakati wa dalili za mwanzo kabisa, antibaiotiks husaidia sana kupunguza mashambulizi ya juu (secondary infections) ingawa hazitaua virusi vinavyosababisha ugonjwa huu, Mbwa pia watahitaji drip ya maji ili kufidia upungufu mkubwa wa maji uliosababishwa na kutapika/kuharisha, pia apewe dawa za kuzuia kuharisha na kutapika pamoja na dawa za usingizi ili apumzishe ubongo wake vya kutosha
KINGA
Hii ndio njia sahihi ya kupambana na ugonjwa huu, siku hizi kuna chanjo moja kwa ajili ya magonjwa manne
DHPP (distemper, hepatitis, parvovirus, and parainfluenza combination) ambapo chanjo hii wapigwe watoto wa mbwa kabla ya kufikisha wiki 8 toka wazaliwe au wapigwe kabla kama mama yao hakuchanjwa kabisa