Hii ni dawa inayukuja na majina kadhaa kama Ivomec, Ivermectin, Zimectin, Iverhart au Tri-heart kutegemea na iana ya mtengenezaji wa dawa hii.
Dawa hii imeonesha mfanikio makuwa katika kupambana na minyoo duara, minyoo bata, minyoo ya moyo, viroboto na ukurutu.Dawa hii huweza kutumika kwenye wanyama kama Mbuzi, Ng'ombe na
Nguruwe na kutokomeza kabisa minyoo, ukurutu na hata kuua viroboto
wanaonyonya damu kwenye wanyama hawa.
Dawa hii pia huweza kuja katika namna mbali mbali za matumizi kama sindano (injectable), ya kunywa (oral drench) na ya kupaka (pour/spot on) na mfugaji anaweza kuamua kununua kwa kadri ya mahitaji yake, urahisi au namna anavyopendelea yeye
Kwa njia ya sindano hupigwa chini ya ngozi (subcutaneous) ambapo kwa Ng'ombe na Mbuzi unaweza kupiga mahala popote ila kwa Nguruwe inapigwa nyuma ya sikio sababu ndio sehemu pekee mbayo haina mafuta
Karibuni kwenye blog yangu ambayo najaribu kutoa elimu kidogo niliyo nayo. Kama unataka kufanya kilimo, ufugaji wanyama, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki, kilimo cha miti ya mbao, kilimo cha majani na malisho ya mifugo, utaalamu wa mbolea na udongo katika mazingira halisi ya ki Tanzania basi wasiliana nami (mitiki1000@gmail.com) NB sihusiki na habari za masoko ya bidhaa yoyote ya kilimo na mifugo, kabla hujaingia kwenye mradi fanya utafiti wa masoko wewe mwenyewe
Tuesday, November 26, 2013
Friday, November 22, 2013
Friday, November 15, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)