KURASA

Tuesday, April 29, 2014

UANDAAJI WA MBEGU ZA MITIKI


 Mbegu za mitiki ni lazima ziandaliwe kabla ya kusia kitaluni, hakikisha umeshaanda kitalu chako mapema na kiwe na udongo wenye rutuba ya kutosha, mwagia maji ya kutosha ili kama kuna magugu yaanze kuota na kung'olewa mapema, hii inasaidia kwa sababu mbegu za mitiki huchukua muda mrefu kuota, sasa ukianza kung'olea na mbegu hazijaota au miche ni midogo utakuwa unaing'oa na yenyewe


 Kwa kila kilo moja ya mbegu ina hitaji ndoo ya maji lita 20, weka mbegu zako kwenye gunia au kiroba, kisha weka vitu vizito kama mawe ili kuhakikisha mbegu zako zinakuwa chini ya maji, kinyume na hapo zitaelea juu na hutapata matokeo mazuri katika uotaji, bila kufanya hivi mbegu zko hazitaota kwa wingi

 Hili ni pipa la lita 200, linatosha kwa kilo 10, badilisha maji yako kila jioni na asubuhi kwa muda wa siku 7. kama utaweka maji mara mbili zaidi unaweza kubadilisha maji mara moja kwa siku, yaani kilo moja kwa maji lita 40. Kama kuna maji yanayotembea kama vijito vidogo basi unaweza kuloweka humo bila kuziondoa kwa siku 7.

 Siku ya 8 anika mbegu zako juani, ni vizuri kama utaziweka kwenye bati ili zipasuke gamba lake na kusaidia uotaji

 Panda mbegu zako kwa msitari, chora mfereji wenye kina cha sentimeta moja na uziweke kwenye huo mfereji mwanzo mpaka mwisho bila kuruka nafasi, acha nafasi ya sentimeta 18 - 20 kati ya fereji na mfereji kama inavyoonekena kwenye picha juu na chini


Baada ya wiki tatu mbegu zitaanza kuota na zitaacha kuota baada ya siku 65, uotaji ni kiasi cha  45% mpaka 50%, kilo moja ina wastani wa mbegu 800 mpaka 1000, kwa hiyo unaweza kupata mpaka miche 500 kwa kilo moja, Mbegu zinapatika kwa WAKALA WA MBEGU WA TAIFA kwa bei ya shilingi 9000/= kwa kilo, wanapatikana Morogoro mjini, eneo la Kihonda ukitokea msamvu kama unaelekea Dodoma ni kama kilometa 3, unaweza kupanda daladala, bodaboda au hata taxi na ukafika